TANZANIA COUNCIL FOR SOCIAL DEVELOPMENT (TACOSODE)

Download Report

Transcript TANZANIA COUNCIL FOR SOCIAL DEVELOPMENT (TACOSODE)

Slide 1

TANZANIA COUNCIL FOR SOCIAL
DEVELOPMENT
(TACOSODE)

UTEKELEZAJI WA MRADI WA UWAJIBIKAJI
WA KIJAMII (SAM)


Slide 2

Utangulizi








TACOSODE ni kifupi cha Tanzania Council for Social
Development.
Ni Baraza la Vyama vya Hiari na Maendeleo ya Jamii
lenye hadhi ya Mwanvuli wa Kitaifa.
Awali Baraza lilijulikana kwa jina la National Council for
Social Welfare Service, lililoasisiwa Februari 1965.
Mwaka 1987 mabadiliko ya jina yalifanyika na kubadilika
kuwa TACOSODE. Hii ilitokana na mabadiliko ya
mwelekeo toka Ustawi wa Jamii kwenda Maendeleo ya
Jamii.
Tokea hapo mpaka sasa Baraza linajihusiha na kujenga
uwezo wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), vikundi
vya kijamii (CBOs) na jamii ili iweze kumudu mazingira
yao.


Slide 3

Dira na Dhamira ya Shirika
DIRA


Kuwa na mashirika yasiyo ya kiserikali na vikundi
vya kijamii imara
na vyenye uwezo wa
kusimamia haki za jamii Tanzania bara.

DHAMIRA
 Kuwa na maendeleo endelevu kwa kujenga
uwezo wa rasilimali watu, taasisi na wananchi
kwa njia ya mafunzo, uwezeshaji wa rasilimali na
mashirikiano kati ya wadau mbalimbali


Slide 4

UFUAJILIAJI WA UWAJIBIKAJI WA KIJAMII- SAM
Utangulizi:
TACOSODE ilichaguliwa kuwa mmoja wa Asasi
mwanachama kutekeleza mradi huu wa uwajibikaji

wa kijamii (SAM) kwenye Mkutano Mkuu wa Policy
Forum uliofanyika Mwezi Mei 2011 katika ukumbi wa
Blue Pearl -Ubungo Plaza.


Slide 5

MALENGO YA MRADI
Lengo Kuu
Kufuatilia Uwajibikaji na Utawala bora wa Serikali ili
kuiwezesha serikali kutoa huduma bora na sahihi
kwa wananchi wake.

Malengo Mahususi






Kujenga uwezo wa jamii kushiriki kikamilifu katika
mchakato mzima wa kupanga mipango ya
maendeleo
Kujenga uwezo wa jamii kusimamia na kufuatilia
matumizi ya rasilimali za umma
Kujenga uwezo wa jamii kujua haki ya kupata
taarifa za utekelezaji wa mipango, mapato na
matumizi ya raslimali za umma


Slide 6

UTEKELEZAJI WA MRADI


Mradi wa uwajibikaji wa kijamii (SAM) ulianza kutekelezwa mwezi
September 2011 Mkoani Lindi Halmashauri ya Wilaya ya Lindi
kwenye sekta ya Elimu ya Msingi.

Mradi ulitekelezwa katika hatua zifuatazo:


Utambulisho

Mradi ulianza kwa kutambulishwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri,
Idara ya Elimu ya Msingi, Idara ya Mipango na Idara ya Fedha.


Mafunzo

TACOSODE kwa kushirikiana na Policy Forum waliandaa na kuendesha
mafunzo kwa Asasi wanachama wa TACOSODE pamoja na watendaji wa
Halmashauri (Afisa Mipango, Afisa Elimu, Madiwani na Watendaji wa Mitaa
na Vijiji).


Slide 7

Mafunzo
Mafunzo hayo yalikuwa ya aina mbili: Moja; kujenga uwezo wa
Asasi wanachama na wafanyakazi wa TACOSODE juu ya dhana
na mchakato mzima wa uwajibikaji wa kijamii. Pili; Mafunzo
juu ya uchambuzi wa
takwimu na taarifa mbalimbali
zitumikazo wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa uwajibikaji wa
kijamii.





Mafunzo yote haya yalifanyika Wilayani Lindi,
Mafunzo ya dhana nzima ya SAM ilihusisha wadau 19,
kwa siku 10.

Mafunzo ya uchambuzi wa
takwimu na taarifa
yalihusisha wadau 18, kwa siku 5.


Slide 8

Mchakato wa Utekelezaji SAM
Hatua tano za Mchakato wa Ufuatilaiji wa Uwajibikaji wa Kijamii :1. Kupanga na kugawanya rasilimali (Je kuna kiasi gani cha

rasilimali na zimepangwa kutumika Vipi?)

2.

Usimamizi wa matumizi (Je rasilimali za umma zinatumika

3.

Ufuatiliaji wa utendaji na ufanisi (Je watoa huduma wanafanya

4.

Usimamizi wa uadilifu (Je ni hatua gani zinachukuliwa

5.

Kufuatilia

kulingana na Mpango?)

kazi kulingana na mipango? na huduma zitolewazo
zinakidhi ubora kusudiwa?)

kudhibiti matumizi mabaya ya arasilimali?)

(Je watendaji wanawajibishwa na
vyombo vya usimamizi juu ya utendaji wao?)
usimamizi


Slide 9

Council Implementation Team(CIT)
1. Khamisi Chilinga

:

Mwenyekiti

2. Gaudensia Shada

:

Katibu

3. Angelina Mrangila

:

Mweka hazina

4. Mahmoud Chembera

:

Mjumbe

5. Paulina Mangunguru

:

Mjumbe

6. Scholastica Nguli

:

Mjumbe

7. Abdallah Ndwango

:

Mjumbe


Slide 10

Matokeo ya uchambuzi
Kupanga na kugawa rasilimali
Halmashauri ya wilaya ya Lindi hupanga mipango
yake kwa kuzingatia mpango mkakati wa wilaya
wa miaka mitano, vipaumbele na sera za taifa. Vile
vile takwimu zilionyesha kuwa mipango huanzia
ngazi ya jamii kwa kutumia zana shirikishi ya
O&OD.
1.

Baada ya kutembelea kata mbalimbali, hakukuwa
na ushahidi wa kutosha kudhihirisha hili.
Kinachofanyika kwenye baadhi ya maeneo ni kuwa
mipango ya miaka ya nyuma huhuishwa na kuingia
kwenye mpango wa mwaka mpya wa fedha.


Slide 11

Vyanzo vya Mapato Halmashauri 2009/2010
 Halmashauri ya wilaya ya Lindi ilipanga kutumia Tshs
11,877,627,900/-, katika bajeti yake, ambapo miradi
ya maendeleo ilipangiwa Tshs 3,423,750,900/= na
Matumizi ya kawaida (Re current)
Tshs
8,453,877,000/-. Katika bajeti hiyo mchango wa
Halmashauri ulipangwa kuwa Tshs. 475,753,000/=
ambayo ni sawa na 4% ya bajeti yote na asilimia
96% ya bajeti walitegemea kuipata kutoka serikali
kuu. (MTEF 2009/10-2011/2012 pg 10).
 Hii inaonyesha uwezo mdogo wa Halmashauri katika
kukusanya mapato na kuweka uwalakini wa utekelezaji
wa mipango yake pindi ruzuku inapochelewa/kuto
tolewa kabisa.


Slide 12

Vipaumbele
vya
halmashauri
kwa
mwaka wa 2009/2010
Elimu ya msingi
Kilimo
Maji
Afya
Miundombinu
Utoaji huduma
Utawala bora

Vipaumbele vya Idara ya
Elimu
Msingi
mwaka
2009/2010
 Kuongeza idadi ya watoto
wanaoandikishwa
na
wanaopata
nafasi
ya
kujiunga na elimu ya
msingi
 Kuboresha mazingira ya
kufundishia na vifaa vya
kufundishia
 Kudumisha kiwango cha
elimu kwa kuwawezesha
walimu kutoa elimu bora


Slide 13

Miradi ya Maendeleo ya Elimu Msingi (MMEM)
Elimu ya msingi ni sekta
iliyotajwa
katika
Mpango
Mkakati (SP) na Mpango wa
Wilaya wa kati MTEF kuwa ni
miongoni mwa vipaumbele
muhimu, lakini mgawo wa
fedha ya utekelezaji wa miradi
ya maendeleo (MMEM) ni
mdogo ukilinganisha na idara
zingine
kwani
ni
Tshs
105,816,000/- sawa na 3% tu
ya
mgawo
wote
wa
Halmashauri
kwa
mwaka
2009/2010 zilitengwa.


Slide 14

Mapokezi ya Fedha za Miradi ya Maendeleo
• Fedha za miradi ya Maendeleo katika wilaya huja kwa
kuchelewa na pungufu, lakini pamoja na kupokea
fedha pungufu ya ile iliyoidhinishwa, Halmashauri
ilitumia fedha hizo chini ya kiwango kwa miradi mipya
na umaliziaji wa ujenzi.
– Mfano Umaliziaji wa nyumba za walimu shule za
msingi Mnyangara, Luhokwe na Lihimilo.
– Baadhi ya miradi iliyopangwa kumalizika kwa
mwaka
huo
haikumalizika
ingawa
fedha
zilipokelewa, mfano umaliziaji wa nyumba za
walimu shule za msingi Kinyope, Narwadi, Litipu,
Malugo, Mbuta na umaliziaji wa darasa
shule ya
msingi Muungano.


Slide 15

• Utofauti wa fedha iliyopelekwa na Halmashauri katika
ujenzi/umaliziaji wa miradi kwenye shule husika
hailingani na taarifa ya fedha iliyotolewa na
Halmashauri.
– Mfano Shule ya Msingi Mtua Ilitengewa Tsh.
1,292,127/- na Halmashauri kukamilisha ujenzi
nyumba ya mwl. Fedha iliyopokelewa site ni Tsh
1,000,000/- tu.
– Nyangao shule ya msingi: Fedha iliyotengwa ni
Millioni 60, iliyotolewa na H/W kwa Mkandarasi ni
Sh.42,000,000/- tu na ilitumika yote. Lakini taarifa
ya ufunguzi wakati wa mwenge inaonyesha ujenzi
umegharimu millioni 78, ambazo Tsh. 22,
121,600/- zilitolewa kitengo cha Wanafunzi
wasioona wanaosoma shuleni hapo.


Slide 16

Masuala ya kufanyia Ushawishi


Ukosefu Mkubwa wa vyoo vya walimu na wanafunzi
katika shule za msingi wilayani Lindi.
 Hili
limejitokeza
katika
maeneo
yote
yaliyotembelewa Mfano Shule ya Msingi Mtua
hakuna vyoo kabisa.
 Walimu hujikimu majumbani kwao au kwa majirani
na wanafunzi hupata huduma hiyo porini.
 Shule ya Msingi Mihogoni hakuna vyoo vya walimu
– kilichopo ni kibovu hakifai kwa matumizi.
 Choo cha wanafunzi ni kibovu hivyo kuhatarisha
maisha ya watoto wanaosoma shuleni hapo.


Slide 17

 Makato ya Kodi ya nyumba kwa Walimu hayalingani na
ubora wa nyumba hizo
 Yapo malalamiko ya walimu kukatwa kodi ya nyumba kwa
6% ya mshahara jambo linalopelekea baadhi ya walimu
kuzihama nyumba hizo na kwenda uraiani ambako
wanapanga kwa bei nafuu kulinganisha na zile za serikali.
 Lakini pia nyumba hizo hazina ubora ukilinganisha na
makato hayo. Mfano Nyumba za walimu Nyengedi hazina
vyoo kabisa na bado mwalimu huyo hukatwa kodi ya
nyumba kwa mwezi.
 Nyumba zingine zina nyufa kubwa na hazikujengwa kwa
kuzingatia viwango vya ujenzi.
 Suala hili lilipelekwa Ofisi ya Mkurugenzi na CIT Team na
kukiri kuwa malalamiko hayo yapo na kutolewa majibu kuwa
limeundiwa tume ya kufuatilia makato hayo na kuangalia
jinsi ya kufanya kupunguza makato hayo sio kwa walimu tu
hata na kwa wafanyakazi wengine wa Halmashauri


Slide 18

Ujenzi wa Mabweni shule ya watoto wenye
Mahitaji Maalum Nyangao na Matumizi ya fedha
ya watoto wenye mahitaji maalumu
 Fedha iliyotengwa katika MTEF 2009/2010 sh. 60 mil lakini
zilizotolewa kwa Mkandarasi ni sh 42,000,000 ambayo
haikutosheleza mahitaji hivyo kulazimika kuchukua fedha
kutoka kitengo cha watoto wasioona kiasi cha Tsh. 22,
121,600/-.
 Halmashauri ifanye mchakato wa kurejesha fedha ya
Kitengo cha wanafunzi wasioona kiasi cha Tsh. 22,
121,600/- ambazo Halmashauri ilitumia.

 CIT ifanye ushawishi na utetezi ili kuhakikisha fedha
iliyotolewa kitengo cha wanafunzi wasioona inarejeshwa.


Slide 19

Hali ya Mazingira ya Shule
 Halmashauri hainabudi kujenga mazingira mazuri
kuwezesha walimu kufanya kazi kwa utulivu na
pia wanafunzi kusoma vizuri. Mazingira hayo ni
pamoja na uwepo wa nyumba bora na Vyoo
vilivyokamilika na vya kutosheleza. Zifuatazo hapo
chini ni picha za vyoo katika baadhi ya Shule na
nyumba za walimu katika Halmashauri ya Lindi


Slide 20

Hali halisi ya choo cha Walimu & Wanafunzi Shule ya
Msingi Mtua


Slide 21

Hali halisi ya choo cha Wanafunzi na Walimu
S/Mihogoni.


Slide 22

Hali halisi ya vyoo na Nyumba za walimu

Choo cha moja ya nyumba za walimu
S/M Nyegendi.

Nyumba ya Mwl. S/M Mtua Kenchi
hazijashikizwa na ukuta


Slide 23

Shule ya Msingi Nyangao & Bweni la Wavulana.


Slide 24

Hali halisi ya bweni la thamani ya Tsh. 39mil
lililokamilika June 2011.


Slide 25

Imeandaliwa na TACOSODE kwa
Ushirikiano na CIT –Wilaya ya Lindi
April, 2012.