ufundishaji wa msamiati

Download Report

Transcript ufundishaji wa msamiati

UFUNDISHAJI WA MSAMIATI
KISWAHILI TEACHING METHODS
NINI MAANA YA MSAMIATI






Msamiati unajumuisha maneno katika maandishi au
mazungumzo.
Kuelewa msamiati ni njia moja ya kuendeleza kiwango cha
lugha, ni sehemu ya ukuzaji wa lugha.
Ni kipengele cha lugha kinachopelekea kukuza uwezo wa
kuzungumza, kuandika na kusoma kwa ufasaha.
Ufundishaji wa msamiati unategemea sana stadi ya kusoma
kwa ufahamu.
Katika ufundishaji wa msamiati inazingatiwa uwezo wa
kutambua maumbo ya maandishi na kupata maana yake.
Lengo kuu la kufundisha msamiati ni kupata maana yake na
kutumia maana hiyo katika mazingira mbali mbali.
NJIA MBALI MBALI ZA KUPATA MAANA YA
MSAMIATI
Kupata maana ya neno kufuatana na neno
lilivyotumiwa katika sentensi au kifungu
kilichosomwa.
 Kuangalia maana ya neno lilisomwa katika
mazingira mengine mbali mbali (neno moja
linaweza kuwa na maana zaidi ya moja)
 Maana ya neno inaweza kutokana na muundo
wake. Hivyo kuchunguza au kuchambua
muundo wa neno ni muhimu. (kuna baadhi ya
maneno yameundwa kwa kuambatanisha
maneno mawili mf mwanahewa, nyamafu,…nk)

INAEND.
•Njia ya muambatano au kujirudiarudia mf polepole, barabara,
chezacheza, nk
•Uchambuzi wa shina la neno mf kata, katika, katisha, kateni,
katwa,…
•Kutumia picha,kitu halisi, kuigiza, kuangalia katika kamusi,
kupata ufafanuzi,
•Kwa kujua kinyume cha neno
•Maneno yanayotokana na lugha ya kigeni.
NAMNA YA KUFUNDISHA

Wanafunzi waone msamiati utakaofundishwa kwa kuorodheshwa
au kwa kusoma sentensi au vifungu vya habari vyenye msamiati
huo. ( lengo ni kutambua maneno hayo na kuona kiasi ambacho
wanafunzi wanayafahamu)

Kupata maana ya maneno kutokana na njia mbali mbali ambazo
zinafaa kwa mazingira ya wakati huo.(unaweza kutumia njia zaidi
ya moja mf, kinyume, ufafanuzi, nk mfano neno: ubora,
ukakamavu, nk.

Kutoa mifano kudhihirisha maana iliyopatikana pamoja na
matumizi mengine ya maneno hayo .


Mazoezi mbali mbali ya kupima uelewaji wake. Kuuliza maswali,
kuwapa sentensi nyengine kuona wameelewa vipi,nk.
INAEND.

Mazoezi ya kufundisha msamiati uliomo katika
habari ifuatayo
MVUA KUBWA
Siku moja wakati wa masika, baada ya mvua kunyesha, sisi sote tulikuwa tukifanya kazi
kama kawaida. Mara tulisikia ngurumo ya kutisha kutoka upande wa mti wetu.
Tulishtuka na kutazamana. Mara tuliona miti mirefu iliyokuwa karibu nasi ikianguka
mmoja mmoja kama migomba iliyoshindana na upepo kwa muda mrefu. Tulipigwa
na bumbuazi!
Katika patashika hiyo, tulijikuta tumefika mtoni. Loo! Mto ulikuwa jito. Maji yaliyojaa
matope yalikuwa yanakwenda kwa kasi mithili ya umeme. Yalichukua kila kitu
kilichokuwa njiani mwake. Miti minene sana na mirefu nayo ikang’olewa kwa nguvu
za maji. Majabali makubwa yakaviringishwa na kutupiliwa mbali.
Baada ya hayo yote ndipo tulitanabahi kuwa tulikuwa tumejitumbukiza katika hatari.
Tulikimbia haraka na kurudi tulikokuwa mwanzoni. Hii ilikuwa gharika ambayo
hatukujua chanzo chake.
(Kutoka, Kiswahili 1, Kidato cha Kwanza, Taasisi ya Elimu, Oxford University Press, Dar
Es Salaam, 1996, uk 48.)