UFUNDISHAJI WA FASIHI

Download Report

Transcript UFUNDISHAJI WA FASIHI

NINI FASIHI?
Ni sanaa inayotumia lugha ambayo inamzungumzia
binaadamu na mazingira yake.
 Unafikiri
kuna umuhimu gani kufundisha
fasihi mashuleni?
 Kuwawezesha
wanafunzi kufichua ukweli na
kupata maarifa yatokanayo na maisha ya
wengine.
 Kuamsha hamu na udadisi katika kuwaelewa
watu wengine na kujielewa wao wenyewe
pia.
 Kuendeleza na kudumisha utamaduni
 Kuwapa wanafunzi mbinu na mitindo mbali
mbali ya kujieleza
 Njia ya kujiburudisha
 Kujenga misimamo mipya katika maisha
 Unafikiri
mambo gani muhimu yanahitaji
kuchambuliwa katika usomeshaji wa fasihi?
 Maudhui
(lengo la msanii)
 Fani (muundo, mtindo, wahusika,
mandhari,lugha,…)
Mambo ya kuchambua katika riwaya na
tamthilia ni :
 kisa (jumla ya matendo yote)
 mtindo (jinsi ya masimulizi )
 wahusika (aina na huduma zao),
 mandhari (mazingira katika masimulizi),
 matumizi ya lugha,
 dhamira (kiini au chimbuko la kisa).
 Ufanisi
utatokana na matayarisho ya
mwalimu na vifaa alivyoviandaa
 Wanafunzi
zote.
lazima washirikishwe katika hatua
Hatua za ufundishaji
 Hatua
ya kwanza ni Kuchagua shairi
 Pili,Kujua madhumuni ya kusoma shairi hilo
(kutaja lengo)
 Tatu, Usikilizaji wa shairi (shairi lisomwe
mara mbili au tatu, lisomwe na mwanafunzi,
mwalimu au kinasa sauti.) Kabla ya
uchambuzi kuanza kuwe na mazungumzo ya
jumla yanayohusu maudhui ya shairi)
 Hatua
ya nne ni ya uchambuzi wa shairi
kutokana na madhumuni/malengo ya
ufundishaji yaliyotolewa. Uchambuzi wa
vipengele mbali mbali uendelee kwa njia ya
mjadala (Kuwe na vipengele mahsusi
vinavyochambulia kulingana na kiwango cha
wanafunzi)
 Hatua
ya tano na ya mwisho ni ya mazoezi
ambayo yataenda sambamba na madhumuni
ya somo. Mf wa mazoezi waandike insha juu
ya umuhimu wa... (ikiwa lengo ni kuelewa
dhamira), waigize sehemu ya ushairi (ikiwa
lengo ni kuelewa utamaduni, tabia, waandike
insha au ushairi kuhusu...(ikiwa lengo ni
kutunga au kueleza), Kueleza maudhui ya
shairi au ubeti fulani kwa lugha ya kawaida
(ikiwa lengo ni maudhui ya shairi).
 (namna
ya kutathmini itategemea na
malengo, ikiwa ni uchambuzi wa fani
unaweza kuwapa shairi jengine wachambue
lugha, fani, muundo, mtindo, nk)
UFUNDISHAJI WA HADITHI
1.
Hadithi zifundishwe kwa njia ya kutambwa
(masimulizi ndio msingi mkuu wa fasihi simulizi)
2.
Vifaa viwepo kama vinasa sauti au mwalimu
mwenyewe anaweza kuwa msimulizi hivyo huwa
ametumika kama ni kifaa cha kufundishia.
3.
Uchambuzi ufanywe kwa kuangalia uwasilishaji
wenyewe mfano wahusika, lugha, muundo, ujumbe
kila inapowezekana.
4.
Mazoezi yafanywe kwa kuzingatia malengo. Mf
kuwataka wanafunzi kukusanya na kutunga hadithi
mbali mbali na kuzisimulia, kuigiza hadithi
zilizosimuliwa, kuzibadili kuwa methali. (unaweza
kuwataka watunge hadithi inayoongozwa na
methali fulani-tathmini pia inategemea na lengo la
ufundishaji).
 Usimuliaji
(story telling)na maigizo ndio njia
zinazopendekezwa katika ufundishaji wa
fasihi simulizi.
 Hata hivyo, mwalimu anaweza kufundisha
tanzu nyengine za fasihi simulizi kama
methali, vitendawili, nyimbo, ngonjera, nk
kwa kufuata hatua zinazolingana na
ufundishaji wa tanzu nyengine, au katika hali
ambayo anahisi itawashirikisha wanafunzi na
kufikia lengo.
 Jambo muhimu la kuzingatia ni malengo,
uwasilishaji na namna ya kutathmini.
FISI AADHIBIWA
 Hapo zamani katika mbuga ya Rijeni wanyama
wadogo walikutana kwa siri kujadili uovu wa Fisi.
Walikutana kwa siri kwa sababu walijua wanyama
kama Simba, Chui na Fisi walikuwa na hamu kubwa ya
kuwashambulia na kuwala. Swala alikuwa kiongozi wa
mkutano na akawaambia wenzake, “Jamani, uonevu
umezidi. Juma lililopita watoto wawili wa Kongoni
waliliwa na Chui, tena Chui alisema hakushiba.
Alitaka sana amshike Kongoni amle, lakini Kongoni
aliwahi kukimbia. Juzi mwanangu Ameliwa na Fisi.
Nilimpiga teke jichoni lakini akataka kunitafuna,
nikakimbia, sasa tufanyeje?”

Basi wanyama walijadili kwa uchungu na kwa muda
mrefu. Wote walitaka sana Chui na Fisi wauawe
haraka. Tatizo lao kubwa lilikuwa jinsi ya kuwauwa.
Wengine walishauri waovu wale wategewe mitego ya
kamba baadaye wapofuliwe. Hata hivyo ilionekana ni
hatari bado. Hatimae sungura akatikisa masikio yake
na kusema, “Kuwauwa niachieni mimi. Nipeni siku
saba nitawaeleza na kuwaonesha nitakachofanya.”
Basi mkutano ukafungwa na kumkubalia Sungura
afanye kazi hiyo. Usiku ulipoingia Sungura alikoka
moto nje ya nyumba yake. Moto ulipokolea vizuri
akatia jiwe moja ndani ya ule moto. Jiwe hilo
lilikuwa na ukubwa wa mpira wa tenisi. Sungura
akaongeza kuni mekoni halafu akaenda kumtafuta Fisi
pangoni mwake.

Sungura alipofika mlangoni mwa pango akasema,
“hodi kwa mzee Fisi!” Fisi alifurahi moyoni, kwa
sababu alijua ile sauti ya Sungura na alijua kuwa
Sungura angeweza kuwa chakula chake. Fisi hakujibu
haraka. Kwa hiyo Sungura akasogea mlangoni na
kubisha tena hodi. Hapo ndipo Sungura alipojikuta
makuchani mwa Fisi! Sungura akaona kifo waziwazi
.Sungura akamwambia “rafiki yangu mzee Fisi vipi
leo? Nakuletea habari nzuri halafu unanikamata!”
Fisi akasema mimi nina njaa ya siku nne halafu
uniletee habari nzuri gani? “Wewe ni rafiki yangu”
Sungura akampoza , “hata kama utanila hutashiba.
Mimi nimekuja nikukaribishe kwangu. Huko nyama ni
tele.”

Fisi alifurahi na kucheka huku akimwachia
Sungura . “Haya ongoza njia. Tena uongeze
mwendo, sio ule mwendo wako wa sisimizi”.
Sungura na Fisi walifika kwa Sungura huku mate
yanamtoka Fisi mdomoni kwa hamu ya nyama.
Hapo Sungura akapanga vitimbi vyake akasema,
“mzee fisi nyama zipo nyingi lakini hizi ni nyama
za tambiko. Kwa desturi za kwetu mnofu wa
kwanza nitakulisha mimi mwenyewe, mradi ulale
chali na ufumbe macho”. Baada ya hapo nyama
nyengine utakula kwa mikono yako.” Kabla
Sungura hajamaliza Fisi alikwisha lala chali, na
kufungua mdomo na pia kufumba macho.

Sungura alicheka kimoyomoyo akatwaa kibanio,
akabana lile jiwe la moto na kulitumbukiza
mdomoni mwa Fisi. Kwa kuwa Fisi alikuwa
amejiandaa kumeza nyama , alilimeza jiwe
haraka sana. Looo! Fisi aliungua koo, kifua na
tumbo. Fisi alibiringika akilia sana na kujitupa
huku na huko hadi akakata roho.

(Kutoka, Kiswahili 2 - Kidato cha Pili, Taasisi ya
Elimu, Oxford University Press, Dar Es Salaam,
1996, uk 5-6.)