Uzazi wa mpango

Download Report

Transcript Uzazi wa mpango

Uzazi wa mpango
Maana ya uzazi wa mpango
Ni uamuzi wa mtu binafsi au mtu na
mwenza, wa lini wazae, watoto wangapi
kufuatana na uwezo na mahitaji yao, na
watoto wapishane muda gani ( ili mradi
isiwe chini ya miaka miwili kwa kutumia
njia za uzazi wa mpango walizochagua.
Sera ya uzazi wa mpango tanzania
• Mtu yeyote mwenye uwezo wa kupata au
kusababisha mimba ‘Ana haki ya kupata
huduma za uzazi wa mpango
• Kijana balehe ambaye anakiri kuanza
kujamiiana ana haki sawa na watu
wengine kupata huduma hizi
Sababu / umuhimu wa uzazi wa mpango
•
•
•
•
Sababu za kiafya
Sababu za kiuchumi
Haki ya binadamu
Maambukizi ya vvu
Faida za uzazi wa mpango
Mama:
• Atapona vizuri baada ya kujifungua
• Atawahudumia vizuri watoto na familia
• Atapata muda wa kufanya shughuli
zingine za kuongeza kipato
• Atapata muda wa kushiriki shughuli za
maendeleo
Faida kwa Baba
• Atafanya kazi kwa amani
• Anakuwa na uhakika wa kipato na vitu vya
kuridhisha watoto wake
• Anakuwa na uwezo wa kuwapatia watoto
mahitaji ya msingi kama shule, chakula,
nguo nk.
• Anapata muda wa kushiriki shughuli za
kijamii
• Anaweza kujiwekea akiba
Faida kwa mtoto
• Anapata muda mrefu wa kunyonya na
hivyo kutopata utapia mlo au magonjwa
hivyo hukua vizuri na afya njema
• Hupata upendo mkubwa toka kwa wazazi
na familia yake
• Hupata huduma zote muhimu na
kuwekewa mipango ya maendeleo ya
baadaye
Faida kwa jamii
•
•
•
•
•
Kuboreka kwa huduma za shule
Kutokuwepo msongamano katika kliniki
Huduma za kijamii huboreka
Rasilimali zitaendana na idadi za watu
Kupungua kwa watoto yatima
Aina za njia za uzazi wa mpango kwa vijana
•
•
•
•
•
Vidonge vya kumeza
Njia za dharura za kuzuia mimba
Njia ya sindano
Vipandikizi
Kondomu za kiume na kike
Semi na vumi potovu kuhusu njia za uzazi
wa mpango
Kazi za vikundi
Orodhesha semi na vumi potovu kuhusu
njia za uzazi wa mpango
Njia za uzazi wa mpango ni salama kutumia,
kwani zimefanjiwa utafiti wa kina na
kuhakikisha kuwa zinafaa.
Kama dawa zingine maudhi madogo
madogo huweza kutokea ambayo huisha
baada ya muda mfupi
AHSANTE
Magonjwa ya ngono
Nini maana ya magonjwa ya ngono?
Ni magonjwa yatokanayo kwa mtu
kujamiiana na mtu mwenye ugonjwa huo
bila kinga
Magonjwa ya ngono yatokeayo mara kwa
mara Tanzania
•
•
•
•
•
•
•
Kisonono
Kaswende
Kandidiasis
Malengelenge ya sehemu za siri
Trikomoniasis
Pangusa
Viotea
Kaswende ya kuzaliwa: (uvimbe wa ini
na bandama)
Genital Warts
Genital Warts
Uhusiano kati ya magonjwa ya ngono na
virusi vya ukimwi
• Uambukizi ni sawa
• Uwepo wa magonjwa ya ngono
unaongeza uwezekano wa maambukizi ya
virusi vya ukimwi kwa asilimia 40
Dalili za magonjwa ya ngono kwa wanawake
• Kutoa maji maji ukeni yasiyo ya kawaida na
yenye harufu
• Maumivu wakati wa kujamiiana
• Maumivu au mfukuto wakati wa kukojoa
• Hali ya kujisikia kwenda haja ndogo mara kwa
mara
• Maumivu makali kutokana na vidonda ndani na
nje ya sehemu za siri
• Matatizo wakati wa hedhi
Dalili kwa wanaume
•
•
•
•
•
•
•
•
Maumivu wakati wa kukojoa
Kutoa usaha/damu katika njia a siri
Vidonda katika sehemu za siri
Kuwashwa sehemu za siri
Kuvimba kwa matezi
Malengelenge katika sehemu za siri
Kuvimba uume
Kuvimba makende
Madhara yatokanayo na magonjwa ya
ngono
•
•
•
•
•
•
•
Ugumba/utasa
Kuvurugikiwa kwa akili
Upofu wa watoto wachanga
Kutunga mimba nje ya mji wa mimba
Kuziba mkojo kwa wanaume
Kuharibika mimba
Kuzaa mtoto mfu
Matibabu ya magonjwa ya ngono
• Mueleze kijana kuwa magonjwa ya ngono
yanatibika na mpatie rufaa ya kuja kituoni
kwa matibabu
• Mfuatilie kuhakikisha amepata matibabu
na amepona sawasawa
Matumizi sahihi ya kondom
• Use a new condom for each acts of sexual
intercourse
• Do not use teeth, fingernails or sharp
• Put condom on erect penis
• Hold tip of condom and unroll it on the erect
penis
• Withdraw from partner after ejaculation when
penis is still erect
• Use only water based lubricants
AHSANTE
Virusi vya ukimwi na ukimwi
Nini maana ya virusi vya ukimwi na ukimwi
Virusi vya UKIMWI ni vijidudu vidogo
sana visivyoweza kuonekana kwa macho,
ambavyo vina shambuliwa na kudhoofisha
kinga mwilini. Virusi vya UKIMWI vinaishi
ktika damu na maji maji mengine ya
mwilini ya mtu aliyeambukizwa. Virusi
hivyo vinaweza kuambukiza mtu mwingine
kwa kupitia maji maji ya mwilini hasa
damu, manii na maji maji ya ukeni.
UKIMWI ni hatua ya mwisho ya
maambukizi yatokanayo na virusi vya
UKIMWI.
Ufahamu juu ya VVU na Ukimwi
• Asilimia 98.4 ya wanawake na asilimia 98.9 ya
wanaume wote Tanzania wenye umri wa miaka
15-49 walishawahi kusikia kuhusu Virusi vya
Ukimwi.
• Kwa upande wa vijijini asilimia 97.9 ya
wanawake na asilimia 99.6 ya wanawake
wanaoishi mijini wenye umri huo walishawahi
kusikia kuhusu Virusi vya Ukimwi
• Kwa wanaume wanaoishi vijijini ni asilimia 98.7
ikilinganishwa na asilimia 99.6 kwa wanaume
wanaoishi mijini
Hali ya Maambukizi ya VVU/Ukimwi
kitaifa
• Asilimia 5.7 ya wanawake na
wanaume wa Tanzania bara
wameambukizwa virusi vya ukimwi.
Wanawake ni asilimia 6.6 na
wanaume ni asilimia 4.6
• Maambukizi ya VVU mijini ni asilimia
8.7 ukilinganisha na asilimia 4.7 kwa
upande wa vijijini
Hali ya Maambukizi Kimkoa
• Kwa Tanzania Bara mikoa yenye
maambukizi ya asilimia 5 au zaidi ni Iringa,
Dar es Salaam, Mbeya, Shinyanga, Tabora,
Ruvuma, Mara, Pwani na Mwanza
• Mikoa yenye maambukizi kidogo zaidi ni
Kigoma, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
• Kwa Zanzibar kiwango cha maambukizi ni
cha chini kuliko vyote
Hali ya Maambukizi ya VVU/Ukimwi:
Kitaifa...
• Asilimia 10.6 ya wanawake wanaoishi
mijini wameambukizwa VVU ukilinganisha
na asilimia 5.3 ya wanawake wanaoishi
vijijini ambao wameambukizwa VVU
• Asilimia 6.4 ya wanaume wanaoishi mijini
wameambikizwa VVU ukilinganisha na
asilimia 4 ya wanaume wanaoshi vijijini
ambao wameambukizwa VVU
Njia kuu za maambukizo ni:
 Kujamiiana na mtu aliyeambukizwa bila kinga
 Mama kumuambukiza mtoto wake akiwa
tumboni au wakati wa kuzaa
 Kuwekewa damu ambayo haikupimwa
 Kuchangia vitu vyenye ncha kali vilivyotumiwa
na mgonjwa mwenye virusi
 Maji maji mengine ya mwilini zaidi ya damu
yana uwezekano wa kuambukiza.
Hatua tofauti za maambukizo ya virusi
vya UKIMWI
Hatua ya 1:
• Maambukizi ya awali (becoming HIV
antibody infected). Watu wengi
wanaopata maambukizi ya virusi vya
UKIMWI, hawajitambui kwamba
wameambukizwa, ila kwa wengine
wanaoanza kuugua mara tu
wanapoambukizwa. Hii inaitwa
subconversion illness.
• Ugonjwa huu unaweza kuchukua wiki
chache na mara nyingi unakuja na mafua
yenye homa, udhaifu wa mwili, uvimbe wa
tezi maumivu kooni, ukurutu au maumivu
ya viungo. Magonjwa hayo
yanaambatana na uenezaji wa virusi
katika sehemu tofauti za mwilini na hasa
katika mfumo wa lymphoid.
Hatua 2:
• Haina dalili (clinicaly asymtomatic stage)
Hatua hii inaweza kuchukua wastani wa
miaka 10 na mtu anakuwa hana dalili za
ugonjwa wowote isipokuwa uvimbe wa
tezi.
• Katika hatua za awali za maambukizo ya
virusi vya UKIMWI, wagonjwa wengi
wanakuwa hawana dalili zozote ingawa
kuna mapambano makali ya kinga.
Wagonjwa wa aina hii wanaweza
kuambukiza virusi vya UKIMWI kwa
wengine.
Hatua 3:
• Dalili za maambukizo ya virusi vya
UKIMWI (symptomatic HIV). Muda
unavyozidi kupita ndivyo mfumo wa kinga
unavyopoteza mapambano na virusi vya
UKIMWI kwa hiyo dalili zinajitokeza. Dalili
za maambukizo ya virusi vya UKIMWI
zinasababishwa na maambukizi tegemezi.
• Matatizo yanayojitokeza ni homa,
maambukizo ya njia ya hewa, kikohozi,
kifua kikuu, kaposisi sarcoma, upungufu
wa uzito, magojwa ya ngozi, maambukizo
ya virusi, utando wa mdomoni, maumivu
na lymphadenopathy.
Hatua 4: UKIMWI
• UKIMWI unathibitishwa kama mtu
mwenye virusi vya UKIMWI amepata dalili
moja au zaidi za magonjwa tegemezi au
sarakani.
Njia salama za kujamiiana ili kuzuwia
magonjwa ya kuambukiza na mimba
zisizotarajiwa.
• Njia salama ni njia yeyote ile ambayo
inazuia au kupunguza uambukizo wa
maradhi ya ngono na UKIMWI pamoja na
mimba zisizotarajiwa. Njia hizi ni zile
zinazoweza kutumiwa bila kupunguza
hisia zako.
Njia isiyo na madhara
• Vile vitendo ambavyo hakuna kujamiiana
kimwili, kama vile kukumbatiana, kupeana
mikono na yeyote.
Njia iliyo na madhara madogo
Kutumia kondom.
• Iliyo na madhara ya wastani.
Ni vile vitendo vya kuhatarisha kwa kiasi
fulani kama vile kutia kidole ukeni au
sehemu ya haja kubwa.
Iliyo na madhara makubwa
• Njia ambazo zinahatarisha sana kwa
sababu zinakuletea kukutana na majimaji
ya mwili ambayo yana virusi kamavile
kujamiiana bila kutumia kondom au
kunyonya uume usiovaliwa kondom
Jinsi ya kumhudumia mgonjwa
mwenye Ukimwi nyumbani:
• Anahitaji ushauri nasaha
• Chakula bora na cha kutosha
• Anahitaji kujizuia na magonjwa mengine
k.m. malaria
• Matibabu ya magonjwa nyemelezi kama
kifua kikuu
• Dawa za kurefusha maisha
• Upendo toka kwa wanakaya na jamii
• Ashirikishwe katika shughuli mbalimbali za
kijamii kutegemea hali yake
Jinsi ya kuzuia maambukizo:
• Kuacha kabisa kujamiiana
• Kubakia na mpenzi mmoja nyote mkiwa
waaminifu na hauna maambukizi
• Kujadiliana juu ya mambo ya ngono
• Kutumia kondom kwa usahihi
• Kutochangia vitu vyenye ncha kali
• Kutumia vifaa safi
 Kutambua magonjwa ya zinaa mapema
AHSANTE
MILA NA DESTURI ZINAZOATHIRI AFYA
YA UZAZI KWA VIJANA
MILA NA DESTURI ZINAZOATHIRI AFYA
YA UZAZI KWA VIJANA
• Mara nyingi vijana wanakuwa wahanga wa
tabia, mila na desturi mbali mbali zenye
athari katika afya ya uzazi kama ukeketaji
wa wasichana wanawake, kudhalilishwa
kingono, kulazimishwa kuolewa au kuoa
mapema na utumiaji wa madawa ya
kulevya.
• Tabia, mila na desturi hizi, huchangiwa
kwa kiasi kikubwa na utamaduni wa eneo
husika, mambo ya kiuchumi, na kijamii na
mazingira yanayomzunguka kijana.
Kazi ya kikundi
Elezea mila na desturi zinazoathiri afya ya
kijana
Baadhi ya vitendo vyenye madhara ni
•
•
•
•
•
Ndoa za kupangwa au kulazimishwa
Ukahaba
Ukeketaji
Madawa ya kulevya
Unyanyasaji wa kijinsia
Madhara ya vitendo hivi kwa afya ya
uzazi ya kijana
Ndoa zilizopangwa au za kulazimisha
 Mimba katika umri mdogo na madhara
yake
 Kuathirika ki-saikologia
 Mahusiano mabaya ndani ya ndoa
 Kuvunjika kwa ndoa au kuachana na
kurudiana mara kwa mara.
 Vijana kutofikia malengo yao kimaisha
Mambo ya kuzingatia kuzuia/kuepuka
ndoa katika umri mdogo:
• Vijana wapewe habari sahihi kuhusu
madhara ya ndoa katika umri mdogo
madhara ya ndoa katika umri mdogo.
• Vijana washauriwe kujihusisha na shughuli
mbalimbali, michezo au masomo.
• Kuhamasisha jamii kutoa haki sawa za
afya ya uzazi kwa vijana wa kike na
kiume.
Ukahaba katika umri mdogo
• Ni mahusiano ya kimapenzi
yanayohusisha kutoa penzi kwa minajiri ya
kupata pesa au zawadi.
• Biashara ya ukahaba wakati mwingine
hufanywa na watu wazima ambao
huwatumia vjana kama vitega uchumi.
Madhara ya ukahaba
• Kuambukizwa magonjwa ya ngono na
UKIMWI
• Mimba zisizotarajiwa
• Unyanyasaji wa kijinsia kama kupigwa,
kutolipwa fedha kwa kazi alizofanya n.k.
• Kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya
kulevya
• Wizi na ujambazi
Mambo yanayosababisha biashara ya
ukahaba katika umri mdogo
•
•
•
•
•
Umasikni
Msukumo wa makundi rika
Mila na desturi
Ukosefu wa kazi
Kutojali/kutowajibika katika masuala ya
familia/binafsi
• Ugonvi katika familia
Njia za kuzuia ukahaba katika umri
mdogo
• Vijana wapatiwe elimu kuhusu stadi za
maisha ili kukabiliana na msukumo wa
makundi rika.
• Vijana wajihusishe na shughuli za
uzalishaji mali.
• Kurekebisha mila na desturi
zinazochangia vijana kujiingiza katika
ukahaba.
• Vijana wasaidiwe/wapewe nafasi ya
kujielimisha zaidi ili waweze
kujijengea mazingira mazuri katika
maisha ya baadaye.
Ukeketaji wa wanawake
• Ni ukataji wa baadhi ya viungo vya nje vya
uzazi vya mwanamke. Kitendo hiki
hufanywa kwa ajili ya kutimiza matakwa ya
mila na desturi za jamii husika.
Sababu za kukeketa wasichana
•
•
•
•
•
Kulinda viungo vya uzazi vya mwanamke
Kuzuia msichana asiwe Malaya
Kuingia rasmi katika rika lingine
Kutambulika katika jamii husika
Kukubalika katika ndoa
Madhara ya ukeketaji
•
•
•
•
•
Maumivu makali wakati wa kukeketa
Kutokwa na damu nyingi
Matatizo wakati wa kujifungua
Maambukizo kama vile ya UKIMWI
Maumivu wakati wa kujamiiana
• Kukosa hamu wakati wa kujamiiana
• Kuharibika kwa viungo vya uzazi vya nje
vya mwanamke
• Hofu, uchungu na wasiwas – hasa
kumbukumbu ya kukeketwa inapomjia
msichana
• Kutojiamini
Njia za kuzuia ukeketaji
• Sheria na sera za kutokomeza ukeketaji.
• Ushirikishwaji wa jamii katika kupiga vita
suala zima la ukeketaji wa wasichana.
• Ushirikishwaji wa viongozi wa kijamii,
kisiasa na kiserikali katika kusaidia
kutokomezaji ukeketaji.
• Kusaidia familia na jamii katika
kurekebisha mila potofu zinazohusu
ukeketaji.
• Kuelimisha na kuwawezesha wanawake
kiuchumi ili waweze kushiriki kikamilifu
katika kutokomeza ukeketaji.
• Kuwahudumia ipasavyo wasichana na
wanawake waliopata madhara ya
yatokanayo na ukeketaji.
• Elimu kwa umma kuhusu madhara ya
ukeketaji kwa wasichana.
Jinsi ya kumtambua mtu aliyekeketwa
• Wengi wao wanapata matatizo ya kutembea na
kukaa wakati wanapotoka kufanyiwa ukeketaji.
• Maumivu makali
• Kutoka damu nyingi sehemu za ukeni.
• Viungo vya uzazi vinabadilishwa na kuwa tofauti
na vya wasichana/wanawake wasio keketwa.
• Kutokuwa na hamu ya kujamiiana.
• Hofu, woga, kusononeka.
• Msongo wa mawazo baada ya kukeketwa (Post
Circumscision Stress).
Madawa ya Kulevya
Sababu za vijana kutumia madawa ya kulevya
• Kutaka kujaribu (curiosity)
• Msukumo wa makundi rika
• Kukosa kazi
• Mahusiano mabaya katika familia
• Kuondoa maumivu
• Kukosa malezi kutoka kwa wazazi
• Kukosa elimu ya kutosha kuhusu madhara ya
madawa ya kulevya
• Matangazo ya biashara yanayoelezea uzuri wa
pombe, sigara
Aina ya madawa ya kulevya na
yanavyotumiwa
•
•
•
•
•
Pombe – Kunywa
Sigara, Tumbuku – kuvuta
Bangi – kuvuta
Heroin - kunusa, kujichoma kwa sindano
Cocaine – kunusa, kubwia, kujichoma na
sindano
•
•
•
•
•
Opium - kunusa
Mandrax – kunywa
Phenobarbitone – kunywa
Petroli – kunusa
Mirungi – Kutafuna
AHSANTE
MTANDAO NA RUFAA
Nini maana ya mtandao
• Mtandao ni kufanya kazi kwa kushirikiana
na watu au vikundi au taasisi nyingine.
Mtandao ni muhimu kwa vile sio rahisi kwa
mtu au kikundi au taasisi kutoa huduma
jumuishi za afya ya uzazi kwa kijana.
Faida za mtandao:
• Hutoa fursa kwa ajili ya mahitaji ambayo
hayajatatuliwa au kushughulikiwa na pia hutoa
nafasi kwa rasilimali kutumika ipasavyo katika
jamii.
• Pia mtandao huimarisha mikutano ya
kubadilishana habari, jinsi ya kuwasiliana na
kupata habari mpya kuhusu afya ya ujinsia na
uzazi kwa vijana. Huendeleza mikakati
iliyofanikiwa ya kutoa huduma ya afya kwa
vijana.
Baadhi ya wadau katika mtandao wa
huduma za afya ya uzazi kwa vijana ni:
• Taasisi za umma
• Mashirika ya hiari yasiyo ya kiserikali
yanayoshughulika na vijana
• Huduma za misaada za kijamii
• Asasi za kidini na mashirika au vyama vya
vijana katika jamii/kijiji.
Rufaa:
Rufaa ni kitendo cha Mwelimishaji rika
kumuelekeza mwanarika kwenye sehemu
nyingine kupata huduma ambazo
mwelimisha rika hatoi. Waelimishaji rika
wanaweza kupata wanarika wenye
matatizo ya kiafya ambayo hawawezi
kuyamudu na hivyo yatahitaji rufaa
kwenda ngazi nyingine.
Baadhi ya matatizo au masuala ambayo
yanaweza kuhitaji rufaa ni pamoja na:
• Tiba ya magonjwa ya ngono ikiwa ni
pamoja na ushauri, ushauri wa hiari na
upimaji wa hiari wa VVU
• kupata njia za uzazi wa mpango
• ushauri na msaada kuhusu matumizi na
ulevi wa dawa
• ushauri na huduma kuhusu kubakwa na
kutoa mimba
• tiba na msaada kuhusu UKIMWI.
Kupanga namna ya kutoa rufaa:
• Zungumza na mwanarika ili ubaini tatizo
au mahitaji yake
• Mwelimishe kuhusu umuhimu wa kumpa
rufaa
• Mpe habari kuhusu sehemu anayoweza
kupata huduma inayohitajika
• Mwandikie maelezo mafupi kuhusu
sababu za rufaa
• Fuatilia ili ujue kama amefanikiwa kupata
huduma
• Tunza kumbukumbu kwa usahihi.
AHSANTE
Kuandaa somo
Mambo ya kuzingatia wakati wa kuandaa
somo
•
•
•
•
•
•
•
•
Madhumuni ya somo
Walengwa
Mada
Malengo
Maudhui
Njia za ufundishaji (njia shirikishi)
Vitendea kazi
Mbinu za tathmini
Kanuni za utoaji elimu
Somo Linatakiwa liwe na:
 linalohusiana na mahitaji ya kiafya na
linalovutia usikivu
 lililo rahisi kueleweka
 linalotoa ujumbe
 lisilo badilika badilika
Hatua za kufuata kabla/wakati wa
utoaji elimu
Kujenga uhusiano
• Wasalimie wanarika katika lugha
inayokubalika
• Jitambulishe jina lako na wale
unaofuatana nao na mada
utakayowasilisha
• Waombe wanarika nao wajitambulishe
(kama inawezekana)
• Waulize wanarika kama wamekaa vizuri
• Tambulisha somo na malengo yake
Kujenga uhusiano
…
• Waulize wanarika wanaelewa nini kuhusu
mada iliyotajwa
• Washukuru wanarika kwa majibu yao
mazuri kuhusu mada ya somo
litakalotolewa
• Ongoza na hamasisha majadiliano ili yawe
yanahusiana na mada inayojadiliwa
washawishi wanarika kujibu maswali
kutoka kwa wenzao
• Endesha somo ukiwatazama wanarika
• Tumia stadi za mawasiliano kwa maneno
na ishara katika kuendesha mazungunzo
Kutathmini somo
• Waulize wanarika kueleza mambo
waliyojifunza katika mada
• Chagua mambo muhimu na omba
wanarika wakueleze
• Waambie wanarika watoe maoni
yao kuhusu mambo waliojifunza
Kutathmini somo
• Waulize wanarika ni mambo
gani wanakusudia kufanya
baada ya somo hilo
• Muda wote wa mazungumzo
sikiliza matamshi ya wanarika
ili uweze kuchambua kiwango
chao cha uelewa
Kufunga somo
• Toa muhtasari wa mambo muhimu ya
mada iliyotolewa
• Waarifu wanarika kuhusu mipango ya
baadaye
Kufunga somo…
• Washukuru wanarika kwa
ushiriki/maudhurio yao mazuri na
waruhusu kutawanyika
• Tayarisha ripoti ya mafunzo ikijumuisha
mambo yote muhimu, terehe, mahali,
sababu, idadi ya washiriki, mazungumzo
yaliyozingatiwa na mipango ya baadaye
AHSANTE
Stadi za maisha kwa vijana
Nini maana ya Stadi
• Stadi za maisha ni mbinu
maalumu, ambazo hutumiwa ili
kumwepusha mtu kukabiliana
na matatizo yatokanayo na
mazingira magumu katika
maisha ya kila siku.
Kazi kwa kila mshiriki
Taja stadi moja ya maisha
unayoikumbuka/fahamu katika
kadi
1.Stadi za kujitambua,
Humfanya kijana ajielewe kuwa yeye ni
nani, ana thamani gani katika jamii,na
anawajibika vipi katika kulinda afya
yake, na
ile ya jamii nzima.
2. Stadi za mahusiano
Humpa kijana mbinu za kuwa na mahusiano
salama baina yake na jamii inayomzunguka
mfano ndugu, wanarika wenzie, watu wa
jinsi tofauti na hata viongozi wake/wazazi
wake.
3. Stadi za mawasiliano
Humpa kijana uwezo wa kuwasiliana
ipasavyo, akitumia maneno na ishara sahihi,
katika nyakati muafaka. Pia humwezesha kuwa
mthubutu, mkweli na mwenye uwezo wa
kuwasiliana bila kuvuruga mahusiano na wengine,
hata kama hakubaliani nao. Uwezo wa
kuwasiliana kuhusu matatizo aliyonayo
humwezesha kijana kupunguza matatizo zaidi.
4. Stadi za kutatua matatizo
Humwezesha kijana kujua mbinu sahihi za
kutatua matatizo aliyonayo kwa kutumia T 3,
yaani Tatizo, Tatuzi na Tokeo. Kijana
hupima kila njia anayofikiria kuwa itamsaidia
kutatua tatizo lake kwa kuzingatia matokeo
ya njia hiyo.
5. Stadi za kufanya maamuzi sahihi
Humpa kijana hatua za kufanyia maamuzi,
pia humwonyesha vituo vya kufanyia
maamuzi. Uwezo wa kujiepusha na tabia
hatarishi zinazopelekea maambukizi ya VVU
na UKIMWI hutegemea sana uwezo wa
kijana katika kufanya maamuzi.
6. Stadi za kuhimili mihemko
Humpa kijana uwezo wa kuikabili na
kuihimili mihemko itokanayo na hisia
zilizomo mwilini mwake, au zile ambazo
angeshawishiwa na wenzake.
7. Stadi za kuhimili msongo
Humpa uwezo kijana kukabili msongo wa
mawazo, matatizo na kumwepusha na
maamuzi kama ya kunywa sumu, kukimbilia
mitaani ama kujiingiza kwenye matumizi ya
madawa ya kulevya.
8. Stadi za uyakinifu
Humwondoa kijana katika fikra mgando,
zimfanyazo kung’ang’ania mazoea na hata
mila na desturi zenye madhara kiafya.
Uyakinifu humpa kijana uwezo wa kuwa na
mwamko katika suala zima la ujinsia na
jinsia, pamoja na kuondoa hofu, ukanaji na
unyenyepa katika VVU na UKIMWI. Hii ni mbinu
muafaka katika kubadilisha mtazamo wa kijana.
9. Stadi za Ubunifu
Humjengea kijana uwezo wa kutumia akili
yake vizuri, pamoja na kuongeza uwezo
wake wa kufikiri haraka. Hii inamtayarisha
kijana hasa katika mazingira ya hatari
ambayo hutokea ghafla, katika upenyo
mwembamba.
10. Stadi za Ushirikeli
Humpa kijana mbinu za kuyatazama
matatizo ya watu wengine kwa macho
yao, ama kujiweka katika nafasi za watu
wengine, matokeo yake akawa na
mtazamo wa kuheshimu mawazo ya
watu wengine, kukubali kutokubaliana na
bila kuzua ugomvi na wengine.
KUMUDU SHUGHULI ZA UELIMISHAJI
RIKA
KUMUDU SHUGHULI ZA UELIMISHAJI
RIKA
• Mipango madhubuti, utekelezaji, ufuatiliaji
na tathmini ya shughuli itawezekana iwapo
tu kuna takwimu sahihi na za kutosha. Ili
kuweza kutoa huduma bora za afya ya
uzazi kwa vijana, mwelimishaji rika
atatakiwa kukusanya, kuchambua kutuma
na kutumia takwimu na taarifa mbalimbali.
Pia anapaswa kutoa mrejesho kwa wadau
mbalimbali wa afya ya uzazi kwa vijana.
Kupanga
• Ni njia ya kuandaa shughuli ili zifikie lengo
lililokusudiwa.
Sababu ya kupanga
• Inasaidia kutambua mahitaji na kuamua
shughuli gani zifanyike. Hivyo unapopanga
lazima uhusishe mambo yafuatayo:
Walengwa ni nani, lini utaanza shughuli
hizo, nyenzo au msaada unaohitajika, nani
atakuwa msimamizi.
Kutengeneza Andalio la Utekelezaji
• Unaanza kuchora andalio lako la
utekelezaji kwa kila siku, kila wiki au kila
robo mwaka, kati ya mwaka au mwaka.
Andalio hilo lazima lionyeshe kitendo
chenyewe, pahali, nyenzo zitazohitajika na
tarehe ya utekelezaji.
Ukusanyaji wa Taarifa za Afya ya Uzazi
kwa Vijana
Unasaidia:
• Kuongeza ufanisi wa kupanga, kuandaa,
kutekeleza na kufatilia.
• Kutoa muongozo wa kutathmini matokeo.
• Kuonyesha mapungufu katika shughuli.
• Nyenzo za usaidizi za baadae na kutafuta
mahitaji ya vifaa na zana nyinginezo kama vile
kondom.
• Kutafuta makundi mbali mbali yanayohitaji
huduma kama vile wasichana, wavulana, vijana
walio kwenye mazingira hatarishi.
Hatua za ukusanyaji wa taarifa:
• Utambuzi wa shughuli zinazohitaji kutekelezwa
• Kutengeneza nyenzo na vitendea kazi vya
kukusanyia taarifa
• Kujaza na kuzihifadhi taarifa
• Kupeleka nakala kwa wahusika
• Kuweka kumbukumbu
• Kutumia takwimu na taarifa kwenye kupanga
shughuli na kufikia maamuzi
Majumlisho ya Taarifa:
• Majumulisho ya taarifa ya kila mwezi
yanaweza kupatikana kwenye kitabu cha
kumbukumbu ambacho muelimishaji rika
anakijaza kila mwaka.
Uwekaji wa kumbukumbu
Kusanya na tunza takwimu na kumbukumbu
kulingana na makundi. Makundi hayo
yanaweza kuwa ni:
• Idadi ya wanarika uliowahudumia
• Eneo analotoka mwanarika
• Umri
• Jinsia
• Aina ya huduma ulizotoa
• Rufaa
Hitimisho
• Sambamba na takwimu, pia andaa
maelezo kuhusu mambo mengine kama
vile maoni ya wanarika kuhusu huduma
unazotoa, matatizo uliyokutana nayo na
mafanikio uliyopata. Kumbuka kutoa
mrejesho kwa wadau wote ikiwemo jamii
unamofanyia kazi.
Na
SHUGHULI
MUDA
KIASHIRIA
MAHITAJI
AHSANTE