wanawake na watoto

Download Report

Transcript wanawake na watoto

Imeandaliwa na
Fatuma Semgaya
Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu.
 Tanzania
ni miongoni mwanchi za Afrika
ambazo zimeridhia mikataba ya kimataifa
mbalimbali ambazo zinawalinda wanawake
kwa namna moja au nyingine.
 Ipo
mikataba ya kimataifa na ya kibara
tofauti tofauti inayo ainisha Haki za
wanawake
 Kwa leo tunaangalia mazingira ya haki za
Wanawake Tanzania,kuna sheria ambazo
zinazowalinda wanawake Tanzania na




Katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Ibara ya
12(usawa wa binadamu), Ibara ya 13 (Usawa mbele ya
sheria - ubaguzi)
Sheria ya ndoa, sura ya 29. Kifungu 66 (kinakataza
kumchapa viboko mwenzi katika ndoa. Hivyo endapo
mtu atamchapa mkewe ama mumewe ni kosa kisheria)
Sheria ya Kuzuia Maambukizi ya Ukimwi(kulinda
maambukizi ya kusudi, usiri wa taarifa)
Sheria ya kuzuia Usafirishaji wa Watu ya mwaka 2008
 Sheria
ya makosa ya jinai sura ya 16
mabadiliko ya 1998 (k.130 ubakaji, k.135
shambulio la aibu, k.138 A-D unyanyasaji wa
aina zote,k157 kufanyamapenzi kinyume cha
maumbile, k.169A ukeketaji ). Pia kinaainisha
aina nyingine za makosa kama Kupigana,
kuumizana, k.89A kutoa vitisho, K.240 -243
mashambulio
Vitendo vya ukatili wa Kijinsia kama ambavyo
vilivyoainishwa kwenye Tamko la Umoja wa Mataifa
la Uondoshaji wa Ukatili Dhidi ya Wanawake la
mwaka 2005 ( the United Nations Declaration on the
Elimination of Violence against Women (UNFPA, 2005)],
limetafsiri Ukatili kumaanisha:
“Kitendo chochote cha ukatili kuhusu jinsia,
ambacho kinaweza kusababisha madhara/maumivu
ama mateso ya kimwili au kisaikolojia kwa
mwanamke, ikiwa ni pamoja na vitendo vya kutishia,
kulazimisha, kunyima uhuru, bila kujali vimefanywa
kisiri ama kwenye kadamnasi.”
Ukatili wa kutumia nguvu
(kumpiga makofi, mateke,
na kumchapa)
- Ukatili wa kisaikolojia
(kusema mambo yanayo
Kufanya kujisikia mdogo,kuku
nyanyasa, kukusimanga ) kulazimisha na
kushinikiza kufanya naye mapenzi/tendo la
ndoa

Ukatili wa kiuchumi (kukunyima mahitaji muhimu
na fedha za kujikimu, kukuzuia kufanyakazi)
Kukuweka chini yake (kukuweka mbali na ndugu
au marafiki, kuchunguza mwenendo wako,
kusimamia na kuzuia upatikanaji wako wa taarifa
au msaada)
 Ukatili unaotokana na mila na desturi :Ukeketaji Kitendo cha kukata kidogo au kuondoa kabisa
sehemu ya uzazi ya mwanamke au msichana kwa
sababu zozote zile.

 Ndoa
za utotoni - ndoa inayofungwa ambayo
mmoja wa wanandoa hajafikisha umri wa utu
uzima, unaosababisha ashindwe kufanya
maamuzi mwenyewe, juu ya afya yake ya uzazi,
mwenzi wake, kumkosa kusoma, kipato.
Hii ni moja ya sababu zinazosababisha ukatili
kwa wanawake na pia ni ukatili.
 Utakasaji na kurithi wajane
 Mauaji ya vikongwe
 Usafirishaji wa watu – (wanawake na watoto)
 Baada
ya kuangalia sheria na mikataba ambayo
inalinda haki za Wanawake Tanzania na
mazingira yanayopelekea ukiukwaji wa Haki za
Wanawake, mchakato wa Katiba ni nafasi
muhimu ya kutoa mapendekezo ya kufanya
mabadiliko katika Katiba mpya.
 Katiba ya sasa haijaelezea haki za Wanawake
kwa upana wake kwahiyo tumeainisha
mapendekezo yanayohusu haki za wanawake
kwenye Katiba mpya.
 Katiba
ya nchi lazima iainishe kwa ufasaha
misingi yote ya Haki za Binadamu yaani
(Kisiasa, kiraia, kiuchumi, na kijamii na
kimaendeleo kuweka ulinzi madhubuti wa haki
hizo.
 Katiba
iainishe na kutoa ulinzi wa haki za
makundi hususani haki za wanawake na watoto



Ionyeshe kuwa Mahakama zote zinaweza kusikiliza
Mashauri ya uvunjwaji wa Haki za Binadamu.
Katiba iainishe kutokuwepo na muuingiliano wa
mihimili ya dola yaani Mahakama, Serikali na Bunge.
Katiba iainishe kuwa mapato yatokanayo na Rasilimali
za taifa yawanufaishe wananchi hasa maeneo
yanayopatikana rasilimali hizo

Katiba ianinishe kuwa watu wote wana haki ya
kupata huduma bora za :
Afya
Maji Safi na Salama
Elimu
Makazi Bora .

Kuwaka na utengwaji wa bajeti endelevu kwenye
sekta za huduma mbalimbali za kijamii jamii.

Mwanamke kuthaminiwa na kupewa ulinzi wa utu
na ubinadamu wake.
 Kuwalinda
wanawake dhidi ya manyanyaso
yote yakiwemo ya Kijinsia na kutoa adhabu
kwa watendaji wa vitendo hivyo.
 Kuondoa
aina zote za Ubaguzi na
unyanyasaji wa Kijinsia hasa kwa walemavu,
wanawake na watoto
 Kutungwa
kwa sheria zinazomlinda mtu
dhidi ya kuteswa, kuadhibiwa kinyama au
kupewa adhabu zinazomtweza ama
kumdhalilisha.

Kuwe na uwiano sawa wa Kijinsia asilimia 50/50 katika ngazi zote za
maamuzi kama vile:
- Bunge
- Mahakama
- Nafasi mbalimbali za uteuzi kama Makatibu wakuu,
- mawaziri,
- manaibu waziri, mabalozi n.k.
- Madiwani Serikali za vijiji, miji na mitaa

Kuwepo na jitihada chanya za kurekebisha mfumo ili kuwa na usawa
katika ngazi zote za maamuzi.

Serikali kutunga Sheria itakayo hakikisha kuwa wanawake wanashiriki
bila ya Ubaguzi katika chaguzi zote.




Katiba kuainisha kuwa kila mtu ana haki ya
kujiunga na chama chochote cha siasa
anachopenda.
Katiba kuainisha kuwa viongozi kutojilimbikizia
mali wakati wa uongozi wao.
Kuwepo na ukomo wa wabunge.
Mawaziri wachaguliwe kulingana na taaluma zao
na vilevile wasichaguliwe kutokana na wabunge.

Mwanamke kulindwa dhidi ya mila na desturi
kandamizi na kuwepo kwa sheria za kumpa
ulinzi mwanamke dhidi ya mila hizo.
 Kuondoa
na kubadilisha sheria zote za
kibaguzi na kandamizi dhidi ya mwanamke
zilizopo sasa mfano sheria ya mirathi, ndoa,
sheria ya Uraia.
 Kuweka
ulinzi wa haki za Wazee dhidi ya
Ubaguzi, mali na kunyanga’nywa

Kutoa haki na kuhakikisha mwanamke anakuwa
na haki ya kupata na kumiliki Rasilimali kama :
 Ardhi/Urithi
 Madini
 Mazao aliyolima mwenyewe.
 Pato lake
Katiba kutambua haki za wajane katika :
- Kurithi mali
- Kulea watoto wake.
-Kuishi kwenye nyumba ya
familia.
-Haki ya kuolewa tena.

 Wanawake
wapewe fursa na usawa katika
ajira, na kuwa na uwiano wa ujira anaolipwa
kati ya wanawake na wanaume.
 Haki
ya ulinzi kwa wanawake na kuwawekea
mazingira mazuri kutokana na mahitaji yao.
 Maliasili
zote za nchi ziwe chini ya mamlaka
ya wananchi ili Kuwepo na kuhifandhi na
ulinzi kwa kutoweka wawekezaji
wanyonyaji.
 Katiba
iainishe kwa kuweka wazi mbele ya
wananchi mikataba yote inayohusiana na
uvunaji na matumizi ya Rasilimali za taifa .
 Wananchi
washirikishwe katika uwekezaji
na umiliki wa ardhi ya umma na mamlaka
yasiwe mikononi mwa rais tu.
 Kuwepo
kwa Mahakama ya kifamilia ili
iweze kutatua matatizo ya kifamilia kwa
haraka na wakati.
 Katiba
kuainisha haki ya watu kuwa na
Uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zao.
 Haki
ya kupata taarifa kwa wakati kuhusu
matukio mbalimbali muhimu kwa maisha na
shughuli za umma pamoja na mikataba yote
iliyoingia baina ya serikali na wawekezaji.

Katiba iainishe jukumu la serikali kutoa taarifa kwa
wananchi.

Katiba iainishe kuwa watu wanastahili kuwa na Uhuru
wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini.


Haki ya wanawake kushiriki katika shughuli za umma
na kuweka jukumu kwa vyombo husika kuhakikisha
ushiriki huo.
Kutoa jukumu kwa serikali kutekeleza mikataba ya
kimataifa ya haki za Binadamu na haki za wanawake
pindi inaporidhiwa na utekelezaji wa majukumu yake
kama yalivyoainishwa kwenye mikataba hiyo.
 Kwa
kuhitimisha, tumeangalia sheria
zinazolinda wanawake,na
zinazowakandamiza wanawake ni jukumu
letu sasa kutumia fursa tuliyonayo
kupendekeza haki muhimu kuingia
katika katiba mpya kwa kuangalia haki za
msingi ambazo haziko kwenye katiba
mpya.