MBINU ZA KUFUNDISHA KUSOMA NA KUANDIKA

Download Report

Transcript MBINU ZA KUFUNDISHA KUSOMA NA KUANDIKA

MBINU ZA KUFUNDISHA
KUSOMA NA KUANDIKA
Ni uwezo wa kuelewa maana maandishi au
maumbo yaliyoandikwa. Msomaji anatumia
maumbo na kugundua taarifa katika
kumbukumbu zake na kutumia taarifa hizi
kujenga tafsiri ya ujumbe wa mwandishi.
 (Mitchell 1982:1 katika Clapham Caroline,1993)
 Usomaji unahusishwa na process ya kutambua
maumbo na kuyapatia maana/kuyafahamu
 Kunahusisha kuona kutamka na kupata maana.
(linear process)
 Inahusisha akili na mwili(metal and physical
activity)

 Ni
muhimu kujifunza kusomakwa sababu
kunapelekea uwezo wa kusoma kwa haraka
na kwa usahihi.
 kusoma kiusahihi kunapelekea kupata taarifa
za uhakika kinyume chake kusoma kimakosa
kunapelekea kupata taarifa zisizo sahihi.
 Kusoma harakaharaka kunaharakisha kupata
taarifa na kidogo kidogo kunachelewesha
kupata taarifa.
 kusoma
kwa kufahamu (lengo ni kuelewa
ujumbe unaokusudiwa katika habari)
 Kusoma kwa mazoezi (lengo ni kumpa
mwanafunzi mazoezi ya kusoma, uwezo wa
kusoma bila ya kudodosa na kwa kuzingatia
vituo)
 ZIPO
HATUA TATU ZA UFUNDISHAJI KUSOMA
 Kabla ya kusoma (pre -reading)
 Wakati wa kusoma (while reading)
 Baada ya kusoma (after reading)
 Kabla
ya kusoma habari aliyoikusudia
mwalimu kwa wanafunzi, mwalimu
anatakiwa awaulize wanafunzi maswali ya
jumla juu ya mada kwa kuwaweka tayari juu
ya kinachokuja, na kuangalia maarifa yao
makongwe kwa ajili ya kuyaunganisha na
maarifa mapya.
 Katika hatua hii pia mwalimu anaweza
kutumia picha inayohusiana na maudhui ya
habari na kuwauliza maswali wanafunzi
kuhusu picha hio.
 Lengo
ni kuwajengea maarifa wanafunzi juu
ya maudhui ya habari.
 Katika hatua hii mwalimu anaweza kuuliza
maswali yanayohitaji jawabu za moja kwa
moja
 Hiki ni nini? Anafanya nini? Au ya kuwataka
wanafunzi wafikiri mf. unafikiri nini kuhusu
picha hii, nini maana ya... faida ....,
unafikiri nini kinaweza kufanywa ili....
 Hapa
mwalimu anaweza kusoma habari kwa
sauti mara moja tu na baadae kuwaachia
wanafunzi wasome wenyewe kimya kimya (
lengo ni kusoma kwa kufahamu , hivyo
haipendelewi kutoa sauti)
 Misamiati iwe imeshafafanuliwa kabla ya
hatua ya kuanza kusoma na itolewe maana
kwa mahitaji ya habari tu.
 Maneno mapya yasizidi matatu kwa
wanafunzi wadogo na sita kwa wanafunzi
wakubwa
 Katika
hatua hii mwalimu awaulize
wanafunzi maswali yanayopima ufahamu wao
wa habari
 Maswali yaanze kwa kuangalia ufahamu wa
kila aya. Mf aya ya kwanza inazungumzia
nini,wahusika gani, vitu,gani sehemu, nk
(skanning quetions)
 Mwalimu
aulize maswali yatakayotofautiana
na ya mwanzo mf wa maswali yanayohitaji
kufikiri, kuchambua, kutoa mawazo, nk.
 Mf unafikiri kwa nini alifanya..., kama wewe
ungefanya nini? Ungetoa uamuzi gani,
unawashauri nini watu wa ina hii...,unahisi
kwa nini serikali ilitoa uamuzi huu
ule...unafikiri mwandishi wa habari hii
amekusudia nini..nk (skimming questions)

MVUA KUBWA
Siku moja wakati wa masika, baada ya mvua kunyesha, sisi sote
tulikuwa tukifanya kazi kama kawaida. Mara tulisikia ngurumo ya
kutisha kutoka upande wa mti wetu. Tulishtuka na kutazamana.
Mara tuliona miti mirefu iliyokuwa karibu nasi ikianguka mmoja
mmoja kama migomba iliyoshindana na upepo kwa muda mrefu.
Tulipigwa na bumbuazi!

Katika patashika hiyo, tulijikuta tumefika mtoni. Loo! Mto
ulikuwa jito. Maji yaliyojaa matope yalikuwa yanakwenda kwa
kasi mithili ya umeme. Yalichukua kila kitu kilichokuwa njiani
mwake. Miti minene sana na mirefu nayo ikang’olewa kwa nguvu
za maji. Majabali makubwa yakaviringishwa na kutupiliwa mbali.

Baada ya hayo yote ndipo tulitanabahi kuwa tulikuwa
tumejitumbukiza katika hatari. Tulikimbia haraka na kurudi
tulikokuwa mwanzoni. Hii ilikuwa gharika ambayo hatukujua
chanzo chake.
 Kuandika
ni stadi muhimu sana katika stadi
za lugha.
 Uandishi unampa fursa mwanafunzi ya
kutumia stadi mbali mbali alizojifunza mf
katika kutumia misamiati, sarufi, taratíbu za
uandishi nk
 Unamwezesha mwanafunzi kutumia akili
katika kufikiri na kupanga hoja.
 Hivyo, uwezo wa kuandika unatambulisha
uwezo wa lugha alionao mwanafunzi katika
kujieleza na kueleweka.
 Ufunuo
(ni uandishi unaozungumzia taarifa
za ukweli mf,jografia, historia,sayansi,
lugha, nkn)
 Ubunifu (ni ubunifu wa tukio au jambo
ambalo si la kweli na kulifanya lionekane la
kweli kwa namna ya matumizi ya lugha na
ufundi mwengine mf kazi za fasihi)
 Ushawishi ( ni uandishi wa kumvutia msomaji
mf barua, risala)
Mwalimu anaweza kutumia mbinu ya vielelezo
kuwasaidia wanafunzi kupata uwezo wa
kuandika.
 Vielelezo vinaweza kuwa mfano wa barua,
hotuba, insha, nk.
 pia uandishi unaweza kufundiswa kwa kuzingatia
kanuni za kitu amacho kinafundishwa mfano
barua risala, insha. nk.
 Mwalimu kwa kusaidiana na wanafunzi anaweza
kuwauliza maswali juu ya muundo wa uandishi
fulani na baadae kuandika ubaoni.
 Inategemewa wanafunzi waone muundo huo
ubaoni baada ya majadiliano na maswali.

Anuani
Tarehe
Maamkizi (baba mpendwa)
Salaamu (Nategemea upo....
Taarifa (lengo la barua hii ni...
Kifungio ( nisalimie...
Jina la mwandishi (mwanao mpendwa...






Wanafunzi wazione kanuni waziwazi ubaoni na mfano
wa matumizi ya kanuni hizo.
Mbinu nyengine ya kufundisha uandishi ni ya kutumia
mazingira
Hapa mwanafunzi anapewa mazingira ya kuandika
kazi na hivyo kumfanya agundue sheria mwenyewe
na kutengeneza kielelezo mwenyewe.
Mfano unaweza kumpa mazingira kuandika barua ya
kuomba kazi mwambie yeye ni nani anaomba kwa
nani, anaomba nini, ana sifa gani, n.k.
Au aandike hotuba yeye ni nani, anahutubia nani,
nini, anategemea nini. nk
Mbinu hii inapendekezwa zaidi kwa wanafunzi
wakubwa.
 Mbinu
yoyote itakayotumika kuwe na muda
wa wanafunzi kufanya mazoezi ya kuandika
darasani.
 Wanafunzi wapewe kazi nyengine juu ya aina
ya utungaji waliousoma na waandike darasani
 Wanaweza kuandika kwa vikundi , au kila
kikundi na aya yake
 baadae kazi hizo zisomwe na kusahihishwa
kwa pamoja darasani