Hali ya mazingira kwa sasa duniani

Download Report

Transcript Hali ya mazingira kwa sasa duniani

Imeandaliwa na
Anna Masasi, LVEMP II
September 2014
1
Mawasilisho
1. Maana ya mazingira
2. Umuhimu wa mazingira katika maisha ya kila siku (Mazingira,
3.
4.
5.
6.
7.
8.
Maendeleo na Familia)
Hali ya mazingira ilivyo kwa sasa duniani
Hali ya mazingira ilivyo Tanzania
Shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira na athari
Juhudi za Serikali katika kupambana dhidi ya uharibifu wa
mazingira
Hali ya Mazingira ya bonde la Ziwa Victoria
Changamoto
2
Mazingira
Neno Mazingira lina maana pana sana;
linajumuisha hewa, ardhi na maji; uhai wa mimea na wanyama,
hali za kijamii na kiuchumi, miundombinu, joto, sauti, harufu
na mchanganyiko wa vyote hivi.
Umuhimu wa mazigira
 Mazingira yanaipatia nchi mahitaji yote ya msingi ya kijamii na
kiuchumi.
 Mazingira ndiyo makazi ya viumbe vyote – mimea na
wanyama ambao ndiyo urithi usiokuwa na mbadala.
 Mazingira ndio msingi katika kupunguza unyonge wa
umaskini.
 Mazingira ni chombo cha kuweka yale yasiyofaa.
3
Ndiyo maana wote tunawajibika kuyatunza.
Hali ya mazingira kwa sasa duniani - 1
Changamoto za mazingira duniani:
Mabadiliko ya tabianchi duniani
Ni mabadiliko ya hali ya hewa kama vile kubadilika kwa majira
kwa mfano mvua kutonyesha kwa wakati, ongezeko la joto,
mafuriko, ukame ongezeko la kina cha bahari, kupungua vya
vina mito na maziwa, nk
Kutoboka kwa utando wa ozone duniani
Gesi chafu za viwandani zinazotoboa utando wa ozone na
kusababisha mionzi ya jua ambayo si rafiki kwa afya ya
wanaadamu na husababisha magonjwa kama vile saratani ya
ngozi, ukuaji wa mimea, nk
4
Hali ya mazingira kwa sasa duniani - 2
Kuongezeka kwa joto duniani
Husabishwa na kukata miti hovyo, shughuli za viwanda
zinazozalisha ukaa kwa wingi. Ongezeko hili la joto
linachangia kuongezeka kwa magonjwa kama vile malaria,
kupote kwa baadhi ya viumbe, kubadilika kwa mfumo wa
ikolojia, kupungua kwa uzalishaji wa baadhi ya mazao k.m
mahindi, mpunga au kupotea kabisa kwa aina ya jamii za
mimea
5
HALI YA MAZINGIRA ILIVYO TANZANIA
Uchambuzi wa kitaifa umebainisha matatizo makubwa ya
Hali ya Mazingira ya Tanzania yanayohitaji kutafutiwa
ufumbuzi wa haraka, Matatizo hayo ni:1. Uharibifu wa Ardhi (land degradation);
2. Ukosefu wa maji safi na salama mijini na vijijini (lack of
3.
4.
5.
6.
accessible, good quality water for both urban and rural
inhabitants);
Uchafuzi wa Mazingira (Environmental pollution;
Kutoweka kwa mazalia ya wanyama pori na baianuai (loss of
wildlife habitats and biodiversity;)
Uharibifu wa mifumo ya majini (deterioration of aquatic
systems); na
Ukataji wa Misitu (Deforestation)
6
SHUGHULI ZINAZOCHANGIA
UHARIBIFU/UCHAFUZI WA MAZINGIRA
Uchafuzi/uharibifu wa mazingira kwa asilimia kubwa
huchangiwa na shughuli za binadamu za kila siku.
Shughuli nyingi zinakiuka taratibu na kanuni za
uhifadhi wa mazingira hivyo kusababisha uharibifu au
uchafuzi. Baadhi ya shughuli hizo ni kama;
 Shughuli za kilimo – kutozingatai kanuni bora
 Ufugaji – kutozingatia kanuni bora
 Shughuli za uvuvi
 Shughuli za kimaendeleo kama vile ujenzi, biashara n.k
 Uchimbaji na usafishaji madini,
 Viwanda, usafirishaji, mahoteli
7
Mambo yanayochangia
uharibifu/uchafuzi wa mzingira
 Umaskini – kutokuwa na njia mbadala wa kujipatia kipato
 Ongezeko la idadi ya watu mijini na vjijini pia – matumizi





makubwa ya rasilimali zilizopo (kugombania)
Jamii kutokuwa na elimu sahihi ya kuhifadhi mazingira na
matumizi bora ya rasilimali (shamba kubwa mavuno kidogo)
Kutoweka uoto – kupanua mashamba na makazi
Matumizi ya maeneo tekechu (sensitive areas) kama kilimo
kwenye miinuko, ardhi oevu, vyanzo vya maji n.k
Utupaji taka (taka maji na ngumu) ovyo
Usimamizi duni wa sheria na taratibu za kuhifadhi mazingira
8
Athari za uharibifu wa mazingira
Uharibifu huu unapunguza ubora wa mazingira kwa ujumla
 Kupungua kwa ubora na kina cha maji kwenye vyanzo
 kupungua kwa ubora wa hewa na udongo
 matumizi yasiyo endelevu ya maliasili
 mabadiliko ya hali ya hewa
Matatizo haya ya kimazingira yanaongezwa na kuongezeka
kwa idadi ya watu na hii inasababisha ushindani na
migongano katika matumizi ya rasilimali za pamoja
9
Kupungua kwa ubora wa maji
Ongezeko la Tope:
 Uharibifu wa ardhi ni kisababishi kikuu cha kujaa
tope kwenye vyanzo vya maji
 Kilimo kwenye miinuko, kingo za mito, misitu na
radhi oevu
 Ongezeko la idadi ya watu pamoja na umaskini
vinachangia kwenye shughuli za kilimo kisicho
endelevu
 Ufugaji mkubwa kuzidi uwezo wa maeneo
unachangia kuleta mmomonyoko wa udongo
 Mahitaji makubwa ya nishati ya miti inachangia
kuondoa uoto na hivyo kusababisha mmomonyoko
wa udongo.
10
Kupungua kwa ubora wa maji na udongo
 Maji taka ambayo hayakutibiwa kwa kiwango
kinachotakiwa toka viwandani na majumbani
 Maji machafu kutoka mijini
 Ukosefu wa vyoo kwenye makazi na maeneo ya
shughuli (kando kando ziwa na fukwe)
 Vichafuzi vinavyokuwepo katika tope, k.m. Mbolea
Uchafuzi huu unasababisha kuingia vijidudu vya
magonjwa kwa binadamu, upungufu wa hewa ya
oksijeni, madini tembo, kuongezeka mbolea (nitrogen
na phosphorus)
11
Matumizi yasiyo endelevu ya maliasili - 1
Uvuvi usioendelevu wa kutumia njia na nyenzo
zisizokubalika.
Kupungua kwa wingi na aina za samaki, kuharibika kwa
makazi ya viumbe
Uharibifu wa ardhi kwa kutokufuata kanuni bora za kilimo
na ufugaji
Ardhi kukosa rutuba na hivyo uzalishaji duni, maporomoko
na makorongo na kukosa ardhi nzuri ya kilimo na shughuli
nyingine
12
Matumizi yasiyo endelevu ya maliasili - 2
Uharibifu wa ardhi oevu
 Uharibifu wa makimbilio na mazalia ya samaki
 Kupoteza uwezo wake wa wa kuchuja uchafu kwenye
maji,
Ardhi oevu kando kando ya ziwa zimeharibiwa na kwa
kubadilishwa kuwa maeneo ya kilimo, kuchimba
udongo na mchanga na kutumika kama sehemu za
kutupa taka. Inakadiriwa asilimia 75 ya ardhi oevu ya
Ziwa Victoria imeharibiwa na karibu asilimia 13
zimeharibika kwa kiwango kikubwa.
13
Matumizi yasiyo endelevu ya maliasili - 3
Uharibifu wa Misitu:
 Hii inasababishwa na uvamizi kwa ajili ya kilimo,
kuongezeka mahitaji ya bidhaa za misitu kama vile
kuni, mkaa na magogo ya kujengea kutokana na
ongezeko la watu.
Kutoweka kwa uoto wa kudumu kumechangia
kuongeza kwa mmomonyoko wa udongo na kutokea
kwa makorongo makubwa.
14
ATHARI ZA UCHAFUZI WA MAZINGIRA
 Madhara Kiafya

magonjwa
mbalimbal;Kansa,maradhi,kuhara,ki
pindu pindu n.k
Mwendakulima
 Madhara kiuchumi


Matumizi yasiyo endelevu kwa rasilimali.
Uzalishaji duni
 Kiikolojia
 Kufa na kutoweka kwa viumbe
mbalimbali hasa wale
walegevu(flagile animals)
Mwime
Chapulwa
 Kijamii
 Migongano na kutoelewana kwa
makundi, jamii au watu mbalimbali
 Uhalibifu wa vyanzo vya maji na
mabadiliko ya tabia nchi.
15
NINI KIFANYIKE KUDHIBITI UCHAFUZI
Baadhi ya njia muhimu za kupunguza uchafuzi ni
pamoja na;
 Kutumia tekinolojia rafiki wa mazingira – vikapu,
mifuko ya karatasi n.k
 Upunguzaji wa uzalishaji taka
 Kutengeneza mbolea kwa taka zinazooza
 Uchambuaji wa taka toka chanzo
 Utupaji wa taka kulingana na matakwa ya utupaji taka
kimazingira (kutibu maji taka)
 Matumizi mengineyo (re-use) na urejereshaji
16
JITIHADA YA KUHIFADHI MAZINGIRA
 Kupata mbadala wa nishati na matumizi ya majiko
banifu, bio gas
 Ushirikishwaji wa jamii kikamilifu katika maoni na
hata maamuzi kwa shughuli zenye mwingiliano na
suala la mazingira.
 Elimu ya mazingira kwa makundi yote ya jamii ili kuwa
na mtazamo chanya katika suala la hifadhi na
usimamizi wa mazingira.
 Shughuli za kimaendeleo zifanyiwe tathmini ya athari
kwa mazingira
 Utashi wa kisiasa wahitajika katika kutoa maamuzi
yenye kujenda dhana nzima ya kuhifadhi mazingira
Kila mtu ashiriki kulinda mazingira
17
Juhudi za Serikali katika mapambano dhidi
ya uharibifu wa mazingira - 1
Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 1997. Madhumuni
ya Sera;
 Kuhakikisha udumishaji, usalama na matumizi sawa ya
rasilimali kwa mahitaji ya msingi ya sasa na ya vizazi
vijavyo bila kuharibu mazingira au kuhatarisha afya na
usalama.
 Kuzuia na kudhibiti uharibifu wa ardhi, maji, mimea na
hewa ambayo ndiyo husaidia mfumo wa uhai wetu.
 Kuhifadhi na kuendeleza urithi wetu na ule
unaotengenezwa na binadamu, ikiwa ni pamoja na
maisha ya viumbe wa aina mbalimbali na vya pekee
nchini Tanzania.
18
Juhudi za Serikali… - 2
Madhumuni ya Sera…
 Kurekebisha hali na uzalishaji wa maeneo yaliyoharibiwa
pamoja na makazi ya watu mijini na vijijini ili watanzania
wote waweze kuishi katika hali ya usalama, kiafya, kuzalisha
bidhaa pamoja na kuishi katika mazingira mazuri yenye
kuvutia.
 Kung’amua na kufahamu mahusiano muhimu kati ya
mazingira na maendeleo na kuhimiza ushirikiano wa mtu
binafsi na jamii katika kuhifadhi mazingira.
 Kuendeleza ushirikiano wa kimataifa kuhusu ajenda ya
mazingira na kupanua ushiriki na mchango wetu kwa pande
zote zinazohusika ikiwa zinahusu nchi jirani na mashirika na
mipango ya ulimwengu pamoja na utekelezaji wa mikataba.
19
Juhudi za Serikali…- 3
Sera ya Taifa ya mazingira ya 1997 ilisisitiza umuhimu wa
kutunga sheria za mazingira na sheria za Sekta nyingine
zinazohusiana na mazingira
Katika kuimarisha utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya
1997, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira imepitishwa na
Bunge (Sheria Na. 20 ya mwaka 2004) na ilianza kufanya kazi
tarehe 1 Julai 2005.
Kila mtu anayeishi Tanzania atakuwa na haki ya kuwa na
mazingira safi, salama na ya kiafya.
20
Sheria ya mazingira ya mwaka 2004
• Madhumunu ya sheria ni kuweka muundo wa
kisheria na kitaasisi katika usimamizi endelevu wa
mazingira;
• Kanuni kadhaa zimekwishaandaliwa na nyingine ziko
katika maandalizi
• Sheria hii inatambua kuwepo kwa sheria nyingine za
kisekta zinazohimiza hifadhi na Usimamizi wa
mazingira.
• Imetafsiriwa katika kiswahili
21
ZIWA VICTORIA
Umuhimu wa Ziwa Victoria
 Hifadhi ya baioanuai
 Ziwa na bonde lake linasaidia kutoa maji kwa matumizi
mbalimbali (Majumbani, Viwandani na Kilimo)
 Uvuvi wa samaki kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi
na kuuza nje ya nchi
 Usafiri na usafirishaji
 Utalii
 Chanzo cha umeme (Mfano Uganda)
22
Umuhimu wa Ziwa Victoria...
 Linawezesha maisha ya watu karibu milioni 3
wanaoishi katika bonde la ziwa Victoria
 Ajira kwa wakazi wa bonde
 Linapokea maji yaliyotumika viwandani na
majumbani na pia maji yenye mbolea na
udongo toka mashambani na maeneo ya
ufugaji.
23
Changamoto za Mazingira Ziwa V.
Ziko kwenye maeneo makuu 4, ndani ya ziwa, kando
kando ya ziwa, kwenye bonde na nje ya mipaka ya
bonde.
Changamoto hizi kwa pamoja zinasababisha uharibifu
wa mazingira ya ziwa, kupunguza uwezo wake wa
kujirudishia hali yake na kuchangia kwa matatizo
yanayojitokeza kuhusiana na matumizi ya rasilimali
24
Matatizo ndani ya ziwa
 Uvuvi usio endelevu
 Uchafuzi katika ziwa na visiwa kutokana na
 kumwagika kwa mafuta (meli n.k),
 taka ngumu
 uchafu wa maji ambayo hayakusafishwa kutoka
viwandani na majumbani.
Uchafuzi huu unapunguza aina na wingi wa samaki
lakini pia unaharibu maeneo muhimu ya mazalia ya
samaki
25
Matatizo kando kando ya ziwa
 Ni matokeo ya kubadilisha ardhi oevu zilizo kando ya
ziwa kwa ajili ya kuendeleza miji na kilimo.
 Ujenzi kando kando ya ziwa na kilimo bila kuchukua
tahadhari za muhimu za kuhifadhi mazingira
kunaongeza uingiaji wa taka maji na taka ngumu
ndani ya ziwa.
 Ubadilishaji wa ardhi oevu kwa makusudi tajwa hapo
juu husababisha kupotea kwa makazi ya viumbe vya
majini na kupunguza uwezo wa uchujaji na ulinzi wa
asili wa mazingira
26
Stresses on littoral zones
•Construction and farming in
shoreline
•Conversion of wetlands
•Poor solid wastes management
•Discharge of untreated effluent,
•Poor sanitation facilities
27
Matatizo katika Bonde
 kupungua kuingia kwa maji katika ziwa
 Matumizi makubwa ya maji ya ziwa
 kuingia kwa gugumaji
 kuongezeka uharibifu wa dakio la maji ikiwa ni pamoja na
mmomonyoko wa udongo na kupotea kwa uoto wa asili
 kuongezeka kwa uchafuzi wa maji kutoka viwandani, maeneo
ya mifugo, kilimo, machimbo ya madini na mitiririko ya maji
mijini.
Haya hubadilisha mfumo wa haidrolojia na ikolojia na
kusababisha kushamiri kwa algae ziwani, kuathiri uvuvi na
njia za vyombo vya majini hivyo kuchangia matatizo katika
matumizi ya rasilimali
28
29
30
Matatizo kutoka nje ya mipaka ya
bonde
 Kusafirishwa kwa mbolea na chemikali
nyingine kupitia upepo
 Mahitaji makubwa ya samaki aina ya Sangara
kwa ajili ya kuuza nje na
 mabadiliko ya tabia nchi
31
Mabadiliko ya tabianchi
 Mabadiliko ya tabianchi yanasababishwa na shughuli za
binadamu lakini pia shughuli za asili.
 Maeneo ambayo yameathirika sana na mabadiliko ya
tabianchi ni kama sekta za maji, afya, misitu na
ardhioevu, nishati, wanyamapori, utalii pamoja na
rasilimali za maji na ukanda wa pwani.
 Katika sekta ya maji nchini mabadiliko ya tabianchi
yamesababisha kupungua kwa mvua na hivyo kupungua
kwa ujazo wa maji katika mabwawa,mito na maziwa
kama ilivyo katika ziwa Victoria
32
Mabadiliko ya tabianchi
 Kuongezeka joto kunachangia kuyeyuka kwa theluji na
barafu kwenye mzingo wa dunia na milimani hivyo
kuchangia kuongezeka kwa maji baharini.
 Yanachangia pia kuongezeka kwa wadudu wageni na
wenye uwezo mkubwa wa kuhimili dawa kwa kiwango
kinachotumika sasa.
 Hali hii inasababisha magonjwa sugu, kuathiri kipato cha jamii
kutokana na magonjwa.
Hivyo, mabadiliko ya tabianchi ni janga la kidunia
linalohitaji juhudi za kidunia (Global problems require
global solutions)
33
Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya Ziwa
Victoria (LVEMP II)
Mradi wa pamoja unaotekelezwa na nchi 5 za
Jumuiya ya Africa ya Mashariki
Dira - ya Jumuiya ya Africa Mashariki
“kuwa na Ziwa lenye ikolojia imara inayokidhi
mahitaji ya jamii kwa chakula, kipato, maji safi,
ajira, mazingira bora yasiyo na magonjwa na
kuhifadhi viumbe hai”.
34
Lengo la Mradi
 Kuimarisha Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Maji
na Samaki
 Kupunguza uchafuzi Ziwani
 Kuinua Kipato cha Wananchi Wanaolizunguka
Ziwa
 Kupambana na changamoto mbalimbali zinazokabili
ziwa Victoria
35
Changamoto - 1
 Jamii kutokuwa tayari kuachana na matumizi
mabaya ya rasilimali kwa kuhofia kupungua
kipato
 Kukosekana kwa uwajibikaji miongoni mwa
viongozi na jamii husika
 Watu kutoona umuhimu wa kufahamu na kufuata
sheria
 Utashi wa kisiasa
 Ardhi iliyo mbali na vyanzo vya maji kutokuwa na
rutuba
36
Changamoto - 2
 Kukosekana kwa shughuli mbadala za kujipatia
kipato
 Ongezeko kubwa la idadi ya watu linalozidi
raslimali iliyopo
 Kukosa elimu ya mazingira
 Ongezeko la uhitaji mkubwa wa malighafi kwa
ajili ya viwanda vyenye masoko makubwa katika
nchi zilizoendelea
 Mabadiliko ya tabianchi
37
Namna ya kukabili changamoto 1
 Elimu endelevu ya utunzaji mazingira itiliwe
mkazo
 Kurutubisha ardhi iliyo mbali na vyanzo vya
maji ili iweze kufaa tena
 Kuwajengea wananchi uwezo wa kuibua na
kuanzisha njia mbadala za kuongeza kipato ili
kunusuru rasilimali zinazoelekea kuisha
 Kuhimiza uzazi wa mpango
38
Namna ya kukabili changamoto 2
 Kuwajengea uwezo wanajamii wa dhana na
mbinu za uwajibikaji wa kijamii
 Kuhimiza usimamizi endelevu wa rasilimali
miongoni mwa nchi zinazoendelea
 Kuchukuwa hatua mbali mbali za kukabiliana
na mabadiliko ya tabianchi kama vile kuhimiza
upandaji miti, kuwepo kwa mazao mbadala,
kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa
39
Utunzaji wa mazingira ni
jukumu letu wote, tuwe
sehemu ya suluhisho
Asanteni kunisikiliza
40