TANDAN FARMS LIMITED by Nicholas Kampa Final

Download Report

Transcript TANDAN FARMS LIMITED by Nicholas Kampa Final

 Kampuni
ya Tandan Farms Ltd imeanzishwa
mwaka 2008, iko Kisemvule – Vikindu, Wilaya
ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani ni km 25 kutoka
mjini Dar es Salaam barabara ya Kilwa.
 Tanzania
hali halisi ya ufugaji ni wa asili, na
wafugaji hawajawezeshwa kufahamu sera na sheria
zinazoongoza ufugaji.Hali ya biashara kwa sasa ni
holela haizingatii viwango vinavyokubalika. Tandan
Farms tunafuga kisasa na tunatoa mbegu bora ya
nguruwe aina ya DUROC na WHITE LARGE. Duroc ni
mbegu nzuri ya nguruwe wa nyama – inanenepa
nyama haina mafuta mpaka 150kgs na white large
inazaa watoto mpaka 18 na ni kubwa.
Mambo ya kuzingatia kabla ya kufuga;
•Maji
•Mbegu bora
•Chakula bora
•Banda bora na safi (70cm width x 100 x 80
length, mlango 25cm x 40cm length)
•Bio Security / Usafi wa mazingira


Dar es Salaam pameongezeka ulaji wa nyama ya
nguruwe yani Demand ya nyama ni kubwa mno kwa ulaji
wa kawaida kufuatana na ubora wa nyama kwa Grade.
Dar es Salaam inatumia tani 8 hadi 10 za nguruwe kila
siku. Kuna machinjio ya kienyeji zaidi ya 22. Machinjio
ya Tandan ni ya kipekee Dar es salaam inayotumia
Technolojia na ubora wa kisasa. Yenyewe yako takribani
3km kutoka shambani tunapofungia na yana uwezo wa
kuchinja nguruwe 50 mpaka 100 kwa siku na pia
tunasindika nyama ya nguruwe. Tunatengeneza bidhaa
nyingi kwa mfano sausage, bacon, ham, salami na
kadhalika. Vilevile tuna mikato tofauti ya nyama na
smoked meat.
 Upatikanaji
wa mifugo kwa kiasi kikubwa
sasa hivi ni mkoa wa Shinyanga, kuhama
wanaongoza, Singida, Morogoro na Iringa.
 Arusha, Moshi, Kagera soko la nyama ni
kubwa bado hawatoshelezi.
 Uwezeshaji wa ubia kibiashara unatokana na
Kampuni yetu ya Tandan Farms tunawauzia
mbegu bora na tunawapa chakula bora kama
tunavyofanya sisi. Soko lao ni sisi wenyewe
watuuzie tusindike nyama zenye ubora.
 Kama
biashara nyingine kuna ushindani wa
kibiashara hasa kwa Kampuni kutoka Kenya
Farmers Choice hii Kampuni ina mtaji wa
kutosha. Sisi mtaji hatuna.
 Bei ya chakula inapanda sana kila wakati
(Mfumko wa bei) ni hatari
 Kupata mkopo kutoka TIB imekuwa ngumu
sana hata siwezi kuelezea ni mambo ya aibu
ya nchi yetu. Hatuna mtaji wakufanyia kazi
(Working Capital)
 Tumetuma
maombi yetu TIB Bank
watuwezeshe mtaji wakufanyia kazi (Working
capital) ili tuweze kununua vifungashio
(packaging) vya kisasa na mashine za utupu
(vacuum) ili tupambane na mauzo.
Tunaogopa kujitangaza maana mahitaji
(orders) ni nyingi sana na vitendea kazi
hatuna vilevile tunaomba Serikali kuondoa au
kupunguza kodi kwenye vifaa na mashine za
kuchinja na kukata nyama.
 Iwe
namba moja Afrika Mashariki kuzalisha mbegu
bora ya Nguruwe
 Iwe namba moja kusambaza nyama bora na salama
Afrika Mashariki.

 Kuhamasisha
ufugaji wa kibiashara na wa
kisasa.
 Kuomba ofisi ya Rais – kuna watu (vigogo)
wamemilikishwa Ardhi ya kufuga lakini
hawafugi kabisa hata ndege pori havumi
miaka mingi. Wapewe wafugaji ili tupate
nyama nyingi.
 Ukosefu wa mfumo na miundombinu wa
uhifadhi wa bidhaa za nyama.
 Pawe ni miundombinu ya soko kwa mfano
mizani kwenye minada ya mifugo.

ASANTENI