mada kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na

Download Report

Transcript mada kuhusu utatuzi wa migogoro ya ardhi baina ya wafugaji na

MADA KUHUSU MAENDELEO YA
UFUGAJI NCHINI NA CHAMA CHA
WAFUGAJI
TANZANIA(CCWT)BAGAMOYO,
PWANI
MKUTANO WA SITA WA BARAZA LA MWAKA WA WADAU WA
TASNIA YA NYAMA
TAREHE 15 HADI 16 2015,
MOROGORO,
UTANGULIZI
• CCWT kilianzishwa tarehe 16 Oktoba 2013 ili:
• Kuwaunganisha wafugaji wote Tanzania na
wadau wengine wa maendeleo
• Kulinda, kusimamia na kutetea haki za
wafugaji na mifugo yao.
• Kuzalisha mifugo bora na mazao yake ili kuwa
na soko bora na endelevu
• Kuhamasisha wafugaji wa Tanzania kufuga
kitaalamu na kibiashara kuzingatia uwezo wa
upatikanaji wa malisho, maji na vyakula vya
UTANGULIZI
• Kushirikiana na wadau wengine kuweka
mfumo wa soko la mifugo unaoeleweka ndani
na nje ya nchi, ikibidi kuendesha machinjio na
viwanda vya usindikaji
• Kujenga mahusiano mazuri na watumiaji
wengine wa ardhi na kuzingatia utunzaji wa
mazingira
HALI HALISI YA UFUGAJI NCHINI
i. Kukosa thamani kwa mfugaji wa Tanzania;
ii. Uadui kati ya serikali na wafugaji kwa
mtazamo wa wafugaji nchini;
iii. Manyanyaso ya wafugaji kutoka kwa
wataalamu wa mifugo; na
iv. Mfumo wa elimu juu uendelezaji wa ufugaji
wa asili haupo na kama upo haujawafikia
wafugaji wa asili.
MAENDELEO YA CCWT
i. CCWT kimeweza kuwa sauti ya wafugaji
Tanzania;
ii. Kuwatembelea wafugaji nchi nzima na
kukitangaza chama;
iii. Kuzuia operation mbalimbali zilizo kandamizi
dhidi ya wafugaji.
iv. Kufanikisha na kurejesha Imani ya wafugaji
kwa serikali
INAENDELEA
• Kuratibu zoezi la kuwatambua wafugaji kwa
ajili ya maeneo yao;
• Kuendesha sensa ya kaya za wafugaji na
mifugo yao kwa kushirikiana na Serikali na
asasi za kiraia;
• Kupunguza manyanyaso kwa wafugaji kutoka
kwa Mamlaka za Hifadhi za wanyama pori
MAFANIKIO YA CCWT KATIKA
KUENDELEZA UFUGAJI NA
KUONDAO MASKINI WA MFUGAJI
• CCWT imeweza kupata vitabu vya mipango ya
matumizi bora ardhi ikionesha maeneo 22 ya
malisho katika wilaya ya Bagamoyo ambayo ni
HA 53,106.9 sambamba na hotuba ya Waziri
• CCWT imefanikiwa kupitia maeneo kadhaa ya
malisho na kuona uwezekano wa kuhamasisha
wafugaji waweke miundo mbinu katika
maeneo hayo.
Upatikanaji wa Masoko bora ya mifugo
 CCWT wilaya ya Bagamoyo imeshafanya
mazungumzo na Bodi ya nyama na kuandaa ziara
ya kibiashara nchini Comoro;
 CCWT imeweza kuwaunganisha wafugaji na
kuwawezesha kupata leseni za biashara;
 Kufanikisha uanzishwaji wa vikundi na vyama vya
ushirika vya wafugaji; mfano Chama Cha ushirika
cha vijana kifugaji wa Kibarbaig na Chama Chama
cha Ushirika wa Ngo’mbe wa maziwa Bagamoyo;
 CCWT hivi karibuni imefanikisha zoezi la
kuwaunganisha wadau wa Bagamoyo na Bodi ya
Upatikanaji wa Mbegu bora za mifugo
• CCWT kwa kushirikiana Mh. Mbunge wa Jimbo
la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kimeweza
kupata Madume 10 bora ya mbegu
watakaogawanywa
katika
wilaya
ya
Bagamoyo.
• CCWT kupitia Afisa Mifugo wa Wilaya ya
Bagamoyo kimeweza kutoa elimu ya
uhimilishaji na unenepeshaji baadhi kwa
baadhi ya wafugaji
CHANGAMOTO ZINAZOMKABILI MFUGAJI
HAPA NCHINI
1. Kutotambuliwa na serikali
2. Wizara haijiamini kama inauwezo wa
kumlinda mfugaji wa asili
3. Mifugo ya asili nchini haijawekewa mpango
wa kufaidi rasilimali kama maji na mapitio ya
mifugo kulingana na watumiaji wengine wa
Rasilimali hizo.
4. Watu kuvamia maeneo ya malisho na Wizara
kukaa kimya kama vile haioni.
5. Kutokuwepo kwa teknolojia rafiki kwa
UTATUZI WA CHANGAMOTO
• Kuimarisha mahusiano vaina ya viongozi na
wafugaji
• Kuwa na vikao vya mara kwa mara baina ya
serikali na wafugaji katika maeneo husika
• Kushirikiana na sector binafsi na NGOs za
ndani na nje kusaidia wazara iweze kujiamini
katika kutoa huduma stahiki kwa wafugaji
• CCWT inaendelea na mchakato wa kujenga
mfumo wa kulinda maeneo ya malisho, njia ya
kufikia maji kushirikiana na wadau wa mifugo
UTATUZI WA CHANGAMOTO INAENDELEA
•
•
CCWT ipo kwenye mchakato wa kutoa elimu ya
Uraia ili wafugaji washiriki katika kura ya maoni
juu ya katiba pendekezwa na kushiriki katika
uchaguzi mkuu ujao wa oktoba ili wathaminiwe
CCWT ina mpango wa kuongea na wizara ili
maeneo ya malisho yapewe hati miliki kuepusha
uvamizi na kuwapa nguvu wafugaji kushitaki
MATARAJIO YA BAADAE YA CCWT
•
•
•
Kuhakikisha wafugaji Tanzania wanakuwa na
Benki yao.
Kuona kuwa wafugaji wanaishi kwa kwa
amani katika maeneo yao chini ya ulinzi wa
wizara na kufaidi rasilimali zilizopo.
Kuhakikisha kunakuwepo na teknolojia rafiki
kwa wafugaji na mifugo yao.
•
•
•
•
NINI KIFANYIKE KUBORESHA TASNIA YA
NYAMA?
Wafugaji wenyewe wahusishwe na mawazo
yao yazingatiwe katika kuboresha Tasnia ya
nyama.
Kuwepo na mikutano ya Mara kwa mara
Wataalamu wasisubiri taarifa ofisini
wazunguke nchi nzima kuwatembelea wadau
Wizara isaidie wadau kupatikana kwa fedha za
kuboresha Tasnia ya Nyama nchini
HITIMISHO
“UFUGAJI,MAISHA YETU, MAISHA YETU
UFUGAJI”
ASANTENI