Haki za vijana na afya ya uzazi Na: Dr. Z. Majapa

Download Report

Transcript Haki za vijana na afya ya uzazi Na: Dr. Z. Majapa

HAKI ZA VIJANA NA AFYA YA UZAZI
Na:
Dr. Z. Majapa
Nini maana ya ujana?
• Ni kipindi cha mpito toka utoto kuingia utu
uzima
• Kina ambatana na mabadiliko ya kimwili,
kiakili,na kimaendeleo
• Mabadiliko hayo huleta mabadiliko ya
kitabia
• Tabia zao zinahusiana na mahali
anapoishi, mila na desturi zilizopo, malezi
aliyopata wakati wa utoto wake.
Nini maana ya kijana
• Ni umri wa miaka 10 – 19 (WHO
wanagawa umri kama ifuatavyo)
• Miaka 10 – 19 = (adolescents) kijana
balehe
• Miaka 10 – 24 = (Young people)
• Miaka 15 – 24 = (youth)
Mgawanyo huu unatokana na hatua za
ukuaji, mahitaji na matatizo
yanavyojitokeza katika umri husika.
Afya ya ujinsia
• Ni hali ya mtu kuwa mzima ambapo
anaweza kufurahia maisha ya ujinsia bila
kuwa na wasi wasi wa kupata maumivu,
mimba au magonjwa yatokanayo na
ngono.
• Afya ya ujinsia ni kipengele katika afya ya
uzazi
Afya ya uzazi
• Ni hali ya kuwa salama kimwili,
kiakili,kiuchumi na kijamii na siyo tu hali ya
kutokuwa na ugonjwa au ulemavu katika
masuala yote yanayohusu mvumo mzima
wa uzazi na jinsi unavyofanya kazi.( ikiwa
ni pamoja na watu (mtu na mke) kuwa na
uwezo wa kuzaa na uhuru wa kuamua
kama wanataka kupata mtoto, lini, na
wototo hao wapishane muda gani.
Afya ya uzazi kwa vijana
• Hii ni hali ya kuwa salama kimwili, kiakili, na
kijamii na sio tu hali ya kutokuwa na ugonjwa
au ulemavu katika masuala yote yanayohusu
mfumo mzima wa uzazi na jinsi unavyo fanya
kazi katika umri wa ujana.
• Hii inajumuisha hali ya kijana kufurahia
maisha yake ya kuwa mwanamke au
mwanaume bila kunyanyaswa, kutopata
magonjwa yatokanayo na ngono na kupata
mimba au kusababisha mimba isizotarajiwa
Umuhimu wa kushughulikia haki ya jinsia na
uzazi kwa vijana
Kundi la vijana katika jamii ni kubwa:
• 65% ya wa Tanzania ni wa umri chini ya
miaka 25
• 31% vijana wa umri wa kati ya miaka 10 –
24
• 12% ya wanawake wanaopata watoto ni
kati ya miaka 15 – 19
• Wasichana wengi hujihusisha na
kujamiiana wakiwa na miaka 17 na
wavulana 18
Umuhimu …..
• Vijana wako katika hatari ya kuambukizwa
magonjwa y ngono ukiwamo ukimwi
• Hali ya uchumi inachangia vijana kujiingiza
katika masuala ya ngono mapema ikiwa
nipamoja na kuoa/kuolewa mapema
• Ni haki yao kupatiwa ushauri, habari na
huduma ya afya ikiwemo afya ya uzazi
Mwongozo wa sera ya afya ya uzazi na
mtoto Kitaifa
Maeneo yaliyopewa kipaumbele nchini
Tanzania:
• Uzazi wa mpango
• Uzazi salama
• Kuzuia na na kutibu magonjwa ya ngono
ikiwa ni pamoja na ukimwi
• Afya ya mtoto
• Afya ya jinsia na afya ya uzazi kwa vijana.
Vipengele vya huduma za afya ya uzazi kwa
vijana
• Uzazi wa mpango ikiwa ni pamoja na njia
za dharura
• Huduma baada ya kutoka kwa mimba
• Elimu ya ushauri kuhusuafya ya uzazi
kuzuia na kutoa huduma kwa maambukizi
ya magonjwa ya ngono ikiwa ni pamoja na
ukimwi
Haki za afya ya uzazi kwa vijana:
Nini maana ya haki?
• Ni kitu ambacho kila mtu kama binadamu
anastahili na anaweza kudai kisheria.
• Haki inaenda sambamba na suala zima la
uwajibikaji.
Kazi ya kikundi
NI ZIPI HAKI ZA AFYA YA UZAZI KWA
VIJANA?
Haki za afya ya uzazi kwa vijana
1. Haki ya kuwa na afya bora ya afya ya
uzazi
2. Haki ya kuwa huru kufanya maamuzi
kuhusu mahusiano ya kijinsia
3. Haki ya kupata elimu , habari kuhusu
afya ya ujinsia na uzazi
4. Haki ya kuwa huru kutokana na
unyanyasaji wa kijinsia
5. Haki ya mtu kuulinda mwili wake
6. Haki ya kupata huduma bora ya afya ya
uzazi inayokidhi mahitaji ya mtu binafsi na
ambazo anazoweza kumudu
Haki za afya ya uzazi kwa vijana…
7. Haki ya kulindwa kutokana na hatari zote
zinazotokana namagonjwa ya kujamiiana
ikiwa ni pamoja na ukimwi
8. Haki ya faragha na usiri wakati wa kupatiwa
huduma ya afya ya uzazi
9. Haki ya kudai haki, kuridhia na
kuheshimiana katika mahusiano ya
kimapenzi
Kazi ya kikundi - buzz
Ni vikwazo gani vinavyomfanya kijana
asitumie haki zake za afya ya uzazi?
Vikwazi vinavyoweza kuzuia kijana asitumie
haki zake za uzazi
• Mtazamo wa mtoa huduma huhusu afya ya
uzazi kwa vijana
• Imani za dini
• Mila na desturi
• Ukosefu wa miongozo kuhusu afya ya uzazi
kwa vijana
• Huduma zilizopo hazikidhi mahitaji ya afya ya
uzazi kwa vijana
• Sera na sheria zilizopo hazikidhi mahitaji ya
afya ya uzazi kwa vijana
Vikwazo …..
• Utoaji wa habari nchini na huduma za afya
ya uzazi kwa vijana, hauna msukumo
unaohitajika kutoka kwa baadhi ya
wanarika, familia jamii na watoa huduma
• Watoa huduma hawana uelewa na stadi
za kutosha kuhusu utoaji habari,elimu na
huduma za afya ya uzazi kwa vijana
• Vijana hawapewi nafasi ya kushiriki katika
huduma za afya ya uzazi kwa vijana
Viwango vya utoaji wa huduma za afya ya
uzazi Tanzania
Viwango vya huduma rafiki za afya ya uzazi
kwa vijana
1. Vijana wote kuweza kupata habari na
ushauri unaostahili kuhusu afya ya uzazi
kulingana na mahitaji, mazingira, upeo na
hali ya ukuaji
2. Vijana wote kuweza kupata huduma za afya
ya uzazi ikiwa ni pamoja na kinga,
uboreshaji, tiba na ukarabati ambazo ni
sahihi kulingana na mahitaji
3. Vijana wote kufahamishwa haki za afya ya
uzazi na haki hizo kulindwa na watoa
huduma na wanajamii
Viwango…
4. Watoa huduma katika vituo vyote wawe
na ufahamu, stadi na mtazamo chanja wa
utoaji huduma za afya ya uzazi; huduma
zitolewe kwa ufanisi na ziwe rafiki kwa
vijana
5.Sera na mifumo iwepokatika vituo ili
kusaidia utoaji wa huduma rafiki za afya
ya uzazi kwa vijana
Viwango …
6. Vituo vyote vya huduma kupangiliwa ili
kutoa huduma rafiki za afya ya uzazi
kulingana na matakwa ya vijana
7. Kuwepo kwa taratibu imara za jamii na
katika familia za kusaidia vijana kupata
huduma za afya ya uzazi
MABADILIKO KATIKA KIJANA BALEHE
Kazi ya makundi
Elezea mabadiliko ya kiakili katika makuaji
na maendeleo ya kijana katika umri
husika
Hatua za makuzi na mabadiliko katika
maendeleo kwa vijana
• Umri wa kati ya miaka (10-13)
• Umri wa Kati ya miaka (14-16)
• Kijana wa rika kubwa miaka (17-19)
Mabadiliko yanayotokea kwa wasichana
• Mwili kukua, kupanuka kwa nyonga, kukua
kwa kwa matiti
• Ngozi kuwa nyororo, chunusi usoni
• Kukua kwa via vya uzazi
• Kuvuja ungo
• Kuongezeka kwa hamu ya mahusiano ya
kijinsia
• Kupenda kuonekana nadhifu
Mabadiliko kwa wavulana
•
•
•
•
•
Kuongezeka urefu, uzito, kukua kwa misuli
Sauti kuwa nzito
Kuota chunusi usoni
Kuota nywele sehemu za siri
Kupata hamu ya kujamiiana
Mabadiliko ya kiakili katika umri tofauti kwa
wasichana na wavulana
Umri wa miaka 10 – 13
• Tabia ya kujaribu mambo
• Uwezo wa kuchanganua mambo
• Kupenda marafiki nje ya familia
• Kupenda uamua mambo mwenyewe
• Kupenda kusikiliza mawazo wa wanarika
Umri wa miaka 14 - 16
• Kupenda kuuliza dhamira za mitazamo na
sera mbali mbali
• Kukua kwa uwezo wa kufikiri matokeo ya
tabia hatarishi
• Kuongezeka zaidi kwa msukumo wa
makundi rika
• Kuongezeka kwa hamu ya kujamiiana na
kupenda marafiki wa jinsi tofauti
Umri wa kati ya miaka 17 - 19
• Kupevuka kwa via vya uzazi
• Kukua kwa uwezo wa kutatua matatizo
• Kukua kwa uwezo wa kujitambua
• Kupungua kwa msukumo wa makundi rika
• Kushirikiana na familia/ kutoa mawazo
yake
• Kutopenda kukaa katika magurupu
• Kukua kwa uwezo wa kushika majukumu
ya familia
• Anaelekea katika maisha ya kujitegemea
Via vya uzazi na kazi zake
Via vya uzazi na kazi zake
• Kwa wanaume:
Via vya uzazi vya mwanaume,
vimegawanyika katika makundi mawili, vya
nje na vya ndani.
Via vya uzazi vya nje vya mwanaume
• Uume:
Uume ni mrija wa kupitishia mkojo na
shahawa, hukakamaa wakati wa
kujamiiana ili kurahisisha wakati wa kuingia
ukeni.
• Mfuko kende:
Ni ngozi inayofunika kokwa. Kazi za mfuko
wa kende ni kulinda kende dhidi ya joto,
baridi au kuumizwa.
Via vya ndani vya mwanaume
• Mrija wa mkojo:
Ni mrefu, mwembamba unaopita ndani ya
uume.
• Tezi ya prosteti:
Ni tezi iliyo karibu na kibofu cha mkojo na
kifuko cha shahawa. Kazi zake, kuteneneza
majimaji ambayo huchanganyika na
shahawa.
• Vifuko vya shahawa:
Ni tezi mbili ndogo, zilizo karibu na tezi ya
prosteti.
Kazi zake ni kutoa shahawa
inayochanganyika na mbegu za kiume na
inavirutubisho.
• Mirija ya kusafirishia mbegu:
Ni vifereji viwili vinavyotoka kwenye kende
na kuunganika na mrija wa mkojo.
Kazi zake ni kupitisha mbegu za kiume toka
kwenye kende.
• Kokwa:
Ni tezi mbili zilizo kwenye mfuko wa kende.
Kazi zake ni kutengeneza na kuhifadhi mbegu za
kiume. Pia zinatengeneza vichocheo
vinavyosababisha uume kusimama.
• Epididimisi:
Ni kifereji kilicho jiviringaviringa na kipo juu ya
kokwa.
Kazi zake ni kuhifadhi mbegu za kiume
zilizokomaa na kuzipitisha kwenda kwenye mrija
wa kusafirishia mbegu.
Via vya uzazi vya mwanamke
Via vya nje.
• Mashavu ya ndani na nje
• Kisimi
Via vya ndani:
• Uke
• Shingo ya mji wa mimba
• Mji wa mimba
• Mirija ya kupitisha mayai
• Kokwa