TAMEPA by Joachim Mmassy Final Agreed

Download Report

Transcript TAMEPA by Joachim Mmassy Final Agreed

LENGO KUU
• 1. Kuwaleta wadau pamoja wa tasnia
kuwezesha kubadilishana
mawazo,uzoefu,na maarifa na
kuainisha kwa pamoja mahitaji
muhimu na changamoto zinazokabili
uzalishaji wa mifugo bora
kibiashara,biashara ya nyama na
bidhaa zake, usindikaji na masoko.
LENGO KUU
• 2.Kuanzisha vyombo/vyama vya
wadau vitakavyowaleta pamoja
wazalishaji,wafanyabiashara na
wasindikaji ili kukidhi matakwa ya
Sheria ya Nyama namba 10 ya 2006
kwa lengo la kusukuma kwa kasi
zaidi maendeleo ya sekta ya nyama
nchini.
HALI HALISI YA USINDIKAJI
• Hali halisi si ya kuridhisha sana kwani
usindikaji unafanyika katika kiwango cha chini
(small scale production) na baadhi yao
wamejikita zaidi katika biashara ya chuni bila
kuongeza thamani.
• Pamoja na changamoto zilizopo tunapongeza
kampuni chache zinazojitahidi kusindika .
Kuna kampuni 4 zinazochinja na kusindika
kuku,2 nguruwe na 6 ngombe.
CHANGAMOTO ZILIZOPO
i.
Upatikanaji wa mifugo bora kipindi chote cha
mwaka inayokidhi mahitaji ya soko.
ii. Gharama kubwa za vifaa na mashine za
machinjio na usindikaji bado vinatozwa kodi ya
ongezeko la thamani & import duty.
iii. Urasimu / mtizamo hasi wa taasisi za fedha kwa
wadau wa sekta katika kupata mitaji ya
uwekezaji.
iv. Gharama kubwa za vifungashio kutokana na
kodi ya VAT.
CHANGAMOTO ZILIZOPO
v.Idadi isiyotosheleza ya wataalam wa fani ya
nyama (meat technologists) nchini ubora
hafifu wa vifaa vinavyopatikana kwa ajili ya
usindikaji.
vi.Udhaifu wa serikali kuthibiti magonjwa ya
mlipuko mara kwa mara mfano FMD n.k
vii.Kutokuwepo kiwanda kikubwa cha kitaifa cha
mfano nchini kama illivyo KMC -Kenya na
BMC – Botswana
CHANGAMOTO ZILIZOPO
xix. Kudorora /kubinafsisha ranchi za taifa
ambazo zilikuwa kitovu cha kuzalisha mifugo
bora kwa ajili ya nyama.
X. Kupungua kwa nyanda za malisho kutokana
na ongezeko la idadi ya watu ,makazi na
shughuli za kilimo cha mazao.
Xi. Elimu duni kwa wafugaji Traditional vs
commercial livestock production.
CHANGAMOTO ZILIZOPO
Xii.Kudumaa kwa chama kutokana na
wanachama kushindwa kutegemeza
chama kwa michango hivyo kuwa
vigumu kuitisha mikutano kwa mujibu
wa katiba.
Xiii.Kukosekana mfumo mzuri wa kuratibu
ili kutambua nani anazalisha nini kwa
kiasi gani na mahitaji halisi ya soko.
JUHUDI ZILIZOFANYIKA
• Pamoja na changamoto zilizopo uongozi
wa chama kushirikiana na Bodi ya
Nyama Tanzania uliainisha aina ya
mashine,vifaa na mahitaji mengine
yanayohitajika kwenye usindikaji nyama
na kuwasilisha serikalini kwa ombi la
kuondolewa kodi ikiwa ni utekelezaji wa
azimio la mkutano wa baraza la mwaka
la Tano.
KUBORESHA TASNIA
• Uboreshaji wa tasnia ya nyama ni
jukumu mtambuka ambalo linahitaji
nguvu ya pamoja kati ya wadau ,serikali
,vyombo mahususi vilivyoanzishwa
kisheria kama Bodi ya nyama Baraza la
mwaka na wadau wote kupanga,
,,kusimamia na kuratibu maendeleo ya
tasnia katika mfumo endelevu kwa
maslahi ya wadau na Taifa kwa ujumla
MWISHO
• Kwa kuwa bodi ya nyama imepewa
jukumu la kulea ,kushauri na kuratibu
shughuli za vyama vya wadau wa tasnia
naomba ikiwezekana ishirikiane na chama
kuandaa mkutano utakaowezesha
wasindikaji kupitia hali halisi ya chama
kubaini mapungufu na kuweka mikakati
mipya ya kuendeleza chama .
ASANTENI KUNISILKILIZA
MENDALIWA NA
JOACHIM MMASSY
KATIBU WA TAMEPA
APRIL 2015
• MKUTANO WA SITA BARAZA LA MWAKA LA
WADAU WA TASNIA YA NYAMA
ULIOFANYIKA MOROGORO GLONENCY 88
•
TAREHE 15- 16 201