Transcript TAXONOMY
UTANGULIZI UCHAMBUZI WA VIUMBE www.bionet-intl.org | [email protected] Mchanganuo huu umekusanywa na BioNET (Posa Skelton & Kornelia Rassmann) kwa ushirikiano na wafwatao Ufahamu wa ulimwengu uliokuzunguka! Henrik Enghoff Natural History Museum of Denmark Ulf Gärdenfors ArtDatabanken, Swedish Species Information Centre Fabian Haas African Insect Science for Food and Health Chris Lyal Natural History Museum, London Yves Samyn 1 Royal Belgian Institute of Natural Sciences Kiswahili: Melckzedeck K. M. Osore, Western Indian Ocean Marine Science Association (WIOMSA) Ensifera ensifera (Boissonneau, 1840) Mchoraji: Ernst Haeckel UTANGULIZI MIMI NI NANI? 2 Je, unataka kujua? Muulize mchambuzi wa viumbe Au bonyeza Kiunganishi hiki … © Stuart Wynne UCHAMBUZI WA VIUMBE NI 3 UCHAMBUZI WA VIUMBE NI … Sayansi ya Kugundua Kutoa jina Kueleza Kuainisha viumbe Ili kuelewa bioanuai (na mengine yanayohusu…) Neno Taxonomy asili yake ni maneno mawili ya kigiriki: Taxis = mgao/mpangilio, nomos = Sheria UCHAMBUZI WA VIUMBE NI 4 KUGUNDUA Samaki aina ya Dracula (Dracula fish) Danionella dracula Amegunduliwa nchini Burma Ameelezewa 2009 © Ralf Britz | Natural History Museum, London Ugunduzi wa viumbe wapya ndio hatua ya kwanza ya uchambuzi wa viumbe. Kila mwaka viumbe wapya wanagunduliwa kote ulimwenguni, kadri wachambuzi wanapo tembelea maeneo mapya, au vinapopatikana vitendea kazi vipya vya kuchambua sampuli UCHAMBUZI WA VIUMBE NI 5 KUTOA JINA Electrolux addisoni (Compagno & Heemstra, 2007) Jina lina muundo gani? Jina la kisayansi ni hati inayo tambulisha viumbe wote Photo: Phil Heemstra | Wikimedia Commons Sio fagio lako la kawaida! UCHAMBUZI WA VIUMBE NI 6 KUELEZEA Sehemu ya mchakato huu inahusu kulinganisha viumbe wanao husiana karibu ili kuthibitisha kama kiumbe fulani ni wa aina mpya. Hypsiboas calcaratus (Troschel, 1848) | Photo: P. J. R. Kok UCHAMBUZI WA VIUMBE NI 7 UAINISHAJI Kingdom - Animalia Phylum - Chordata Class - Mammalia Infraclass - Eutheria Order - Artiodactyla Family - Bovidae Subfamily - Caprinae Genus - Ovis Species - Ovis aries Jina langu ni Dolly! MAJINA NI MUHIMU UAINISHAJI ni muhimu katika 8 maisha yako ya kila siku Uainishaji ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Hutuwezesha kupanga vitu katika utaratibu unaofaa kama uhakiki mali katika (Supermarket) maduka makubwa. Je, unategemea kuzipata bidhaa za maziwa zimeorodheshwa pembeni mwa zile za usafi wa nyumbani? Photo: G. R. South MAJINA NI MUHIMU MAJINA ni muhimu katika 9 siku maisha yako ya kila Photo: Sergio Kaminski | Wikimedia commons Drawing: Peter Aertsen ? Hebu fikiria kama yasingekuwepo majina ya watu na vitu… Photo: Wikimedia commons | public domain MAJINA NI MUHIMU MAJINA yanahitajika 10 kwa mawasiliano Muis Panya マウス Ποντίκι Souris 쥐 فأس Мышь Mouse Mus Maus © Kornelia Rassmann Ratón 老鼠 Majina ya kawaida au ya lugha za asili ni muhimu kwa mawasiliano ya kila siku lakini matumizi yake ni finyu kutegemea mahali na lugha MAJINA NI MUHIMU MAJINA YA KISAYANSI 11 kwa mawasiliano kimataifa Alternanthera philoxeroides Bursaphelenchus xylophilus Photo: Gary Buckingham USDA Agricultural Research Service, United States | forestryimages.org Photo: L.D. Dwinell USDA Forest Service, United States | forestryimages.org Pseudophilotes sinaicus Photo: BioNET-NAFRINET Kutumia jina la kisayansi ni hakikisho kwamba tunazungumza kuhusu kiumbe fulani bila pingamizi kutokana na eneo letu kijiografia au lugha MAJINA NI MUHIMU 12 Kulijua JINA SAHIHI - kunaokoa fedha Photo: Oliver Spalt | Wikimedia commons Scotinophara lurida Photo: Natasha Wright, Florida Department of Agriculture and Consumer Services, Bugwood.org Elimu ya uchambuzi imesaidia kubaini aina ya kombamwiko weusi 24 tofauti inchini Ufilipino, na kati ya hao ni 2 pekee ndiyo waharibifu walioshambulia mchele. Ujuzi huu anaokoa mamilioni ya dola katika matumizi ya viuwa tilifu vya wadudu kwa kuwadhibiti na husaidia kulinda mazingira. See case study no. 39 MAJINA NI MUHIMU KUTOJUA JINA 13 - kunaweza kuua! Boletus aurantiacus | Photo: Wikimedia commons | public domain Nile au nisile? Muulize mchambuzi wa uyoga (mycologist)! MAJINA NI MUHIMU 14 LINNAEUS "Ikiwa hauyajui majina ya vitu, ni kazi bure kuelewa umuhimu wa vitu hivyo" Critica Botanica 1737 Carl von Linné (au Linnaeus), ndiye “baba wa uchambuzi wa viumbe”, yeye ndiye aliyeweka msingi wa mfumo wa kisasa wa majina – wakuwapa viumbe majina kisayansi. Carl von Linné, 1707-1778 Drawing: AMNH Library Linnaeus ndiye alieanzisha uainishaji thabiti na sahihi unaohitajika kuieleza bioanuwai, bidhaa za biashara, ununuzi wa mbegu za ukulima, udhibiti wa wadudu waharibifu, au ushughulikiaji wa aina nyingine ya maeneo mengi yanayohitaji ujuzi wa uchambuzi wa viumbe. UCHAMBUZI - MANUFAA 15 UMUHIMU NA UHUSIANO NA BIOANUWAI © A. De Kesel Uelewa wa uchambuzi wa viumbe una manufaa kwa sekta nyingi zinazoshirikiana kufanya kazi moja kwa moja au kwa namna mbalimbali na bioanuwai. Ikiwa unajihusisha na biashara ya kuigiza na kutoa bidhaa inchini, uhakiki wa chakula, madawa, afya ya jamii, mabadiliko ya tabia inchi, usalama wa viumbe, kilimo, kilimo cha bustani, uvuvi, sayansi ya mifugo, madini, utalii, au hata kazi za jikoni, masuala ya sekta hizi zote yanahitaji elimu ya dunia hai. Uelewa wa uchambuzi wa viumbe unatuwezesha kuelewa uanuwai wetu wa viumbe. UCHAMBUZI - MANUFAA 16 UFAHAMU WA DUNIA HAI © Kornelia Rassmann Utofauti wa viumbe mbali mbali unafanya dunia yetu iwe ya utata. Uelewa wa uchambuzi wa viumbe unasaidia kufahamu huu utofauti kwa njia ya kupanga na kwa kuuweka ulimwengu wetu katika makundi yanayo eleweka vizuri. UCHAMBUZI - MANUFAA UCHAMBUZI WA VIUMBE manufaa kwa ustawi wa binadamu Photo: Bigstockphoto.com Photo: ??? Photo: Posa A. Skelton 17 Huleta uelewa wa msingi katika maeneo mbali mabli ya manufaa kwa mwanadamu yakiwemo uhifadhi wa bioanuwai, kukabiliana na madadiliko ya tabia nchi, usalama wa viumbe , ukulima,ufugaji samaki, afya, utalii, biashara na mengine mengi. UCHAMBUZI - MANUFAA 18 UCHAMBUZI WA VIUMBE ni Swala muhimu kimataifa Husaidia katika maamuzi mema ya sera na udhibiti, hutoa muongozo katika huduma za msingi (kwa mfano katika ukulima, dawa) na ni msingi wa miundombinu ya Malengo ya Milennia yanayohusu kupunguza umaskini, kupambana na magonjwa na kuendeleza mazingira. © Kornelia Rassmann UCHAMBUZI - MANUFAA 19 MSINGI WA ELIMU kwa sayansi nyingine Photo: G. R. South Photo: BioNET-MESOAMERINET Elimu ya uchambuzi wa viumbe husaidia maeneo mbalimbali ya kisayansi pamoja na sayansi ya hifadhi, biolojia ya uzinduzi, biologia ya uvumbuzi, ikolojia, biojiografia, dawa na mengine mengi. UCHAMBUZI - MANUFAA 20 Uhifadhi wa BIOANUWAI Kwa kutambua bioanuwai zetu tunaweza kuzihifadhi na kuzitumia kwa uendelevu. © Posa A. Skelton Kwa mfano: Hifadhi mbalimbali zimeanzishwa kwa sababu ya kugundulika kuwa maeneo ya viumbe hadimuni au maeneo hayo kutambulika kuwa makazi ya viumbe waliodhaniwa kuwa wameshatoweka. Brachylophus bulabula – aina mpya ya Iguana (aina ya mjusi mkubwa sana) anaye patikana tu katika nchi ya Fiji. UCHAMBUZI - MANUFAA 21 TABIA NCHI kukabiliana na mabadiliko Kusambaa kwa viumbe kutaathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi. Maktaba ya viumbe huchangia pakubwa kuhifadhi kumbukumbu za kudumu za kihistoria jinsi viumbe wa aina mbali mbali walivyo sambaa, na kutoa fursa nzuri ya kutabiri uwezekano wa © Gert Brovad viumbe hao kutoweka, kuenea kwa wadudu waharibifu na maambukizi ya magonjwa na kusaidia katika hatua za kukabiliana na mazingira. UCHAMBUZI - MANUFAA 22 VIUMBE WAVAMIZI & WADUDU WAHARIBIFU Usimamizi mzuri Utumizi wa kombamwiko wa aina ya Cyrtobagous salviniae kudhibiti kuenea kwa gugu maji mkubwa wa aina ya Salvinia molesta. Viumbe wavamizi huathiri karibu kila aina ya mazingira duniani na ni tishio kubwa kwa bioanuai. Ili kuepukana na hathari hizi, wachambuzi wa viumbe wenye uzoefu na vifaa vya kutosha wanahitajika kutoa taarifa upesi na kutambua haraka aina na vifaa muhimu vinavyohitajika kutumiwa na viongozi na wanajamii. Photo: Katherine Parys, Louisiana State University, United States See case study no. 27 UCHAMBUZI - MANUFAA 23 SERA / MAAMUZI Viumbe wanaoorodheshwa na Mkataba kwa ajili ya Biashara ya Kimataifa ya Viumbe Wanaotishia Kuangamia (ujulikanao kama CITES) hulindwa kwa viwango na aina tofauti dhidi ya matumizi holela. Karibu aina zote za mimea hii zimeorodheshwa na CITES, idadi kubwa katika Kiambatanisho cha pili (appendix II) ambacho kinajumuisha aina ambazo sasa hazitishiwi na kuangamia lakini zinaweza kuangamia kama biashara haitadhibitiwa kwa makini. Uelewa wa uchambuzi wa viumbe husaidia kuratibu sera na mfumo wa muongozo. Kwa mfano: Mkataba kwa ajili ya Biashara ya Kimataifa ya Viumbe Wanaotishia Kuangamia (CITES ), hutegemea taarifa sahihi za uchambuzi kufanikisha udhibiti mzuri wa biashara ya aina ya viumbe hao, kama vile orchids (aina ya mmea wa maua). © Martin Voggenreiter clockwise: Ophrys fusca, Orchis italica, Cypripedium calceolus, Ophrys lutea UCHAMBUZI - MANUFAA 24 UGUNDUZI WA VIUMBE HAI & AFYA Mimea yenye dawa ni muhimu katika sehemu nyingi duniani, na uchambuzi wa viumbe hutumika kutambua mimea yenye manufaa, kama vile tunda la Noni. © Posa Skelton - Morinda citrifolia © Stuart Wynne - Niphates digitalis Sifongo wa baharini (marine sponges) ni chanzo kizuri cha misombo ya muhimu kwa kutengeneza madawa, viungo vya chakula na vifaa vingine kwa matumizi ya kibiashara. Elimu ya uchambuzi wa viumbe husaidia kugundua na kubainisha haya. UCHAMBUZI - MANUFAA 25 UHAKIKA WA VIUMBE HAI & BIASHARA Mdudu asiye fahamika anapopatikana katika shehena ya kilimo, anaweza kusababisha kupungua kwa kasi ya biashara duniani na shehena husika inaweza kucheleweshwa kwa muda mrefu na gharama kubwa ikisubiri mdudu huyo atambuliwe barabara. Katika hali hii, uelewa wa uchambuzi wa viumbe unaweza kuokoa fedha. Madai ya kuwepo kwa aina fulani ya mba (anaye julikana kama Karnal bunt fungus) katika shehena ya ngano toka nchi ya Australia kulisababisha kukataliwa kwa shehena hiyo kuingia nchini Pakistan. Kwa kutumia uchambuzi wa viumbe, ilibainika kwamba chembechembe zilikua sio za mba husika ambao hutambulika kwa kuvamia maeneo. Kutatuliwa kwa swala hilo kulizuia kusitishwa kwa biashara ya ngano yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni nne. For a similar case study see case study no. 8 Tilletia indica|Photo: Ruben Durán, Washington State University, Bugwood.org UCHAMBUZI - MANUFAA 26 KUPUNGUZA UMASKINI& UHAKIKA WA CHAKULA © bluerain | Dreamstime.de Kupunguza umaskini, uhakika wa chakula na uhifadhi wa viumbe hai huenda sambamba. Kimataifa, umaskini na uhaba wa chakula mara nyingi hupatikana sehemu zilizopoteza idadi kubwa ya viumbe hai. Uelewa wa uchambuzi wa viumbe husaidia kuendeleza mazingira yenye afya katika nchi zinazoendelea, ambapo hupatikana kiwango kikubwa cha bioanuai duniani, lakini pia idadi kubwa ya watu wa kipato cha chini vijijini wakitishiwa na upungufu wa bioanuai. © imagedirekt.de CHANGAMOTO UCHAMBUZI WA VIUMBE: 27 kuendeleza elimu yetu Viumbe wapatao 18,500 wa aina impya waligunduliwa mwaka 2007 Hadi sasa, aina takriban milioni 1.8 wamegunduliwa. Inakisiwa yakwamba idadi kamili ni kati ya milioni 5 hadi 50. Tafakari mfano huu: Katika utafiti uliyohusisha kiumbe aitwaye cricket (anayefana kama panzi) wa nchini Australia, asilimia 76 ya viumbe hao waligunduliwa kuwa wapya. Unka boreena (Otte & Alexander) | Photo: David Rentz From Otte, D., and R. D. Alexander. 1983. The Australian Crickets (Orthoptera: Gryllidae). Academy of Natural Sciences of Philadelphia. UKUBWA tu wa KUKUMBATIWA CHANGAMOTO Sio hoja © Tatiana Goydenko | Dreamstime.com © Josef Szasz–Fabian | Dreamstime.com 28 Uchambuzi unahusu sio tu viumbe wenye karama wanaojulikana na kila mtu, kama vile Nyangumi, na wanyama wengine wakubwa wanaoishi nje ya Afrika kama Giant Panda, na Polar bear (aina ya dubu). Unahusu pia viumbe wadogo wanaosababisha mazingira yetu kustawi. Baadhi ya viumbe hawa wadogo wadogo wanaweza kutufaa maishani mwetu (mfano chachu) ama kutuathiri (mfano mbu anaye eneza malaria)! CHANGAMOTO DUNIA ina SHANGAZA Hippocampus satomiae | © Rudie Kuiter © John Sear 29 Sayari yetu ina maajabu mengi ya kushangaza na hazina nyingi – viumbe wapya hugunduliwa kila siku lakini mwanadamu (Homo sapiens kwa jina la kisayansi) haupi ugunduzi huu thamani inavyostahili. Kiumbe huyu aitwaye Seahorse (mwenye umbile la farasi mdogo sana anayeishi baharini) aliyegunduliwa rasmi mwaka 2008 ndiye mnyama mdogo sana wa aina yake. Ana urefu wa 13.8 mm na kimo chake ni takriban 11.5mm. Una hamu ya kujua mengi kuhusu UCHAMBUZI WA VIUMBE? MAELEZO Hapa utapata maelezo zaidi kuhusu... Uchambuzi wa viumbe Global Taxonomy Initiative (GTI, Convention on Biological Diversity)| European Distributed Institute of Taxonomy (EDIT) |Natural History Museum, London, UK) |Royal Belgian Institute of Natural Sciences | BioNET-International Aina ya viumbe Encyclopedia of Life (EoL) |Wikispecies | ARKive |IUCN Red List | Top 10 New Species Discoveries International Institute for Species Exploration (IIES) | Tree of Life | Census of Marine Life (CoML) | Catalogue of Life (ITIS, Species2000) | Global Biodiversity Information Facility (GBIF) Umuhimu wa uchambuzi, aina ya viumbe & bioanuai BioNET case studies |GTI case study on taxonomy & climate change | Convention on Biological Diversity – 2010 International Year of Biodiversity 30 Photos: BioNET-SAFRINET, BioNET ANDINONET, BioNET-EAFRINET, BioNET-NAFRINET