UJASILIAMALI - Mwanza City Evangelism

Download Report

Transcript UJASILIAMALI - Mwanza City Evangelism



Mjasiliamali ni mtu anaekuwa na maono ya
biashara,anayegundua fursa,akakusanya
rasilimali na kuthubutu kuanzisha mradi kwa
imani kwamba atafanikiwa katika mradi huo
Ni mtu anaebadilisha mawazo kuwa bidhaa
au biashara



Kuongeza ajira
Kukuza uchumi wa nchi
Kuongezeka kwa mawazo mapya ya biashara










Anatafuta fursa
Mbunifu
Anayediriki kutenda
Anayejiamini
Anayetafuta habari
Anatimiza makubaliano katika kazi
Asiyeyumba
Anautashi wa ubora na ufanisi
Anayeweka malengo
Anayepanga na kusimamia



Hufanya vitu kabla ya kuambiwa au
kulazimishwa na matukio.
Hujitahidi kupanua biashara, bidhaa au
huduma katika maeneo mengine.
Huchukua fursa zisizo za kawaida kuanzisha
biashara mpya, kupata ufadhili, vifaa, ardhi,
mahali pa kazi au msaada.



Hukokotoa hatari kwa kujua na kutathmini
vitu mbadala.
Huchukua hatua za kupunguza hatari au
kudhibiti matokeo.
Hujiweka katika mazingira yanayohusu
changamoto au hatari za wastani.

Anaejitofautisha na wenzake kwa namna
tofauti tofauti kama rangi ya
bidhaa,muundo,namna ya kuuza,kifungahio
n.k



Hutafuta njia za kufanya mambo vizuri, kwa
haraka sana na kwa gharama nafuu.
Hufanya mambo ambayo yanafikia au kuzidi
viwango vya ubora.
Huweka au kutumia taratibu ili kuhakikisha
kuwa kazi inakamilika kwa wakati au kuwa
kazi inafikia viwango vya ubora
vilivyokubaliwa.




Hushikilia uamuzi wake wakati wa kukabiliana
na upinzani au kukosa mafanikio mapema.
Huonyesha kujiamini katika uwezo binafsi wa
kukamilisha kazi ngumu au kukabiliana na
changamoto.



Hujitolea binafsi au kutumia jitihada zisizo za
kawaida kukamilisha kazi.
Hushirikiana na wafanyakazi au kuwafuatilia
kuhimiza kazi ifanyike.
Hujitahidi kuwaridhisha wateja na kuwa na
uhusiano mzuri wa muda mrefu katika kipindi
kidogo tena.



Hutafuta mwenyewe taarifa kutoka kwa
wateja, wasambazaji au washindani.
Hufanya utafiti binafsi wa jinsi ya kutoa
bidhaa au huduma.
Hushauriana na wataalamu kuhusu ushauri
wa kibiashara au kitaalamu




Hupanga malengo na shabaha ambavyo vina
umuhimu na kuleta changamoto binafsi.
Hufafanua kwa uwazi malengo mahsusi ya
muda mrefu.
Huweka malengo ya muda mfupi
yanayopimika.



Hutumia mikakati ya makusudi ili kushawishi
wengine.
Huwatumia watu muhimu kama mawakala
kukamilisha malengo yake.
Hufanya kazi ya kuanzisha na kudumisha
mawasiliano ya kibiashara



Mara nying hufanya
vitu kwa ubunifu
Huajiri mtu na
kumpatia ujuzi ili
aweze kuihudumia
jamii vizuri
Anafanya shughuli
kwa taratibu ili
aweze kupata
matokeo
anayoyahitaji



Hufnya vitu kwa
kuiga
Huajiri mfanyakazi
ili biashara ifanye
vizuri na kupata
faida kubwa
Anafanya kazi kwa
haraka haraka na
wakati mwingine
hapati
anachokitarajia


Mjasiriamali
anaangalia
mafanikio kwa
atakachokiacha
Anajishindanisha
mwenyewe


Anaangalia
mafanikio kwa
maendeleo yake
mwenyewe au kwa
wafanyakazi wake
au kwa mbia
mwenzake
Anajitahidi sana
kuwashinda
washindani wake



Anamuona mteja
kama chanzo cha
kazi yake
Anachukua
maamuzi wakati
mwingine ni hatari
kwa kazi yake
Huweka mikakati ya
shughuli kuendelea
hata kama yeye
hatakuwepo



Anamuona mteja
kama chanzo cha
mauzo na mapato
Anaogopa sana
kuchukua maamuzi
ambayo yanaweza
kuhatarisha faida
yake
Yeye ndio
yeye,asipokuwepo
mambo yanakwama


Lengo ni
kubadilisha dunia
Panapokuwa na
ugumu hufuata njia
sahihi ya kutatua


Lengo ni kupata
faida
Mara nyingi
hutumia njia za
mkato katika
kutatua matatizo au
ugumu wa jambao
TAFADHALI ANGALIA MASWALI YAFUATAYO NA
KISHA UJIPIME MWENYEWE
KITU CHA MSINGI NI KUWA MUAMINIFU WAKATI
UNAJIPIMA
1.Ninafanya vitu mwenyewe. Hakuna
anayepaswa kuniambia nifanye jambo.
2.Kama mtu akiniwezesha kuanza,
ninaendelea vizuri.
3.Sitaraji jitihada zozote mwenyewe mpaka
nilazimike kufanya hivyo..

1.Ninapenda watu. Ninaweza kuelewana na
mtu yeyote.
2.Nina marafiki wengi - Simhitaji mwingine
zaidi.
3.Watu wengi wananiudhi.

1.Watu wengi hunifuatisha na huendelea kwa
mafanikio ninapoanzisha kitu.
2.Ninaweza kutoa maagizo kama mtu
ananifahamisha tunachopaswa kufanya.
3.Ninamwachia mwingine aendeleze kazi.
Kisha ninaendelea kama ninataka.

1.Ninapenda kusimamia mambo na
kuhakikisha yanakamilika.
2.Ninaweza kushika madaraka kama
nikilazimika, bali ningependelea mtu
mwingine ashike.
3.Kila wakati yupo mtu anayetaka kujionyesha
jinsi alivyo stadi wa vitu. Ninasema mwacheni
afanye hivyo.
1.Ninapenda kuwa na mpango kabla ya kuanza
jambo. Kwa kawaida mimi ndiye hupanga
mambo wakati kundi linataka kufanya kitu.
2.Ninafanya vizuri labda mambo yavurugike.
Kisha huacha.
3.Mambo yanapagwa vizuri kisha kitu
kinajitokeza na kusababisha matatizo mengi
mno. Kwa hiyo nayachukulia mambo kama
yanavyokuja.

1.Ninaweza kuendelea madhali ninapenda.
Sijali kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa
jambo ambalo ninalitaka.
2.Nitafanya kazi kwa bidii kwa muda, lakini
ninapotosheka, ninaacha.
3.Sioni kwamba kufanya kazi kwa bidii
kunawafikisha popote.
1.Ninaweza kuamua kitu kwa haraka nikipaswa
kufanya hivyo. Kwa kawaida huwa SAWA.
2.Ninaweza kama nina muda wa kutosha.
3.Nikilazimika kuamua jambo haraka, baadaye
ninafikiri ningeweza kuamua vinginevyo.
1. Wanaweza. Sizungumzi vitu nisivyokusudia.
2. Najaribu kuwa muwazi wakati wote. Lakini
wakati mwingine ninasema tu kilicho rahisi
zaidi.
3. Kwa nini ujisumbue kama mtu mwingine
haoni tofauti




Kama nikiamua kufanya jambo. Siruhusu kitu
chochote kinizuie.
Kwa kawaida ninakamilisha ninachokianza –
kama kinakwenda vizuri.
Kama hakiendi mara moja, ninaacha. Kwa
nini kusumbua akili yako?




Huwa siumwi!
Nina nguvu ya kutosha kwa mambo mengi
ninayotaka kufanya.
Huishiwa nguvu haraka kuliko rafiki zangu
walio wengi.


Kama majibu yako mengi yaliyokuwa ya 1
huenda una kitu kinachofaa katika kuendesha
biashara. Kama sio, unaelekea kuwa na
matatizo zaidi kuliko ambavyo unaweza
kuyashughulikia mwenyewe. Afadhali utafute
mwenza ambaye ni mzuri zaidi katika mambo
ambayo huyawezi. Kama majibu mengi
yalikuwa ya 3, hata mwenza mzuri hataweza
kukupatia msaada unaohitaji.

Nchini Tanzania,watu wengi wanaingia
kwenye shughuli za jiasiriamali na kuanzisha
biashara ndogo kwa sababu kuu tatu (3)




Kwanza,kukosa elimu ya kutosha ambayo ingesaidia
katika kupata ajira rasmi
Pili,Kukosa njia mbadala ya kupata kipato na hivyo
kupelekea ugumu wa maisha katika familia
Tatu,Kurithi kutoka kwa wazazi
Nne,Kutotaka kuajiriwa au kuwa chini ya mtu


Kiwango cha ujasiriamali nchini Tanzani bado
kipo chini ukilinganisha na nchi nyingi.Hii
inatokea wakati tuna rasilimali nyingi sana
ikiwemo bahari,maziwa,mbuga za
wanyama,ardhi nye rutuba,dhahabu,milima
n.k
Changamoto kubwa ipo kwetu na serikali
katika kubadilisha rasilimali hizi kwa ufanisi
na mafanikio ili ziwe bidhaa au huduma
zitakazopelekwa sokoni katika bei ya
ushindani





AHSANTENI SANA
THANK YOU
WABEJA SANA
WAKORA WAITU
MURAKOZE CHANE