MTAALA WA UICC WA HPV na SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a.
Download ReportTranscript MTAALA WA UICC WA HPV na SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a.
MTAALA WA UICC WA HPV na SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 01 Sura ya 8.a. Mpango wa mawasiliano ya kiafya kwa mabadiliko Joe B. Harford, PhD Taasisi ya Kitaifa ya Saratani Bethesda, Marekani UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 02 Mawasiliano ya kiafya (1) • Ufafanuzi: utafiti na matumizi ya mikakati ya mawasiliano kufahamisha na kuathiri uamuzi wa kibinafsi na wa kijamii ambao unaimarisha afya • Hadhira lengwa: umma wa kawaida, wafanyakazi wa huduma za afya, au wabuni sera au makundi yoyote madogo miongoni mwa haya UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 03 Mawasiliano ya kiafya (2) • Dhamira: ustawishaji wa ujumla wa afya ambao shirika au wakala hulenga kuunda • Malengo: matokeo maalum ya mawasiliano yanayolenga kusaidia dhamira ya jumla - Yanayofikika (yaani, yenye uhalisi) - Yanayopimika - Yaliyo na umaalum wa muda • Mkakati: mitazamo ya jumla ambayo inatokana na, na kuchangia katika kufikia dhamira na malengo yaliyobainishwa UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 04 Mawasiliano ya kiafya (3) • Hadhira: lengo lililonuiwa la mawasiliano • Kitengwa: seti ndogo ya hadhira iliyonuiwa ambayo inatofautiana kwa njia ambazo zinaathiri mtazamo unaochukuliwa ili kuwasiliana • Ujumbe: funzo la kuchukua nyumbani linalolenga mabadiliko yanayosababisha afya iliyostawishwa • Mazingira: machaguo ya mahali na muda wa kufikia hadhira nuiwa kwa ujumbe • Njia: Vifaa vya kufikisha ujumbe huo UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 05 Mpango wa mawasiliano Itifaki katika kuunda mpango: Dhamira Malengo 1. Weka dhamira 2. Fafanua malengo 3. Buni mikakati & mbinu UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Mikakati & Mbinu Slaidi 06 Kile ambacho mawasiliano ya kiafya yanaweza kufanya (1) • Kuongeza maarifa na ufahamu wa swala, tatizo au suluhisho la kiafya • Kuathiri utambuzi, imani na mitazamo ambayo inaweza kubadilisha kaida za kijamii • Kuchochea hatua • Kudhihirisha au kueleza ujuzi wa kiafya kwa mifano UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 07 Kile ambacho mawasiliano ya kiafya yanaweza kufanya (2) • Kuimarisha maarifa, mitazamo, au mienendo • Kuonyesha manufaa ya mabadiliko ya mwenendo • Kutetea kauli katika swala au sera ya afya • Kuongeza utashi au msaada wa huduma za afya • Kuondoa uwongo na na kuelewa visivyo • Kutia nguvu uhusiano wa kimashirika UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 08 Athari ya mawasiliano ya kiafya • Kwa watu binafsi: kubadilisha ufahamu, mitazamo, ujuzi na ahadi kuwa mabadiliko ya mwenendo • Kwa makundi: athari muhimu katika afya ya watu binafsi kwenye kundi • Katika mashirika: kueneza ujumbe miongoni mwa wale walio kwenye mashirika hayo • Katika jamii: kubadilisha afya ya watu binafsi kupitia katika mabadiliko kwenye kaida za kijamii UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 09 Upungufu wa mawasiliano ya kiafya • Hayawezi kufidia huduma za afya au mfiko wa huduma za afya usiotosha • Hayazalishi mabadiliko endelevu katika mienendo changamani ya kiafya bila utaratibu mkubwa zaidi wa mabadiliko (k.m., kushughulikia mfiko, kanuni na sera) • Hayana ufanisi sawa wa kushughulikia maswala changamani au yale yanayoleta mabishano UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 10 Mawasiliano ya kiafya pamoja na mikakati mingine • Yanaweza kusababisha mabadiliko endelevu ambapo mtu binafsi huchukua na kudumisha mwenendo mpya wa kiafya au shirika au jamii huchukua na kudumisha mwelekeo mpya wa sera • Yanaweza kushinda vizuizi/matatizo ya kimfumo kama vile mfiko usiotosha kwa huduma za kiafya UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 11 Mitazamo unganishi • Mawasiliano kwa umma wa kawaida, wagonjwa, watoa huduma za afya, wabuni sera (yeyote anayehitajika kufanya au kurahisisha mabadiliko) • Mabadiliko ya sera (k.m., sheria mpya, kanuni, taratibu za utendaji) • Mabadiliko ya kiteknolojia (k.m., bidhaa mpya au iliyosanifishwa upya, dawa, huduma, au matibabu au mabadiliko katika uwasilishaji wa bidhaa zilizoko, dawa, huduma, au matibabu) UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 12 Jitihada za mawasiliano: maswali • Je, shirika letu linao (au linaweza kupata) utaalamu na rasilimali zinazohitajika? • Je, shirika letu linayo mamlaka au udhamini unaohitajika? • Je, jitihada zetu zitakuwa zinarudufu zile za wengine? • Je, shirika letu linao muda na rasilimali za kiwango kipi kushughulikia swala hili? • Je ni nini, kama kunacho kitu, kinachoweza kufanikishwa kwa uhalisi ikizingatiwa vikwazo vyetu vya muda na rasilimali? UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 13 Uwongo kuhusu mpango wa mawasiliano • Utaratibu wetu hauwezi kumudu utafiti wa hadhira • Utafiti wa soko hauhusiki katika utaratibu wa afya • Hatuna muda wa kupanga - tunahitaji kuanza utaratibu sasa • Ni bora zaidi kutumia njia ambazo tumezizoea na tumezitumia awali • Ikiwa tutatumia njia moja tu, tunafaa kutumia vyombo vya habari • Kutumia vyombo vya mawasiliano vya tarakimu ongezi kunahitaji uwezo mkubwa wa kiufundi ambao tutapata ugumu kuuhimili • Kutokuwa na vyombo vya mawasiliano vya tarakimu ongezi katika utaratibu kutaonyesha kwamba tumepitwa na wakati na hatuna ujuzi wa kiteknolojia UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 14 Muhtasari wa jumla wa mchakato wa mawasiliano 1 4 Kufanya mpango & ukuzaji wa mkakati Kukadiria ufanisi & kufanya marekebisho UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Kukuza & kufanya majaribu ya awali kwa dhana, ujumbe & nyenzo 2 Kutekeleza utaratibu 3 Slaidi 15 Sifa bainifu za kampeni zilizo na ufanisi (1) • Dhamira ya kampeni imefafanuliwa kwa ufanisi • Hadhira iliyonuiwa imebainishwa vyema • Ujumbe umebuniwa kwa ufanisi • Nyenzo zimejaribiwa awali na kusahihishwa kwa ufanisi • Kampeni imetekelezwa kwa ufanisi UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 16 Sifa bainifu za kampeni zilizo na ufanisi (2) • Dhamira ya kampeni imefafanuliwa kwa ufanisi - Tambua dhamira kubwa zaidi - Bainisha ni kiungo kipi (viungo vipi) cha dhamira kinaweza kuathiriwa na kampeni - Eleza malengo maalum yaliyo chini ya dhamira - Fungamanisha malengo haya kwenye mpango wa kampeni UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 17 Sifa bainifu za kampeni zilizo na ufanisi (3) • Hadhira iliyonuiwa imebainishwa vyema - Tambulisha kundi ambalo linalengwa na kampeni - Dhukuru kutambulisha makundi madogo kwa ujumbe uliorekebishwa kuyafaa - Jifunze mambo mengi zaidi iwezekanavyo kuhusu hadhira iliyonuiwa/zilizonuiwa - Ongezea taarifa kuhusu imani, vitendo vya sasa, na mazingira ya kimaumbile kwa taarifa ya kidemografia UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 18 Sifa bainifu za kampeni zilizo na ufanisi (4) • Ujumbe uliobuniwa kwa ufanisi - Changia mawazo ili kubuni ujumbe ambao unaweza kuingiliana vyema na dhamira ya kampeni na hadhira iliyonuiwa/zilizonuiwa - Tambua njia na asili zinazofikiriwa kuwa za kusadikika na za kushawishi na hadhira iliyonuiwa/zilizonuiwa - Dhukuru muda na mahali bora zaidi pa kufikia hadhira na tayarisha ujumbe vilivyo - Teua baadhi ya ujumbe unaowezekana na panga kuufanyia majaribio ya awali UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 19 Sifa bainifu za kampeni zilizo na ufanisi (5) • Nyenzo zilizojaribiwa awali na kusahihishwa kwa ufanisi - Teua mbinu za kufanya majaribio ya awali (k.m., makundi lengwa, mahojiano ya kina, n.k.) - Fanya majribio ya awali kwa ujumbe na nyenzo na wale wanaoshiriki sifa za hadhira nuiwa - Chukua muda katika kusahihisha ujumbe na nyenzo kulingana na matokeo yaliyopatikana kutoka kwa majaribio ya awali UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 20 Sifa bainifu za kampeni zilizo na ufanisi (6) • Kampeni zimetekelezwa kwa ufanisi - Kufuata mipango iliyokuzwa kwa kampeni - Wasiliana na watekelezaji na washirika inavyohitajika ili kudumisha utekelezaji mwororo - Anza kutathmini mpango na michakato ya kampeni kuanzia siku ya kwanza kundelea mbele UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 21 Muhtasari wa jumla wa mchakato wa mawasiliano Unahitajika kwa mawasiliano yanayolenga idadi ya watu wa kawaida, wafanyakazi wa huduma za afya na wabuni sera 1 4 Kufanya mpango & ukuzaji wa mkakati Kukadiria ufanisi & kufanya marekebisho UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Kukuza & kufanya majaribio ya awali kwa dhana, ujumbe & nyenzo 2 Kutekeleza utaratibu 3 Slaidi 22 Kwa nini kupanga ni muhimu (1) • Kupanga husaidia: - Kuelewa swala unalolishughulikia - Kubainisha wajibu unaofaa kwa kampeni - Kutambua mitazamo ya kusababisha na kuunga mkono mabadiliko yanayotamanika - Kuanzisha mchakato wa utaratibu ulio na mantiki UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 23 Ni kwa nini kupanga ni muhimu (2) • Kupanga husaidia: - Kuunda utaratibu unaounga mkono malengo yaliyofafanuliwa - Kuweka aula ili kutumia rasilimali hadi upeo - Kugawa majukumu - Kukadiria maendeleo - Kuzuia majanga Kigezo cha msingi: kushindwa kupanga ni kupanga kushindwa UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 24 Ni kwa nini kupanga ni muhimu (3) • Kupanga kunahitaji muda na rasilimali lakini kunawakilisha uwekezaji ambao hulipa gawio baadaye • “Ikiwa huna muda* wa kufanya kwa usahihi, ni lini utakuwa na muda* wa kufanya upya?” (Kocha Maarufu wa UCLA wa Mpira wa Vikapu, John Wooden) * au rasilimali UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 25 Hatua za kupanga (1) • Kadiria swala la afya na bainisha viungo vyote vya mabadiliko yanayowezekana (yaani, mawasiliano na mabadiliko ya huduma, sera n.k.) • Fafanua malengo ya mawasiliano • Fafanua na jifunze kuhusu hadhira inayonuiwa/zinazonuiwa • Chunguza mazingira, njia na shughuli zinazofaa zaidi kwa kufikia hadhira iliyonuiwa/zilizonuiwa • Tambua washirika wanaoweza kuwepo na panga ushirika nao • Kuza mkakati wa mawasiliano na fanya rasimu ya mpango UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 26 Hatua za kupanga (2) • Kigezo kikuu cha kupanga ni kufafanua dhamira na malengo kwa ufupi na uwazi • “Ikiwa hujui unakoenda, barabara yoyote itakufikisha huko” (Lewis Carroll – Alice in Wonderland) UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 27 Kuhakiki taarifa iliyoko • Tatizo au swala • Tukio na/au utapakaaji wa tatizo la kiafya • Nani ameathirika (hadhira iliyonuiwa inayowezekana) ikiwa ni pamoja na umri, jinsia, ukabila, hali ya kiuchumi, elimu au kiwango cha kusoma, mienendo sababishi au banifu (zaidi ya vipengele vya kidemografia) • Athari za tatizo kwa watu binafsi na jamii • Asili au hatua za uzuiaji zinazowezekana • Suluhu, matibabu au tiba zinazowezekana UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 28 Je, mashirika mengine yamefanya nini ? • Kujumuisha mitazamo mingine kama vile utetezi wa mabadiliko ya sera au ya kiteknolojia • Wasiliana na makundi haya ili kugundua: - Ni nini ambacho wengine wamejifunza? - Ni taarifa gani ambayo wengine huenda wakachangia katika mpango wako? - Ni nini kingine kinachohitajika? - Ni fursa zipi zilizoko kwa kushirikiana na nguvu za ushirikiano? UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 29 Kufafanua malengo ya mawasiliano • Husaidia kuweka aula miongoni mwa shughuli za mawasiliano zinazowezekana na kutambua ujumbe utakaotumiwa kwa kila moja • Hutumiwa kama mkataba au mapatano kuhusu kusudi la jitihada na husaidia katika kubainisha matokeo ambayo yanafaa kupimwa • Jitihada nyingi za mawasiliano hukosa kufaulu tu kwa sababu malengo asili hayakuwa na busara UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 30 Malengo (1) • Yanayounga mkono dhamira • Yanatia hamasa (yaani, yana matamanio) • Ni ya busara na uhalisi (yaani, yanaweza kufikika) • Yaliyo maalum kwa mabadiliko yanayotamanika, idadi lengwa ya watu, na kipindi cha muda ambacho mabadiliko yanafaa kuchukua • Yanayoweza kupimwa, ili kukuruhusu kufuatilia maendeleo hadi kwenye matokeo yanayotamanika • Yana uratibu wa aula, ili kuelekeza kugawa kwa muda na rasilimali UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 31 Malengo (2) • Malengo hueleza matokeo yanayotamanika wala si hatua zinazohusika katika kuyafikia • Jitihada za mawasiliano pekee haziwezi kufikia malengo yote lakini zinaweza: - Kuunda mazingira yenye kuunga mkono mabadiliko ya mtu binafsi, ya shirika, na ya kijamii kwa kuathiri mitazamo, imani au sera - Kuchangia katika ari ya mabadiliko ya mwenendo yaliyo na upana zaidi kwa kutoa ujumbe unaotia hamasa, kushawishi, na kuwezesha mabadiliko ya mwenendo katika hadhira maalum iliyonuiwa UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 32 Malengo ya uhalisi kwa rasilimali zilizoko • Ni nini kinahitajika ili kufikia malengo ikilinganishwa na kile kilichoko? - Wafanyakazi, watu wa kujitolea, washauri. - Rasilimali za matumizi - Huduma zinazopatikana kutoka kwa asili nyingine zo (k.m., nyenzo zilizoko) - Taarifa kuhusu swala, hadhira iliyonuiwa, jamii, miundo ya vyombo vya mawasiliano , n.k. (Tunahitaji kuufanya utafiti huu?) - Bajeti iliyoko kufadhili jitihada hizi - Muda ulioko kwa kukamilisha utaratibu huu UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 33 Hadhira na vitengwa vya hadhira • Fafanua kwa kutumia sifa bainifu za - Kimwenendo: shughuli zinazohusiana na afya au machaguo - Kitamaduni: ufasaha wa lugha, dini, ukabila, muundo wa kifamilia, hali za maisha, n.k. - Kidemografia: shughuli za kazi, mapato, hadhi ya kielimu, mahali pa kuishi - Kimwili: jinsia, umri, kiwango cha kuwa wazi kwa hatari za kiafya, hali ya kimatibabu - Kisaikografia: mitazamo, msimamo wa maisha na afya, maoni, imani, maadili, n.k. UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 34 Uwekaji vitengwa kwenye hadhira • Kiini cha ufanisi ni kuweka idadi nuiwa ya watu katika vitengwa kwa kurejelea sifa bainifu zinazohusika kwenye mwenendo wa kiafya wa kubadilishwa • Mahali penye mantiki pa kuanzia ni mwenendo wenyewe: linganisha wale wanaoshiriki katika mwenendo unaotamanika na wale ambao hawashiriki na kisha tambua viamuzi vya mwenendo wao. • Watu wawili binafsi huenda wakawa sawa kidemografia, kimaumbile, na kitamaduni, lakini mmoja wao anaweza kuwa tayari anashiriki katika mwenendo unaotamanika na mwingine asishiriki: mmoja yuko kwa hadhira lengwa na yule mwingine hayuko UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 35 Kuweka aula kwa hadhira • Huenda kukawa na zaidi ya hadhira nuiwa moja: - Weka aula - Gawa rasilimali kwa kila mojawapo • Hadhira za pili au za “kufikia” ni zile zilizo na athari kwa hadhira nuiwa ya msingi au zile ambazo ni lazima zifanye kitu ili kusababisha mabadiliko katika hadhira nuiwa ya msingi UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 36 Maarifa kuhusu hadhira (1) • Je, hadhira nuiwa inajuwa nini tayari kuhusu swala ikiwa ni pamoja na kuelewa visivyo? • Je, mitazamo, imani, na utambuzi wao ni upi au vizuizi vyao dhidi ya mabadiliko ni vipi? • Je, hadhira nuiwa iko tayari kwa mabadiliko kwa kiwango kipi? • Ni manufaa yapi ambayo hadhira tayari inahusisha na kufanya mabadiliko yanayotamanika ya kimwenendo? • Je, ni vipengele vipi vya kijamii, kitamaduni, na kiuchumi vilivyo na uwezo wa kuathiri ukuzaji na utekelezaji wa utaratibu? UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 37 Maarifa kuhusu hadhira (2) • Ni lini na wapi (nyakati, mahali, hali ya akili, n.k.) ambapo hadhira nuiwa inaweza kufikiwa? • Je, ni njia ipi ya mawasiliano (k.m., vyombo vya habari, simu, mikutano, mawasiliano ya kielektroni, wavuti, n.k.) hufikia hadhira nuiwa? • Je, watu fulani binafsi (au mabawabu) wanaoyo athari kwa hadhira nuiwa au wanadhibiti mfiko wake? • Mapendeleo ya hadhira nuiwa ni yapi kwa mujibu wa mitindo ya kujifunza, mivuto, lugha, na toni? UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 38 Mazingira, njia, na shughuli (1) • Si mazingira, njia, na shughuli zote huundwa sawa kwa mujibu wa ufanisi wa kufikia hadhira nuiwa • Mahali: je, hadhira nuiwa inaweza kufikiwa kwa ufanisi mkubwa zaidi nyumbani, kazini, wakati wa usafiri, baina ya nyumbani na kazini, n.k.? Je, wana uwezo wa kuchukua hatua katika mazingira hayo? • Wakati: je, ni lini hadhira nuiwa humakinika na kufunguka zaidi kwa ujumbe? • Hadhira inafaa kufikiwa pale ambapo na wakati ule ambapo ni wasikivu na wanaweza kuchukua hatua kwa ujumbe unaotolewa • Je, mazingira fulani huchangia katika kusadikika kwa ujumbe? UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 39 Mazingira, njia, na shughuli (2) • Njia za utoaji wa ujumbe zinazochunguzwa hutofautiana miongoni mwa mandhari mbalimbali na zinabadilika upesi: - Baina ya watu binafsi - Kundi - Kishirika na kijamii - Vyombo vya habari - Vyombo vya habari vya tarakimu ongezi (barua pepe na mtandao) • Njia zinafaa kudhukuriwa kulingana na uwezo wao wa kuweka ufahamu, kuchangamsha hadhira nuiwa kutafuta taarifa/huduma, kuongeza maarifa, kubadilisha mitazamo, na kubadilisha mwenendo UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 40 Chaguo la njia • Je, njia fulani itaweza kufikia hadhira nuiwa, na inaaminika na hadhira nuiwa? • Je, njia fulani inafaa kwa ujumbe? • Je ni idadi ipi ya watu binafsi inayofikiwa kupitia kwa kila njia? • Je ni gharama zipi zinazohusiana na kutumia njia fulani? • Je njia fulani itaweza kuimarisha ujumbe unaotolewa kupitia kwa njia nyinginezo? UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 41 Manufaa ya kuunda ushirika • Kufanya kazi na washirika kunaweza kuzidisha ufikiaji na ufanisi wa ujumbe - Mfiko uliozidishwa kwa hadhira nuiwa - Kusadikika kwa ujumbe kulikozidishwa - Ongezeko katika idadi ya ujumbe ambao unaweza kutolewa - Rasilimali za ziada (zinazoshikika na zisizoshikika) - Ongezeko la utalaamu na tajriba - Msaada ulipanuka wa shughuli za aula - Ufadhili wenza wa matukio na shughuli UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 42 Gharama za kuunda ushirika • Kufanya kazi na washirika kunaweza: - Kuchukua muda mwingi (kutambulishwa na kushirikishwa kwa washirika) - Kuhitaji kubadilisha utaratibu (vitu tofauti vitakuwa na aula tofauti na makubaliano kupitia katika mwafaka huenda yakahitajika - Kusababisha kupoteza kwa “umiliki” (muamana una uwezekano mkubwa wa kugawanywa) • Amua ni unyumbulikaji wa kiasi kipi ambao unao wa kuingiza mshirika bila kukiuka uadilifu wa utaratibu. UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 43 Uundaji wa mpango wa ushirika (1) • Kurasimisha (k.m.f., mkataba ulioandikwa) hutoa kujitolea na uwazi wa kiasi kikubwa zaidi • Wajibu na majukumu ya kila mshirika pamoja na wafanyakazi wake yanafaa kufafanuliwa kwa uwazi • Muundo (uchaguzi wa mwenyekiti, ajenda zilizoandikwa kwa mikutano, ripoti za mara kwa mara) • Uwajibikaji unahitajika na vigezo kukubaliwa kwa ajili ya kuamua ikiwa washirika wanaheshimu kujitolea kwao • Unyumbukaji na mwafaka unahitajika ili kuepuka kupoteza washirika ambao wanaweza kuharibu jitihada UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 44 Uundaji wa mpango wa ushirika (2) • Mafunzo huenda yakahitajika ili kufikisha mchango wa washirika kwenye upeo na kuwafanya kuwa wafanyakazi walio na ufanisi zaidi na /au watetezi wa utaratibu • “Umiliki” ni muhimu: kila mshirika anafaa kuhisi kuwa anacho kiguzo katika muungano na anao wajibu tendaji katika ushirika • Rasilimali za nje zinaweza kutafutwa kutoka nje ya muungano • Vipimo na ratiba zinawezesha upimaji wa maendeleo ya ushirika UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 45 Uundaji wa mkakati ya mawasiliano • Unaolingana na maarifa kuhusu matakwa, mahitaji, maadili, na mfiko wa hadhira iliyonuiwa • Unaoongozwa na utafiti wa kawaida wa mawasiliano na kanuni zilizowekwa za mawasiliano na mwenendo • Unaotulizwa na uhalisi wa vizuizi katika rasilimali na muda wa mwisho wa utekelezaji uliowekwa • Unaowapatia washiriki na washirika wote mwelekeo wa kuendeleza ujumbe na nyenzo thabiti • Vipengele vyote vya utaratibu vinafaa kutangamana na mkakati UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 46 Mpango wa mawasiliano (1) • Vipengele vyote vya matokeo ya mchakato wa upangaji vinafaa kurekodiwa katika mpango wa mawasiliano ulio na upana ambao unachukuliwa kuwa ‘mpango makini’ ambao: - Unaelezea mipango ndani ya shirika (na ndani ya ushirika wowote) - Unaunga mkono na kuthibitisha uhalali wa maombi ya msaada wa kifedha - Unatoa rekodi ya wapi ambapo utaratibu ulianzia - Unaonyesha mageuko/mabadiliko ya utaratibu jinsi muda unavyopita UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 47 Mpango wa mawasiliano (2) • Muhtasari wa kauli ya dhamira kuu, malengo, mikakati na mbinu • Muhtasari wa maarifa ya hadhira iliyonuiwa • Mipango ya kukuza na kujaribu ujumbe na nyenzo • Mipango ya utekelezaji (ugavi, ukuzaji , na utathmini wa mchakato) • Mpango wa utathmini wa matokeo • Kazi pamoja na vipimo vya muda kwa utekelezaji na utathmini UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 48 Sasa hiki hapa ni kiumbe kilichopevuka. Utaona kuwa ukuaji wa kiini na sitoplazimu, pamoja na kile kinachoonekana kuwa rasimu ya kwanza ya mpango wa mkakati. UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 49 Marejeo na shukrani • Wasilisho hili litokana kwa kiasi kikubwa na chapisho “Making Health Communication programmes Work” lililochapishwa katika hali ya kusahihishwa mnamo mwaka wa 2002 na Taasisi ya Kitaifa ya Saratani ya Taasisi za Kitaifa za Afya katika Idara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani (Chapisho la NIH Nambari. 02-5145) • Chapisho lote linaweza kupatikana kutoka kwa NCI kupitia kwa tovuti www.cancer.gov UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD Slaidi 50 Asante Wasilisho hili linapatikana katika: www.uicc.org/curriculum UICC HPV and Cervical Cancer Curriculum Chapter 8.a. Planning health communications for change Joe B. Harford, PhD