VIFAA VYA KUFUNDISHIA

Download Report

Transcript VIFAA VYA KUFUNDISHIA

Nini maana ya vifaa vya kufundishia?

   Ni kitu chochote kinachotumiwa na mwalimu /mwanafunzi kwa ajili ya kushajihisha usomeshaji na kujifunza.

Vipo vifaa ambavyo mwalimu ndio anatumia zaidi (ubao, projector, nk) Vipo ambavyo mwalimu na mwanafunzi wanatumia kwa pamoja (vitabu vya kiada)

 Unafikiri sifa gani zinahitajika kwa Kifaa cha kufundishia kilichobora na kitakachopelekea lengo la kujifunza kufikiwa?

 Angalia kwa makini vifaa vifuatavyo kisha toa maoni yako.

AINA ZA MANENO NOMINO KIVUMISHI KIELEZI KITENZI KIWAKILISHI

Aina za sentensi Sentensi sahili Sentensi shurtia Sentensi ambatano Sentensi changam ano

            FISI AADHIBIWA Hapo zamani katika mbuga ya Rijeni wanyama wadogo walikutana kwa siri kujadili uovu wa Fisi. Walikutana kwa siri kwa sababu walijua wanyama kama Simba, Chui na Fisi walikuwa na hamu kubwa ya kuwashambulia na kuwala. Swala alikuwa kiongozi wa mkutano na akawaambia wenzake, “Jamani, uonevu umezidi. Juma lililopita watoto wawili wa Kongoni waliliwa na Chui, tena Chui alisema hakushiba. Alitaka sana amshike Kongoni amle, lakini Kongoni aliwahi kukimbia. Juzi mwanangu Ameliwa na Fisi. Nilimpiga teke jichoni lakini akataka kunitafuna, nikakimbia, sasa tufanyeje?” Basi wanyama walijadili kwa uchungu na kwa muda mrefu. Wote walitaka sana Chui na Fisi wauawe haraka. Tatizo lao kubwa lilikuwa jinsi ya kuwauwa. Wengine walishauri waovu wale wategewe mitego ya kamba baadaye wapofuliwe. Hata hivyo ilionekana ni hatari bado. Hatimae sungura akatikisa masikio yake na kusema, “Kuwauwa niachieni mimi. Nipeni siku saba nitawaeleza na kuwaonesha nitakachofanya.” Basi mkutano ukafungwa na kumkubalia Sungura afanye kazi hiyo. Usiku ulipoingia Sungura alikoka moto nje ya nyumba yake. Moto ulipokolea vizuri akatia jiwe moja ndani ya ule moto. Jiwe hilo lilikuwa na ukubwa wa mpira wa tenisi. Sungura akaongeza kuni mekoni halafu akaenda kumtafuta Fisi pangoni mwake.

Sungura alipofika mlangoni mwa pango akasema, “hodi kwa mzee Fisi!” Fisi alifurahi moyoni, kwa sababu alijua ile sauti ya Sungura na alijua kuwa Sungura angeweza kuwa chakula chake. Fisi hakujibu haraka. Kwa hiyo Sungura akasogea mlangoni na kubisha tena hodi. Hapo ndipo Sungura alipojikuta makuchani mwa Fisi! Sungura akaona kifo waziwazi .Sungura akamwambia “rafiki yangu mzee Fisi vipi leo? Nakuletea habari nzuri halafu unanikamata!” Fisi akasema mimi nina njaa ya siku nne halafu uniletee habari nzuri gani? “Wewe ni rafiki yangu” Sungura akampoza , “hata kama utanila hutashiba. Mimi nimekuja nikukaribishe kwangu. Huko nyama ni tele.” Fisi alifurahi na kucheka huku akimwachia Sungura . “Haya ongoza njia. Tena uongeze mwendo, sio ule mwendo wako wa sisimizi”. Sungura na Fisi walifika kwa Sungura huku mate yanamtoka Fisi mdomoni kwa hamu ya nyama. Hapo Sungura akapanga vitimbi vyake akasema, “mzee fisi nyama zipo nyingi lakini hizi ni nyama za tambiko. Kwa desturi za kwetu mnofu wa kwanza nitakulisha mimi mwenyewe, mradi ulale chali na ufumbe macho”. Baada ya hapo nyama nyengine utakula kwa mikono yako.” Kabla Sungura hajamaliza Fisi alikwisha lala chali, na kufungua mdomo na pia kufumba macho.

Sungura alicheka kimoyomoyo akatwaa kibanio, akabana lile jiwe la moto na kulitumbukiza mdomoni mwa Fisi. Kwa kuwa Fisi alikuwa amejiandaa kumeza nyama , alilimeza jiwe haraka sana. Looo! Fisi aliungua koo, kifua na tumbo. Fisi alibiringika akilia sana na kujitupa huku na huko hadi akakata roho.

(Kutoka, Kiswahili 2 - Kidato cha Pili, Taasisi ya Elimu, Oxford University Press, Dar Es Salaam, 1996, uk 5-6.)

       Vifahamike Visomeke Visikike Vionekane (viwe vikubwa vya kutosha) Viwasilishe dhana iliyokusudiwa Viendane na maadili ya jamii Vilingane na viwango vya wanafunzi

      Visiwe na athari kwa wanafunzi Visimjenge khofu mwanafunzi (kutokueleweka,nk) Vimsaidie mwanafunzi kujiamini,vimhamasishe Visiwe na tafsiri nyingi/dhana nyingi kwa wakati mmoja Vizingatie tofauti ya wanafunzi katika ufahamu/ugumu Vichorwe vizuri vivutie (attractive)

       Picha za vitu halisi Vitu halisi Michoro (drawings) Vivuli vya mazungumzo au habari Redio na vinasa sauti Ramani Chati na vielelezo

      Kadi zenye malekezo Vitabu vya kiada Ubao na chaki Vipande vya habari vilivyotayarishwa na mwalimu, kutoka magazetini, vitabuni,nk Projecta computer

      Kurahisisha ufahamu kwa wanafunzi Kuwachangamsha wanafunzi Kuwashirikisha wanafunzi ,kutumia akili zao kwa kuzalisha mawazo yatokanayo na vifaa vinavyotumika Kuhifadhi muda Vinapelekea Kumbukumbu ya muda mrefu Vinasaidia maneno (support verbal instructions)

 Vinapelekea kuifanya dhana kuonekana (verbal idea to be concrete)

  Ref. Mbumda F. (1996)

Mbinu za Kufundisha lugha ya Kiswahili

Tomlison Brian (2004)

Material development in language teaching