Huduma ya mimba baada ya kuharibika

Download Report

Transcript Huduma ya mimba baada ya kuharibika

Huduma baada ya kujifungua
Taarifa anayotakiwa kupewa kijana
baada ya kujifungua:
• Kujadiliana kuhusu wasiwasi na matatizo
aliyonayo.
• Kufuatiliwa matatizo aliyokuwa nayo
wakati wa ujauzito kama kukataliwa na
aliyempa mimba, alikuwa haipendi/haitaki
mimba.
• Upungufu wa damu.
• Kuzungumzia uzazi wa mpango na
umuhimu wa kujikinga na magonjwa ya
ngono.
Taarifa ….
• Muda wa kupumzika na mazoezi.
• Lishe bora ili kurudisha afya yake na kwa
maziwa ya mtoto.
• Kuhudhuria kliniki ili kuangaliwa afya yake
na mtoto
• Usafi wa mama na mtoto
• Upendo kwa mtoto
• Umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya
mama
Ahsante kwa kunisikiliza
Huduma baada ya mimba
kuharibika
Maana ya kuharibika kwa mimba
• Ni kuharibika/kukatishwa kwa mimba
katika umri wa chini ya miezi 7 (wiki 28).
Mimba inaweza kutoka yenyewe au
kutolewa makusudi.
Aina za kuharibika kwa
mimba
1. Kutoka yenyewe
Ni mimba zinazoharibika na kutoka bila
kuchokonolewa/kuchokozwa. Hii huweza
kusababishwa na homa kama za malaria,
magonjwa ya ngono, matumizi ya madawa
makali au kupigwa.
Mimba iliyotolewa
•
Ni kutoka kwa mimba baada ya
kuchokonolewa/kuchokozwa kama kwa
kumeza madawa kwa makusudi hayo,
kuingiza vijiti au vyombo kwenye shingo
ya mji wa mimba. Pia mimba huweza
kutolewa kama kuna sababu na ushauri
wa daktari (inapotishia uhai)
Dalili za mimba inayotoka
•
•
•
•
•
•
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Mtoto kuacha kucheza
Mwili kuishiwa nguvu
Damu kutoka ukeni
Majimaji yenye harufu kutoka ukeni
Kichefu chefu na hata kutapika
Madhara ya kutoa mimba
•
•
•
•
Maambukizi
Kupoteza damu nyingi
Kuumizwa via vya uzazi
Kuathirika na sumu ya dawa zilizotumika
kutoa mimba
• Kuwa tasa/ugumba
• Kifo
Jinsi ya kuzuia utoaji mimba
• Kuacha ngono
• Kutumia kinga kwa usahihi kama njia za
uzazi wa mpango
• Kutumia njia ya uzazi wa mpango za
dharura
UMUHIMU WA HUDUMA KWA KIJANA
ALIYEHARIBU MIMBA (POST ABORTION
CARE)
• Huduma ni muhimu kwa kijana balehe ili
kuzuia madhara yatokanayo na kuharibu
mimba.
Taarifa anayotakiwa kupewa kijana
aliyeharibu mimba:
• Huduma hii inapatikana katika vituo
vya afya.
• Inatolewa na mtoa huduma mwenye
utaalamu huo
• Ni haki ya kijana
• Mimba nyingine inaweza kutunga siku
saba baada ya kuharibika
Taarifa anayotakiwa kupewa kijana
aliyeharibu mimba:
• Njia za uzazi wa mpango isipokuwa
kitanzi, zinaweza kutumiwa mara
baada ya mimba kuharibika.
• Epuka kufanya ngono hadi damu
baada ya kuharibika mimba
itakapokoma, kwa kufanya hivyo kuna
hatari ya kupata maambukizo.