a : kodi ya mapato viwango

Download Report

Transcript a : kodi ya mapato viwango

NA: L. MTAFYA
SEPTEMBA,2014






MADA NDOGO
UTANGULIZI
KODI YA MAPATO
KODI YA MLAJI
KODI ZA KIMATAIFA
MAPATO MENGINEYO
A : KODI YA MAPATO
Na.
MAELEZO
VIWANGO
WAKAZI
WASIO WAKAZI
Kodi ya makampuni:
Kodi kwenye mapato yote ya kampuni
30%
30%
Makampuni yanayopata hasara kwa miaka 3
0.3% ya mauzo ya Hakuna
mwaka
Mfululizo (Isipokuwa kwenye biashara ya kilimo, huduma
ya afya au elimu).
Makampuni yaliyoandikishwa katika soko la mitaji la Dar
es Salaam yenye hisa zilizouzwa kwa umma kufikia
25%
25%
30% au zaidi katika kipindi cha miaka mitatu ya
mwanzo.
Kodi kwenye mapato ya Tawi la kampuni ya nje.
Hakuna
30%
Kodi kwenye Mapato yaTawi yanayorejeshwa nje, lisilo na
Hakuna
10%
ukazi.
WAKAZI
Kodi za zuio:
2
.
Gawio la hisa kutoka kampuni zilizoandikishwa kwenye DSE
5%
Gawio kutoka Kampuni mkazi kwenda kampuni nyingine mkazi ambayo
5%
inamiliki hisa 25% au zaidi.
Gawio la hisa kutoka kwenye makampuni mengine
10%
WASIO
WAKAZI
5%
Hakuna
10%
kamisheni kwa wakala kwa kutuma fedha kwa njia ya simu za mkononi
10%
Hakuna
Riba
Mrahaba
Huduma za Kiufundi na kiutawala (Uchimbaji madini, mft &gesi)
10%
15%
5%
10%
15%
15%
Usafirishaji nje ya nchi
Kipato kutokana na ukodishaji nyumba au ardhi
Ada ya bima
Malipo ya ada kwa wakurugenzi (kazi kwa muda)
Ada itokanayo na maliasili
Hakuna
5%
10%
0%
15%
15%
20%
5%
15%
15%
Ada ya huduma
5%
15%
Malipo kwa kuuza biadhaa
Serikalini au Taasisi za
Serikali
Aina nyingine za kodi ya zuio
2%
15%
15%
15%
Kukodisha ndege
10%
15%
Kukodisha rasilimali
0%
15%
nyinginezo (other assets)
MUHIMU: Malipo kwa mtu asiye mkazi kwa kukodisha ndege kwa mtu anayefanya biashara ya
usafiri wa anga yamesamehewa
Faida Halisi kwa kuuza rasilimali
Watu binafsi (Hisa na milki ya ardhi na majengo)
10%
20%
Makampuni
30%
30%
Misamaha katika mauzo ya rasilimali:
a) Mwenye makazi binafsi
Faida ya shilingi milioni 15 au pungufu.
b) Ardhi kwa ajili ya kilimo
Thamani ya soko chini ya shilingi milioni 10.
c) Hisa
Hisa zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar-es-Salaam
zinazomilikiwa na mkazi mwenye umiliki wa chini ya 25%
Kodi ya mkupuo mmoja:
(i) Mauzo ya ardhi na majengo
(ii) Usafirishaji wa bidhaa na abiria
nje ya nchi
10%
20%
Hakuna
5%
Kumbuka
(i)Kodi ya zuio hulipwa ndani ya siku Saba baada ya kila mwisho
wa mwezi wa makato.
(ii)Taarifa huwasilishwa TRA ndani ya siku 30 kila baada ya kipindi
cha miezi 6
Kodi ya Mapato ya mtu binafsi
Mapato kwa Mwezi
Mapato yasiyozidi sh. 170,000
Mapato yanayozidi sh170,000 lakini
hayazidi sh. 360,000
Mapato yanayozidi sh. 360,000
lakini hayazidi sh. 540,000
Mapato yanayozidi sh. 540,000
lakini hayazidi sh. 720,000
Mapato yanayozidi sh.720,000
Kiwango cha Kodi
Hakuna Kodi
12% ya mapato yanayozidi sh. 170,000
Shs.22,800 + 20% ya mapato yanayozidi
Sh. 360,000
Shs. 58,800+ 25% ya mapato yanayozidi sh.
540,000
Shs. 103,800 + 30% ya mapato yanayozidi sh.
720,000
Kiwango cha mwaka: Mapato yasiyozidi Sh. 2,040,000/= hayatozwi kodi.
Kumbuka:
1. Wafanyakazi wanaochangia kulingana na kifungu namba 12 cha Sheria ya Mfuko wa
Elimu ya mwaka 2001, mchango huo unaweza kusamehewa kodi endapo maombi
yatatumwa kwa Kamishna.
2.Mapato ya mwezi ni pamoja na mshahara, malipo kwa kazi za ziada, bonasi,
kamisheni, na marupurupu mingine ya ajira
3.Mapato ya asiye mkazi kwa mwajiri mkazi yatatozwa 15%, Japo jumla ya mapato ya
asiye mkazi hutozwa 20%
Marupurupu haya hayatozwi kodi pale ambapo mwajiri hana madai ya makato
kutokana na umiliki, matengenezo au matumizi ya gari.
Bei ya soko itatumika kukadiria marupurupu ya aina nyingine.
a. Gari:
Magari yatatozwa kodi kutokana na uwezo wa injini ya gari na
umri wa gari kulingana na jedwali lifuatalo:
Uwezo wa injini ya
Umri wa Gari
gari
Lisilozidi miaka
Linalozidi miaka
mitano
mitano
Usiozidi 1000c.c
250,000/=
125,000/=
Unaozidi 1000c.c na
500,000/=
250,000/=
usiozidi 2000c.c
Unaozidi 2000c.c na
1,000,000/=
500,000/=
usiozidi 3000c.c
Unaozidi 3000c.c
1,500,000/=
750,000/=
Viwango vya kodi kwa wafanyabiashara wadogo wakazi
Mauzo kwa mwaka
Uzingatiaji wa kifungu cha 80 cha Sheria ya
Kodi ya Mapato (Utunzaji wa kumbukumbu)
Mauzo yasiyozidi sh. 4,000,000
Hakijazingatiwa Kimezingatiwa (Kumbukumbu
(Kumbukumbu zinazoridhisha)
zisizoridhisha)
Hakuna
Hakuna
Mauzo yanayozidi sh. 4,000,000 na Sh. 200,000
yasiyozidi sh. 7,500,000
Mauzo yanayozidi sh.7,500,000 na Sh. 424,000
yasiyozidi sh. 11,500,000
4% ya mauzo yanayozidi sh.
4,000,000
Sh. 140,000 + 5% ya mauzo
yanayozidi sh.7,500,000
Mauzo yanayozidi
Sh. 728,000/=
sh. 340,000
sh. 11,500,000 na
+ 6% ya mauzo yanayozidi
yasiyozidi sh.
sh. 11,500,000
16,000,000
kwa mwaka.
Mauzo yanayozidi
Sh. 1,150,000
Sh. 610,000+ 7% ya mauzo yanayozidi
sh. 16,000,000 na
sh. 16,000,000 kwa mwaka.
yasiyozidi sh.
20,000,000
1. Endapo mauzo ghafi kwa mwaka yatazidi sh. 20,000,000/= ni lazima kutengeneza
hesabu za mizania kulingana na biashara.
2. Mauzo kwa mwaka zaidi ya 14m anunue na kutumia EFD
Uwasilishaji wa ritani na malipo ya kodi ya mapato.
a) Tarehe za malipo ya kodi ya awali kwa walipakodi wanaofunga hesabu kwa kufuata
mwaka wa kalenda*
i) Kabla au mnamo tarehe 31 Machi ii) Kabla au mnamo tarehe 30 Juni
iii) Kabla au mnamo tarehe 30 Septemba
iv) Kabla au mnamo tarehe 31 Desemba
*Malipo hufanyika katika kipindi cha miezi mitatu mitatu kutegemea tarehe ya kufunga
hesabu za biashara.
b) Ritani za mwisho wa mwaka wa malipo ya kodi: Huwasilishwa ndani ya
miezi sita tangu tarehe ya kufunga hesabu za mwaka wa mapato.
c) Riba kutokana na ucheleweshaji wa malipo: Ucheleweshaji malipo
unaambatana na kutozwa riba kwa kiwango kilichoidhinishwa na benki kuu
kwa wakati huo kujumlisha na 5% kwa mwaka.
d)Faini ya kutotumia EFD:
i. Faini ya awali
ii. Kushindwa kutumia mashine za kodi za kielektroniki (EFD) au kutotoa risiti za
kielektroniki, tozo la faini ya Sh 3,000,000 au kifungo kisichozidi miezi 12
kitatolewa au vyote.
iii. Kuifanya mashine isifanye kazi na mengineyo si chini ya sh. M1 au kifungo
cha miezi 3 au vyote
iv. Kutodai risiti ni mara 2 ya kodi iliyokwepwa
Kodi ya kuendeleza ufundi stadi (SDL)
Kiwango ni 5% ya malipo yote aliyolipa mwajiri kwa wafanyakazi wake
kwa mwezi husika.(Tanzania Bara na Zanzibar)
MUHIMU:
(i)Taasisi za Serikali ambazo hazitegemei ruzuku ya Serikali pia
zinatakiwa kulipa SDL
(ii)Jumla ya malipo ni majumuisho ya mshahara, malipo ya likizo, likizo
ya ugonjwa, malipo yoyote yanayohusisha likizo, kamisheni, mafao,
bonasi, malipo ya kujikimu, usafiri, malipo ya kujiburudisha au malipo
yoyote yanayoendana na utendaji kazi husika isipokuwa malipo yale
yaliyotumika katika utekelezaji wa moja kwa moja wa kazi ya mwajiri.
Punguzo katika rasilimali na viwango vyake
Daraja
Maelezo
1*
Viwango
Kompyuta pamoja na vifaa vinavyohusiana na kompyuta, mashine zinazoshughulika na takwimu,
vifaa/mashine zinazojiendesha zenyewe, mabasi makubwa na madogo yenye uwezo wa kubeba abiria
37.5%
wasiozidi 30, magari ya mizigo yanayobeba uzito sio chini ya tani 7, mashine nzito zinazotembea nchi
kavu na zile zinazohusika na ujenzi.
2* Mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 30 au zaidi, magari makubwa kwa ajili ya kazi maalum,
matrekta na matrekta yaliyojengewa makontena, reli, garimoshi na mashine zake, meli,
matishari(barges), vyelezo(tags), na mashine nyingine zinazojiendesha zenyewe, mitambo na mashine
25%
zake pamoja na mashine ya upepo, jenereta za umeme, na mashine za usambazaji) zinazotumika
katika uzalishaji au katika shughuli za madini, mitambo na mashine maalum kwa ajili ya matumizi ya
jamii, na mashine au mitambo mingine kwa ajili ya umwagiliaji na mashine zake.
3* Samani za ofisini, vifaa vya ofisini na mashine/mitambo, pamoja na rasilimali ambazo hazikujumuishwa
12.5%
kwenye madaraja mengine.
4** Uchunguzi wa maliasili, na hati miliki za uzalishaji maliasili, pamoja na matumizi yanayofanyika wakati
20%
wa kutafiti, kuzalisha, na kuendeleza maliasili.
5** Majengo na sura mbali mbali za ujenzi, mabwawa, hifadhi ya
maji, uzio, na shughuli nyingine za kilimo zenye asili ya kudumu
20%
kwa muda mrefu, shughuli za mifugo na uvuvi
6** Majengo, sura mbalimbali za ujenzi (structures), na shughuli
nyingine zinazofananana hizi zenye asili ya kudumu kwa muda 5%
mrefu ambazo hazipo katika daraja la 5.
7** Rasilimali zinazokosekana katika daraja la 4 na zisizoshikika.
Hugawanywa kwa muda
wa maisha ya rasilimali.
8** Mitambo na mashine (pamoja na mashine za upepo, jenereta za
umeme, na mashine za usambazaji) zinazotumika kwenye
kilimo, pamoja na mashine za kodi za kielektroniki (EFD) kwa
100%
wasio sajiliwa na VAT, Vifaa kwa matumizi ya utafutaji wa madini
na mafuta
Kumbuka:
1* Uchakavu hukokotolewa kwenye thamani ya rasilimali ambayo tayari imeshapunguzwa (Diminishing
Value Method).
2** Thamani ya rasilimali kwa mwaka wa kwanza ndio inayotumika katika kukokotoa uchakavu kila
mwaka (Straight Line Method).
B. KODI ZA MLAJI
KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT)
(i) Usajili wa VAT
Kiwango cha usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani: Kiwango cha mauzo yanayotozwa kodi cha zaidi
ya shilingi milioni arobaini (milioni 40) kwa mwaka, au kiwango kinachozidi milioni 10 kutokakana na
mauzo yanayotozwa kodi ya miezi mitatu inayofuatana.
(i) Viwango vya VAT
Aina ya bidhaa na au huduma zinazohusika
Kiwango (VAT)
Bidhaa na huduma zinazotozwa kodi - Tanzania bara
18%
Uagizaji na uingizaji wa bidhaa na huduma toka nje kuingia Tanzania bara.
18%
Uuzaji wa bidhaa nje ya nchi.
0%
(i) Unafuu maalum wa VAT
Baadhi ya watu au asasi zinapewa unafuu maalum wa Kodi ya
Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha 100% au 45% ya kodi
ya bidhaa au huduma Kwa mujibu wa jedwali la 3 la Sheria ya
Kodi ya Ongezeko la Thamani
(i) Uwasilishaji wa Ritani ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
Bidhaa na Huduma zitolewazo hapa nchini, siku ya mwisho ya kazi ya mwezi unaofuata
mwezi wa biashara
Bidhaa toka nje - Pindi malipo ya Ushuru wa Forodha yanapolipwa
(i) Marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani:
 Katika kipindi cha siku thelathini (30) baada ya kuwasilisha hati ya uthibitisho kutoka
kwa mkaguzi aliyesajiliwa kama mtaalamu na mshauri wa kodi.
 Marejesho ya mara kwa mara ya Kodi ya Ongezeko la Thamani:- Wafanyabiashara
wenye marejesho yenye asili hii wanaruhusiwa kuwasilisha maombi ya marejesho
yao kila mwezi.
MUHIMU:
Kila mfanyabiashara aliyesajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani anatakiwa kutumia mashine
za kodi za kielektroniki (EFD).
Ushuru wa Stempu
Maelezo
(i) Kuhamisha
(ii) Kwenye ardhi kwa ajili ya
kilimo
(i) Hati za kisheria na mikataba
za biashara
Msamaha:
Risiti kwenye mauzo au huduma inayohusiana na biashara
Kuhamisha umiliki wa mali (Assets) katika chombo maalum kwa mdhumuni ya kutoa dhamana
zinazotegemea mali hiyo.
MUHIMU:
Ushuru wa Stempu kwenye hati mbalimbali, unapaswa kulipwa ndani ya siku 30 baada ya
kusaini mkataba husika.
13
Ushuru wa Forodha
Bidhaa
Kiwango cha Ushuru
(i) Bidhaa za Mtaji, Malighafi zitumikazo kuzalisha
0%
bidhaa, dawa na vifaa vya hospitali, Jembe la mkono,
matrekta ya kilimo na pembejeo za kilimo.
(ii) Bidhaa ambazo hazijakamilika
10%
(iii) Bidhaa za mlaji na zilizokamilika
25%
(iv) Baadhi ya bidhaa hutozwa ushuru zaidi ya 25% kwa lengo la kulinda viwanda vya
ndani. Hii ni pamoja na
 Maziwa yaliyosindikwa na bidhaa za aina hiyo,
 Maziwa ya mtindi na mafuta ya maziwa yaliyoongezwa ladha,
 Sukari itokanayo na miwa au viazi na bidhaa za aina hiyo,
 Magunia ya katani,
 Vitenge, Khanga na Nguo za mitumba.
15.
16.
Ushuru wa mafuta ya petroli na Sh. 263 kwa lita
dizeli
Ushuru wa huduma za viwanja vya ndege
Safari za nje
Dola za kimarekani 40
Safari za ndani ya nchi
Sh. 10,000
17.
18.
19.
Ada za huduma ya bandari
Kwa wasafiri wakazi
Sh. 500/Kwa wageni
Dola za kimarekani 5
Ada ya usajili wa chombo cha moto kwa mara ya kwanza
Ada ya kusajili gari
Sh. 150,000/Ada ya kusajili pikipiki
Sh. 45,000/Ada ya usajili kwa namba binafsi
Sh. 5,000,000 kwa miaka 3
Ada ya mwaka ya gari ni kama ifuatavyo
Ujazo wa Injini
Ada kwa mwaka
Usiozidi 500 cc
Sh. 50,000/501 - 1,500 cc
Sh. 150,000/1,500 - 2,500 cc
Sh. 200,000/zaidi ya 2,500 cc
Sh. 250,000/Trekta kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kilimo, pikipiki na Yamesamehewa
Bajaj
kulipa ada za mwaka
MUHIMU: Ada za magari zinalipwa kwa njia ya simu za kiganjani,wakala wa
Maxmalipo na Benki
20
21.
Ada ya ukaguzi wa chombo cha kuzima moto
Gari/Pikipiki yenye ujazo kati ya 1cc mpaka 500cc
Sh 10,000
Gari/Pikipiki yenye ujazo kati ya 500cc na 1500cc
Sh 20,000
Gari/Pikipiki yenye ujazo kati ya 1500cc na 2500cc
Sh 30,000
Gari/Pikipiki yenye ujazo zaidi ya 2500cc
Sh 40,000
Ada ya kuhamisha umiliki wa chombo cha moto



ASANTENI KWA KUNISIKILIZA
MASWALI, MAONI, CHANGAMOTO,
USHAURI ……………
NAMBA ZA SIMU BURE UKIWA NA
MAULIZO 0786-800000, 0713-800333, 0800110016 VODA AND TTCL